Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Wewe ndio utuambie ni makundi gani yameanza baada ya 2001. Pia hata kama yameanza baada ya 2001, haibadilishi maana ya kwamba hayo makundi yanafungamana kwa kiasi kikubwa na imani ya kiislam, hasa JIHAD.
Usiwe unakurupuka dogo , fuatilia hayo makundi aliyotaja hapo juu .
 
Hawa watu walisumbua sana Mkiru na kwa kweli mfumo mzuri wa usalama wa nchi(Jeshi na Polisi,UST,MI) ulisaidia kuikoa nchi na mikono ya magaidi
Ulihitajika ukatili mapemaaa. Ingawa Zitto Kabwe na wenzie waliingiza siasa na kuubeza.
Sasa kungekwa na kilio kikubwa na makaburi yasiyo idadi toka Lindi, Rufiji, Kibiti, Mkuranga, Dar, hadi Tanga.
Wanasiasa uchwara wazingatia matumbo ni watu hatari sana.
 
Ulihitajika ukatili mapemaaa. Ingawa Zitto Kabwe na wenzie waliingiza siasa na kuubeza.
Sasa kungekwa na kilio kikubwa na makaburi yasiyo idadi toka Lindi, Rufiji, Kibiti, Mkuranga, Dar, hadi Tanga.
Wanasiasa uchwara wazingatia matumbo ni watu hatari sana.
Wanasiasa sio wa kuendekeza hasa kwenye military operations
 
 
Vita kuu ya kuuchafua Uislamu duniani ni DISINFORMATION.

Mwandishi wa makala hii analipa huu upupu alioumwaga. Hajaanza leo. Na analipwa na watendaji wa wasio waaminifu, wavuta bangi.

Ndio maana nimeuuliza mwanzoni tu.

Huu ujumbe wa makala unaolenga kuufungamanisha uislam na ugaidi.

Je, HIVI MAGAIDI WENYEWE NDIO WANAOJIFUNGAMANISHA NA UISLAM au WAANDISHI NDIO WANAOFUNGAMANISHA UGAIDI NA UISLAM?

Tuseme nchi hii kuna ugaidi wa kutengenezwa. False Flag Terror.

Tatizo la nchi la nchi yetu ni ubaguzi wa kidini tu hakuna cha ugaidi wa Waislam na Uislam.

......ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.


Nitaweka threat inayojitegemea waraka wa waislam kwa serikali ukiitahadharisha serikali iache kuwalea waandishi wote wa kikundi hichi kinachofadhiliwa kuuchafua uislam.

Kama serikali haina mkono wake tunahitaji wamtafute azori ili atueleze ukweli wa mambo
We nae tutolee huu ujinga wako na mapovu Kila comment bwana.

Kila siku mnakuja na jambo hilo hilo la uislamu unachafuliwa. Kwa kitu kipi cha maana mlichonacho hadi dini yenu ichafuliwe?

Ni swala la kuamini (Imani )tu? Yani mtu akibadili dini na kuwa muislamu,hiyo itaniathiri vipi Mimi nisiye muislamu?

Mfano Mimi nimekaa Zanzibar ambako Kuna uislamu zaidi ya 90% ,hiyo Ina athari Gani kwangu nisiye muislamu? Mbona maisha yanaenda vile vile ?

Huu udwanzi wa kulalamika "uislamu unachafuliwa " mnatuchosha. Huo uislamu una nini cha maana hadi upigwe vita enyi wanafiki?
 
𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐠𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐲𝐚 𝐀𝐧𝐬𝐚𝐫 𝐚𝐥-𝐬𝐮𝐧𝐧𝐚.

- 𝐍𝐣𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐛𝐢𝐭𝐢 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐥𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐲𝐚 𝐂𝐚𝐛𝐨 𝐃𝐞𝐥𝐠𝐚𝐝𝐨.

- 𝐖𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐨𝐤𝐨𝐭𝐚 𝐦𝐢𝐢𝐥𝐢 𝐧𝐚 𝐯𝐢𝐜𝐡𝐰𝐚 𝐯𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞𝐧𝐢.

𝐒𝐄𝐇𝐄𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝟬𝟭:

Tarehe 20 mwezi huu wa tano, waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Dkt. Stergomena Tax analiambia bunge kuwa hali ya usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji bado haitabiriki.

View attachment 3003798

Kwa maneno machache bado hali si shwari na sababu ni uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Ansar Al-Sunna ambacho kinafanya mashambulizi huko nchini Msumbiji, jimbo la Cabo Delgado linalopakana na mipaka ya kusini mwa Tanzania.

Hivyo ni bayana, kama kikundi hiki bado kinahema, basi hatuna uhakika wa usalama wetu huko mpakani. Waulize wakazi wa vijiji vya mpakani, Kitaya na Michenjele, huko halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara juu ya USIKU ule.

Usiku huo wa tarehe 14/10/2020, giza halikuja mpweke kwenye ardhi yao bali liliambatana na wageni wasiowatarajia.

Ikiwa ni majira ya saa moja, wanatahamaki wamo katikati ya mashambulizi ya kundi kubwa la watu wenye silaha za moto.

View attachment 3003799

Watu wanakimbia huku na kule wakipiga mayowe ya hofu. Wavamizi wanachoma nyumba, magari, zahanati na pia ofisi ya kata.

Sekeseke la zaidi ya nusu saa. Kifo ama uhai.

Hali kuja kutulia, watu wanatoka walikojificha na walikokimbilia, wanakuja kuokota miili ya wenzao waliopigwa risasi na wengine waliochinjwa kama kuku.

Lakini mbaya, wanabaini wapendwa wengine hawapo. Wamebebwa wakaongozana na 'mabwana' wale kurudi huko walikotokea. Wengi wao wakiwa mabinti wa makadirio ya miaka 14 mpaka 20.

(pichani ni mwanaume aliyepoteza mke na mtoto wake wa kwanza)

View attachment 3003801


Baada ya wiki moja kupita, siku ya Alhamis tarehe 22 Oktoba, ndo' aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Nyakoro Sirro anasimama mbele ya vyombo vya habari na kusema tukio lile lilifanywa na magaidi waliovuka mpaka kutoka nchini Msumbiji.

View attachment 3003822

Magaidi hao walikuwa 300 kwa idadi na wamefanya uhalifu ikiwemo mauaji. Baadhi wakakimbia na wengine wakakamatwa wanaendelea na mahojiano. Anasema lengo ni kupata mtandao wote wa magaidi.

Mtandao ulioanzia kule MKIRU (Mkuranga, Kibiti & Rufiji).

Kwa mujibu wa kamanda Sirro, wale Ansar al-sunna waliopo Msumbiji leo hii jimbo la Cabo Delgado, ambao ndo' wanamfanya waziri Stergomena Tax kusema kuwa usalama hautabiriki mpakani mwetu na Msumbiji, mtandao wao ulianzia hapa nchini mkoa wa Pwani.

Ila ni kweli Pwani tu? Kuna mahusiano gani na kwanini tena jimbo la Cabo Delgado mpaka leo hii? Mbinu za hawa magaidi ni zipi? Jeshi la SADC na Rwanda wamefikia wapi? Hali ya sasa ipoje na Rwanda ananufaikaje na mgogoro huu?

Ikumbukwe ripoti ya hivi karibuni, tarehe 17 Aprili 2024, kutoka gazeti la serikali ya Msumbiji, 'Boletim da Republica' imetolewa orodha ya watu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kushirikiana na kikundi hiki cha ugaidi, miongoni mwao wametajwa watanzania wawili; bwana Ally Yusuf Liwangwa (47) kutoka Dar es Salaam na bi. Safina Maulana (36) kutoka Mtwara.

View attachment 3003806

Sasa turudi kwenye siku ile ya tarehe 5, Oktoba 2017. Siku ya kwanza kabisa risasi kurushwa hewani kwa jina la Ansar al-sunna.

Siku hiyo katika mji wa pwani - Mocimboa de Praia - jimbo la Cabo Delgado, mambo yanabadilika ghafla katikati ya usiku na alfajiri.

View attachment 3003807

Kuanzia saa saba ya usiku, kundi la watu wanaokadiriwa thelathini kwa idadi wakiwa na silaha za moto na baridi, wanavamia mji huu wakilenga vituo vya wanausalama.

Mpaka kufikia saa kumi alfajiri, vituo vitatu ambavyo ni Mocimboa district police, kituo kidogo eneo la Awasse na kituo cha polisi cha maliasili na mazingira vinaripoti kushambuliwa na kutokea majibizano ya risasi.

View attachment 3003808
View attachment 3003814

Msemaji wa jeshi la Polisi, kamanda Inacio Dina (pichani), anawaambia waandishi wa habari mashambulizi hayo yamepelekea vifo vya maafisa polisi wawili na wavamizi watatu lakini ripoti zinasema watu 14 walifariki na pia vituo viliripoti kupotelewa na silaha.

View attachment 3003811

Wavamizi hao walikuwa wanazungumza lugha ya Kireno, Kiswahili na Kimwani. Hiki Kimwani ni lugha ya watu wa pwani ya eneo hili.

Kamanda anasema pia wamefanikiwa kuwakamata wavamizi kadhaa na hao watasaidia kupata taarifa zaidi ya wavamizi wenzao.

Kamanda anapoulizwa kuhusu mafungamano ya wavamizi hao na waislamu wenye itikadi kali mathalani Al-shabab wa kule Somalia, anasema ni mapema sana kusema hivyo. Watu hao kutumia 'local languages' za hapa Msumbiji kunamaanisha ni watu waliokulia hapahapa.

View attachment 3003815

Na hili linatukumbusha miezi sita nyuma ambapo redio ya taifa, Radio Mozambique, iliripoti kukamatwa kwa wanaume watatu wanotuhumiwa kuwa na 'connection' na Al-shabab.

Wanaume hao walikuwa wanawakataza watu kwenda vituo vya afya vya serikali na pia kuwapeleka watoto wao shule.

View attachment 3003816

Lakini baadae walikuja kuthibitika hawana mahusiano yoyote na Al-shabab ya Somalia japo wakaazi walikuwa wanawaita jina hilo, hivyo wakaishia kushikiliwa kwasababu ya kusababisha mashaka ya usalama.

Kamanda Inacio anawaondoa hofu wananchi akisema kikosi maalum cha kupambana na ugaidi kipo kazini na hivyo hali ya usalama itakomaa hivi punde.

Lakini tofauti kabisa na anachosema, huu ndo' unakuwa mwanzo rasmi wa mfululizo wa mashambulizi na mauaji katika jimbo la Cabo Delgado mpaka kuja kuvuka mpaka wa Tanzania.

View attachment 3003818

Kabla ya mwezi Oktoba kuisha, 'mabwana' wanamjibu kamanda kwa mashambulizi mawili katika kijiji cha Maluku na karibu na kijiji cha Columbe.

Mwezi unaofuata (Novemba) tarehe 29 wanavamia vijiji vya Mitumbate na Maculo. Wanaharibu kanisa na pia wanachinja watu wawili.

View attachment 3003819

Tarehe 13 January 2018 wanaingia mji wa Palma na kumwaga risasi sokoni na kwenye ofisi ya serikali. Watu watano wanakufa.

Tarehe 12 March, wanavamia kijiji cha Chitolo na kuchoma nyumba hamsini pia wanaua wakazi. Na kwa siku tatu mfululizo 20, 21 na 22 mwezi Aprili wanavamia vijiji kadha wa kadha wakiua na kuteka watu.

View attachment 3003823

Ni mwezi unaofuata, Umoja wa Afrika (AU) unathibitisha ripoti ya gazeti la Afrika Kusini iliyosema kuna wapambanaji wa Islamic State wamekwishaingia ndani ya Msumbiji, ripoti ambayo serikali ya Msumbiji ilikuwa inapingana nayo hapo awali.
View attachment 3003826
Na kilichofuatia baada ya hapo, ndo' hali ikawa mbaya zaidi. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huo 2019, watu zaidi ya arobaini na sita wakaripotiwa kuuawa kwa risasi na kuchinjwa kama kuku ikiwemo watoto wadogo.

View attachment 3003824

Achilia mbali nyumba lukuki ziliishia kuchomwa moto, watu kujeruhiwa na wengine kutekwa.

Si polisi, si jeshi la Msumbiji (FDS) wote wako hoi.

Mabwana hawa waliwavua nguo, kila mtu akaona uchi wao. Namna walivyo duni kwenye vifaa na mafunzo, na namna walivyo 'corrupt'.

View attachment 3003828

Wananchi wanasema mara kadhaa wameshuhudia wanajeshi wakikimbia eneo lao la ulinzi muda mfupi kabla ya eneo hilo kushambuliwa na magaidi. Wengine wanaiba mitumbwi ya wananchi ili wakimbie kujinusuru.

Kwa kaliba hii, mashambulizi yanazidi kutiririka, magaidi wakiamua wachinje ama wakatekate kama kuni (dismembering).

Zoezi hilo linaenda mpaka mwishoni mwa mwaka 2019 ambako serikali ya Msumbiji inakiri kuhitaji msaada, wamezidiwa.

Kwa kupitia FDS wanawekeana mkataba na jeshi la mamluki (mercenary) Wagner Group la nchini Urusi, na kwa mara ya kwanza kabisa mapema ya mwezi Oktoba mwaka 2019, mashambulizi ya kwanza ya FDS wakishirikiana na Wagner Group yanashika hatamu na yanaleta mafanikio.

View attachment 3003830
Wanawakimbizia magaidi huko misituni na wanafanikiwa kukamata watu makumi kwa makumi walokuwa wanasafiri kutoka jimbo la Nampula kwenda kuongeza nguvu ya magaidi huko jimbo la Cabo Delgado.

Lakini nguvu hii ya soda haikuchukua hata mwezi. Magaidi wanajibu kwa mtindo wa mashambulizi ya kushtukiza (ambushing) na FDS wanapoteza wanajeshi ishirini huku Wagner wakipoteza wanajeshi saba.

Mwezi wa kumi na moja, FDS wanapoteza tena wanajeshi kadhaa huku Wagner wakipoteza wanajeshi watano.

View attachment 3003832

Kipigo hiki kinapelekea pande hizi mbili, FDS na Wagner Group, kuingia kwenye mgogoro. FDS wanailaumu Wagner kutokuwaheshimu maafisa wao na huku Wagner wanalaumu jeshi la FDS pamoja na raia kuwa 'undiscplined'.

Hivyo oparesheni inafeli.

Wagner wanaondoka zao na katika ombwe hili, mkuu wa jeshi la Polisi, kamanda Bernadino Rafael, anaona afanye jambo upesi ili kujiimarisha kiusalama.

Anawasiliana na bwana Lionel Dyck, mkurugenzi wa jeshi binafsi toka nchini Afrika Kusini, Dyck Advisory Group (DAG), ambayo inahusika na utoaji wa vifaa na wataalamu wa mapambano ya kivita.

View attachment 3003837

Wanaweka makubaliano ya kupatikana kwa helikopta sita za vita na pia msaada wa anga kuwakabili magaidi.

Kwa muda huo 2020, hapo Msumbiji kulikuwa na helikopta moja tu ya combat, Russian-built MI-8, tena waliyopewa kama msaada na Rais Putin mwaka 2017.

View attachment 3003840

DAG wanaanza oparesheni yao April, 2020, wakikatiza anga la Msumbiji kupambana pembeni ya wanausalama.

View attachment 3003855

Lakini misheni yao ikiwa imebakiwa na wiki mbili tu kumalizika, linatokea shambulizi la mji wa Palma.

Shambulizi kubwa la kigaidi kupata kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa Afrika.

Watu takribani 1,200 - 1,400 wanauawa ndani ya siku moja. Maiti zinazagaa barabarani. Mamia ya watu, ikiwemo watoto, wanaokotwa wakiwa hawana vichwa.

View attachment 3003862

Shambulizi hizi linashtua jumuiya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC), na sasa linaazimia kufanya kitu upesi kabla hatujaipoteza nchi ya Msumbiji mazima.

View attachment 3003933

Na Rwanda naye habaki nyuma. Anaingiza miguu yake eneo hili akidai kuisaidia Msumbiji kupambana na ugaidi ni njia mojawapo ya kujihakikishia usalama wake kama nchi.

View attachment 3003866

Lakini hana interests zingine hapa?

Kama hapana, je vile vikao vyake na raisi wa Msumbiji, Felipe Nyusi, pembeni ya mkurugenzi wa TotalEnergies, bwana Patrick Pouyanné, vinatoa ujumbe gani?


Ikumbukwe shambulizi hili la mji Palma lilitokea karibu na mradi mkubwa wa dola 'mabilioni' ulio chini ya kampuni ya kifaransa ya TotalEnergies na kupelekea kampuni hiyo kufunga shughuli zake kwa muda usiojulikana.

View attachment 3003938

Lakini yote kwa yote, Msumbiji imefikaje hapa? Intelijensia yake ililala wapi? Hawa magaidi ni kina nani na wanataka nini hapa Cabo Delgado?

Kuna mahusiano gani na mambo ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji)?

Habari inaanzia kule Mombasa, Kenya, miaka 12 ilopita...

𝐓𝐔𝐍𝐆𝐎𝐉𝐄 𝐒𝐄𝐇𝐄𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝟬𝟮:
Very interesting brother
 
Hayo makundi ndio maana unatakiwa kusoma origin yake ni shambulio la Marekani .. Lile kundi lililohusika ndio wakaja na haya madogo ili kukamata wahusika real .

Osama ni zao la USA , ameua ndugu zake huko Iraq mpaka akaja kugombana na hao USA .
Kwa nini huyo Osama na Shehe Rogo wanapewa heshima kubwa miongoni mwa waislamu? Tena waislamu wengine wanaenda mbali na kuwabandika picha zao hadi kwenye magari hao waislamu wenye misimamo mikali kama Osama na Rogo.

Tatizo lenu nyie waislamu ni unafiki uliopitiliza. Mtu (miongoni mwenu) akifanya mabaya na jamii ikakemea, nyie mnatokeza mbele na kukemea pia kwamba "huyu hausiki na uislamu" ,"huyu siyo muislamu" "hakuna uislamu wa hivyo" "huyo haujui usilamu".

Juzi hapa mmemkataa Shehe wenu maarufu NURDIN KISHKI na wengine kumuita kafiri na mzushi,haujui uislamu kisa amesema ni ruksa katika uislamu kutafuta utajiri kwa kutumia majini.

Ni kwa nini baadhi yenu wanapokengeuka na kutenda yasiyofaa mnawatoa katika uislamu?

Uislamu unawezaje kuexist bila watu? Hao Boko Haram kule Nigeria wanatesa na kuua watu kwa jina la uislamu lakini humu mnautetea uislamu auhusiki unachafuliwa. Uislamu ni Vacuum? Si ili kuwe na uislamu inabidi kuwe na waislamu?

Kwanza mnatuharibia Uzi mnapojistukia na kujihami kwa kuanza kuutetea uislamu wakati mleta mada hajauongelea kabisa uislamu kwenye Uzi wake. Toeni huu utumbo wenu asee!!
 
Kwa nini huyo Osama na Shehe Rogo wanapewa heshima kubwa miongoni mwa waislamu? Tena waislamu wengine wanaenda mbali na kuwabandika picha zao hadi kwenye magari hao waislamu wenye misimamo mikali kama Osama na Rogo.

Tatizo lenu nyie waislamu ni unafiki uliopitiliza. Mtu (miongoni mwenu) akifanya mabaya na jamii ikakemea, nyie mnatokeza mbele na kukemea pia kwamba "huyu hausiki na uislamu" ,"huyu siyo muislamu" "hakuna uislamu wa hivyo" "huyo haujui usilamu".

Juzi hapa mmemkataa Shehe wenu maarufu NURDIN KISHKI na wengine kumuita kafiri na mzushi,haujui uislamu kisa amesema ni ruksa katika uislamu kutafuta utajiri kwa kutumia majini.

Ni kwa nini baadhi yenu wanapokengeuka na kutenda yasiyofaa mnawatoa katika uislamu?

Uislamu unawezaje kuexist bila watu? Hao Boko Haram kule Nigeria wanatesa na kuua watu kwa jina la uislamu lakini humu mnautetea uislamu auhusiki unachafuliwa. Uislamu ni Vacuum? Si ili kuwe na uislamu inabidi kuwe na waislamu?

Kwanza mnatuharibia Uzi mnapojistukia na kujihami kwa kuanza kuutetea uislamu wakati mleta mada hajauongelea kabisa uislamu kwenye Uzi wake. Toeni huu utumbo wenu asee!!
Hamna kitu kama hicho , Abdul rogo kauliwa kwa shambulio alikuwa ni mwanaharakati , gari alilokuwa amepanda na fimilia yake limeshambuliwa , unataka kusema nn kma sio kushambulia fmilia nzima. Ameuliwa akiwa mshukiwa wa kufadhili ugaidi sio kwamba alishikwa na hatia ila kashambuliwa kwa akiwa katika gari kama Tundu LISSU .

Ndio maana unatakiwa kufuatilia haya mambo , uislamu kumtukuza shekhe au mtu fulani ni ''SHIRKI'' hata awe nan duniani ...


Shekhe ndio nan ? Huku hamna kumtukuza kiongozi zaidi ya QUran na sunnah , ukienda kinyume unachapwa hata makofi kama marehemu Mwinyi kule Tnga .
Ndio maana unaambiwa ukienda nje ya uislamu basi sio muislamu , ukijihusisha na ugaidi ni kinyjme cha uislamu nchi zeny sheria za kiislamu adhabu yako ni kifo .

Wewe mwenyewe hushangai propaganda zote ila watu wanaslimu kila siku . je, wao hawaoni kama uislamu ni ugaidi 😀 😀 😀 ...

Uislamu uko perfect ila waislamu hawapo perfect , zile hukumu ulitaka ahukumiwe nan ?
 
Mmemshambulia Tundu lissu risasi so alikuwa gaidi ? ROgo ni ishu ya kisiasa na kuongea ukweli.
Cheki ulivyo mdwanzi.

"Rogo ni ishu ya kisiasa" uko sawa kweli? Nani asiyesikiliza mahubiri ya huyo Shehe marehem? Au mnadhani mawaidha yake mnasikiliza peke yenu?

Mwaka 2017 nipo nimepanga zangu nyumba Moja na jamaa mmoja muislamu sana (jamaa alikuwa serious na dini vibaya). Siku Moja katika Moja ya mawaidha yake akaweka mawaidha ya huyo Shehe Rogo.

Jamaa (mpangaji) alikuwa analifungulia Redio lake anataka Kila mtu asikie mahubiri ya kwenye Redio yake

So,hiyo siku akaweka mawaidha ya Rogo.

Shehe Rogo anakuambia "Ukimwona mkristo na kafiri yeyote anakaribia kukata roho kwa kiu,usimpe maji,mwache afe,Tena ikiwezekana mwaishe mapema kabisa usisubiri mpaka afe na kiu.

Kwa maelezo yake alikuwa anasema makafiri hawapaswi kuachwa wakaishi maana wameukataa uislamu. Na waumini wote kwenye msikiti walikuwa wanaitikia "Takbiiir" Kila anachosema.

Nimeongelea hiki kipande maana kilinifanya kuanzia siku ile nimchukie yule mpangaji kwa moyo wangu wote. Ubinadamu uko wapi sasa hadi umuue mtu asiye Imani yako?

Miaka 7 imepita,Leo wewe hapa jf unakuja kusema serikali iliingiza siasa ikamuua Rogo.

Bure kabisa wewe na wenzio msio na ubinadamu.
 
Cheki ulivyo mdwanzi.

"Rogo ni ishu ya kisasa" uko sawa kweli? Nani asiyesikiliza mahubiri ya huyo Shehe marehem? Au mnadhani mawaidha yake mnasikiliza peke yenu?

Mwaka 2017 nipo nimepanga zangu nyumba Moja na jamaa mmoja muislamu sana (jamaa alikuwa serious na dini vibaya). Siku Moja katika Moja ya mawaidha yake akaweka mawaidha ya huyo Shehe Rogo.

Jamaa alikuwa analifungulia Redio lake anataka Kila mtu asikie mahubiri ya kwenye Redio yake

So,siku Moja akaweka mawaidha ya Rogo.

Shehe Rogo anakuambia "Ulimwona mkristo na kafiri yeyote anakaribia kukata roho kwa kiu,usimpe maji,mwache afe,Tena ikiwezekana mwaishe mapema kabisa usisubiri afe na kiu.

Kwa maelezo yake alikuwa anasema makafiri hawapaswi kuachwa wakaishi maana wameukataa uislamu. Na waumini wote kwenye msikiti walikuwa wanaitikia "Takbiiir" Kila anachosema.

Nimeongelea hiki kipande maana kilinifanya kuanzia siku ile nimchukie yule mpangaji kwa moyo wangu wote. Ubinadamu uko wapi sasa hadi umuue mtu asiye Imani yako?

Miaka 7 imepita,Leo wewe hapa jf unakuja kusema serikali iliingiza siasa ikamuua Rogo.

Bure kabisa wewe na wenzio msio na ubinadamu.
Acha kuwa mpumbavu tangu lini serikali inashambulia watu ? serikali ilikuwa na uwezo wa kumfikisha mahakamai wakati Rogo kashambuliwa .


View: https://youtu.be/go3z4EPz_Bc?si=6ybIdWvlRRSZqaVT

Minyoo ya Nguruwe inakuharibu kichwani hata kufikiria hujui.

Bila ya mchongo wa vyeti fake hauna jipya , kumbe hata hujui unaongela , basi kashambuliwa kama Tundu Lissu .
 
Back
Top Bottom