SoC01 Njia ya upatikanaji wa fedha kupitia mzunguko wa fedha nchini

SoC01 Njia ya upatikanaji wa fedha kupitia mzunguko wa fedha nchini

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 13, 2021
Posts
5
Reaction score
6
Mzunguko wa fedha ni kiwango cha fedha ambacho kipo katika jamii kupitia matumizi mbalimbali ya serikali. Mzunguko wa fedha hutokana na sera mbalimbali ambazo ni zimewekwa na Bank kuu katika kuruhusu kiwango cha mzunguko wa fedha

KWA NAMNA GANI MZUNGUKO WA FEDHA UNAWEZA KUWA MDOGO
Mzunguko wa fedha unaweza kuwa mdogo pale sera za fedha zinapokuwa na ongezeko la riba katika bank .mfano kama watu wanatozwa kodi kubwa katika mikopo hii itafanya wakopaji kuwa wadogo na kufanya wanaoweka fedha bank kuongezeka na kufanya fedha katika jamii kuwa ndogo. Fedha zilizopo bank zinapoazimwa (borrowing) kwa riba kubwa kupunguza waazimaji na kufanya mzunguko wa fedha kuwa mdogo

MBINU ZA KUONGEZA MZUNGUKO WA FEDHA KUPUNGUZA UGUMU WA UPATIKANAJI WA FEDHA
Serikali inaweza kuongeza mzunguko wa fedha nchini kupitia njia zifuatazo
1. kupunguza kiwango cha riba kwa wenye uhitaji wa mikopo katika mabank.
Upunguzaji wa riba katika bank ungesaidia watu kukopa bank na hivyo kuchochea kuanzishwa kwa biashara mbalimbali ambapo mzunguko wa fedha utaongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kuchochea kupunguza ugumu wa maisha miongoni mwa jamii

2. Kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma.
kama serikali itaongeza mishahara kwa watumishi wa umma itachochea ongezeko la mzunguko wa fedha kwa sababu hii itakuwa ni njia mojawapo ya kuruhusu fedha iloyopo serikalini kuingia katika mzunguko katika jamii kwa wingi na kufanya matumizi ya watu kuongezeka na kuchochea ongezeko la wajasiriamali. Fedha inapokuwa katika mzunguko mkubwa hupunguza ugumu wa maisha na hali duni katika jamii kutokana na urahisi wa upatikanaji wa fedha

3. Kuongeza kiwango cha Kuajiri kwa kiasi kikubwa
Ongezeko la ajira litachochea watu kupata fursa za kujiongezea kipato na hata kupunguza ugumu wa maisha na hivyo kuongeza mzunguko wa fedha ambao utasaidia maendeleo katika maisha ya mtu binafsi na katika jamii kwa ujumla. Lakini pia kufungua sekta ambazo zitachochea ongezeko la ajira na hata kuongeza pato la nchi.

4. Kupunguza kodi kwenye makampuni na biashara mbalimbali nchini
Kama serikali itapunguza kiwango cha kodi katika makampuni mbalimbali nchini itasaidia upatikanaji wa bidhaa kwa bei nafuu pamoja na urahisishwaji wa njia mbalimbali za huduma za kifedha ikiwemo bank kutoa mikopo kwa riba nafuu na vilevile makato ya miamala ya makampuni ya mawasiliano kuwa nafuu zaidi

FAIDA ZA ONGEZEKO LA MZUNGUKO WA FEDHA
Mzunguko wa fedha unapokuwa mkubwa huweza kuleta faida zifuatazo
1. Kuongezeka kwa uwekezaji nchini
Mzunguko mkubwa wa fedha huchochea uwekezeji kuongezeka na kuchochea kuongezeka kwa sekta mbalimbali ambazo zitaongeza ajira na kuongeza pato la nchi, watu wataweza kufungua biashara mbalimbali kutokana na riba nafuu na kusaidia ukuaji wa wajasiriamali nchini

2. Kupunguza hali duni ya maisha katika jamii
Mzunguko wa fedha unapokuwa mkubwa hurahisisha upatikanaji wa fedha na hivo basi kufanya maisha miongoni mwa jamii kuwa ya kawaida tofauti na mzunguko wa fedha unapokuwa mgumu huchangia ugumu wa maisha na kusababisha maisha duni katika jamii kwa wingi

HITIMISHO;
Mzunguko wa fedha unapokuwa mkubwa unafaida sana japo unaweza leta mfumuko wa bei, (inflation) serikali bado ipo katika mkakati wa kuongeza mzunguko kwa njia salama ambapo njia mojawapo ni ongezeko la matumizi katika serikali (Government expenditure) kupitia ongezeko la ujenzi wa miundo mbinu ambayo huchochea uwepo wa ajira na ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Ni vyema serikali yetu ya Tanzania iendelee na mikakati ikiwemo kuongeza nafasi za ajira na kupunguza riba katika mabank kuchochea ukuaji wa biashara na hali ya maisha katika jamii kwa ujumla
 
Upvote 4
Back
Top Bottom