permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
Kunywa pombe zilizopo mpaka ziishe, hii ndio dawa ya ukweliHabarini za wakati huu wote humu
Mimi kila mwaka najiwekea malengo za kufanya jambo/mambo flani au kuacha vitu/tabia ambazo zinanirudisha nyuma kimaendeleo.
Mwaka unaoisha nilipanga sichepuki na nikaweka mikakati namna ya kupambana na hilo. Nashukuru Mungu nimeweza hilo.
Mwaka huu nahitaji kuacha pombe, japo nimepunguza kwa kiwango kikubwa. Maana mwanzoni sikuweza kulala bila kunywa ila kwa sasa naweza bila tatizo japo kuna watu imebidi nikosane nao ili nifikie hatua hiyo.
Ishu inayonitatiza ni kuwa nahisi nisipokuwa makini ntarudi kulekule kwa sababu hamu ya kunywa haijaisha ila najikaza sana.
Nachowaomba ni kujua, je hakuna dawa ya kumfanya mtu aione kama uchafu flani hivi ili nisiwe naitamani? Nilishawahi kusikia watu wanaongea kuwa ipo lakini sina ushahidi kama kweli ipo. Msaada tafadhali
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app