KERO Njia ya Pugu Road (Vingunguti hadi Jet Corner) kuna harufu kali, sijui tatizo ni nini?

KERO Njia ya Pugu Road (Vingunguti hadi Jet Corner) kuna harufu kali, sijui tatizo ni nini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wale tunaoishi na kufanya shughuli zetu Pugu Road, kuanzia Vingunguti hadi Jet Corner kipindi cha nyuma eneo hilo lilikuwa na hali ya hewa nzuri, lakini siku hizi hali imebadilika, kumekuwa na harufu mbaya na nzito ambayo wakati mwingine inafanya iwe vigumu hata kufanya kazi na kuendelea na shughuli za kawaida.

Kinachonitatiza zaidi ni kwamba hatujui chanzo halisi cha harufu hiyo, tunajiuliza kama inatokana na viwanda vilivyopo maeneo hayo, uchafu unaozalishwa na shughuli mbalimbali, mifereji ya maji machafu au vyanzo vingine vya mazingira.

Sitaki kumtuhumu mtu au kiwanda bila ushahidi, lakini hali tunayokutana nayo ni ya kweli na inahitaji mamlaka husika ifanye uchunguzi na kutuambia chanzo chake.

Kwa hiyo, naomba mamlaka za mazingira, Halmashauri pamoja na NEMC zifanye uchunguzi wa eneo hili na kutupa majibu ya wazi kuhusu chanzo cha harufu hiyo na hatua zinazochukuliwa.
 
Back
Top Bottom