Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Ufala #1 ni
Kunywa pombe halaf inakutesa mwenyewe, unawasumbua wengine au inakugeuza kua mtumwa

Ufala #2 ni
Hunywi pombe halaf huna unachokifanya

Ufala #3 ni
Kuchukia pombe na kupenda sigara

Ufala #4 ni
kuanza kupayuka au Kujisifia umelewa kwa pombe ya kununuliwa

Ufala #5 ni
Kua mlevi wa kupindukia wa pombe, zinaa na sigara kwa pamoja

Ufala #6 ni
Kuchukia pombe na kufurahia kudanga na kuish kwa ndugu

Ufala #7 ni
kufurahia pombe na kufurahia kudanga/mizinga na kuish kwa ndugu

Ufala #8 ni
kumchukia mlevi ikiwa hajabughudhi maisha yako wala ya mwingne

Ufala #9 ni
Kua mlevi badala ya mnywaji

Ufala #10 ni
kuona starehe yako ni bora kuliko ya mwenzako.

Ufala #11 ni
kuacha kunywa pombe halaf hakuna mabadiliko yoyote ya kiuchumi, ki fikra, ki maamuzi/vitendo n.k

Ufala #12 ni
kutokua na starehe ya kukupa furaha hata moja ila bd unapambana tu kutafta maisha.

Ufala #13 ni
Kumdharau/kumchukia mlevi ikiwa akili yako ukiwa mzima na ya kwake akiwa amelewa zinalingana au amekupita

Mwisho kbsa, kama katika utafutaji wako unawaza mafanikio tu na hujawah kupanga/waza kutafuta furaha na amani, Huo ni ufala na Nusu na wewe ni popona

Akili kumchwako, za kuambiwa changanya na zako.
 
Kuna mdau wangu ambaye ni ndugu wa karibu namtafutia dawa ya kuacha pombe, sisi familia tumeamua tuchukue maamuzi haya baada ya kuona anaharibikiwa,familia yake imesambaa ,ameuza kila kitu sababu ya pombe. Tafadhali mwenye dawa ya kuacha pombe asaidie
 
Tafta kuna nyuzi zimo humu zinaelezea vizuri swala hilo kiufasaha, ila ngoja nkuulize vizuri huyo ndugu yako anakunywa pombe tuu bila kuchanganya any drugs kama cocaine? Maana siamini kama kuna mnywaji pombe anaefikia hatua ya kuuza vijiko na sahani za nyumbani
 
Hakuna dawa, tangu utoto mshua alinizoesha pombe nilipofikia 20+ nilikuwa nakunywa hata bia 7 silewi maana pombe nilikuwa kama imenizoea but now nina miaka kumi hivi sijawahi kunywa niliamua tu mwenyewe kuacha, so naamini kuacha hakuhitaji dawa ni maamuzi tu
 
Pombe na umalaya ..ni RAFIKI WA UMASIKIN.


mkiambiwa mnaanza oohooooo Wee mshamba...mambo yako ivi mwanzo utaanza kwa bia tatu..siku utakua kwa stress unapiga 8-10.. Ndo mwanzo wakua chapombe.

Alafu kabla yakunywa, muwe mnaangalia historia za ukoo wenu kwanza kuhusiana na hasari za ulevi
 
Dawa ipo: Kuna samaki anaitwa ningu, chukua nyongo yake muaekee kwenye pombe, mhhh! atatapika sana na kuanzia siku hiyo atakuwa ameacha pombe mazima. Kwa dawa nyinginezo za kuacha pombe nitafute inbox.
 
Back
Top Bottom