Afadhali umeleta hii mada na mimi imenigusa.Mimi kuna wakati nakunywa bia nikichanganya na pombe kali naugua siku nne.
Ndugu yangu pombe inaua haraka na taratibu.Mfano ukinywa pombe kali mizinga minne tumboni hakuna kitu huamki.
Vishawishi vya pombe ni pesa na marafiki.Kuacha pombe ni rahisi mno kuliko sigara.Fanya hivii!!
1.Epuka kwenda kwenye maeneo ya pombe mfano bar
2.Kuacha marafiki ulikuwa unakunywa nao ni ngumu na sio vizuri maana wakati mwingine si ajabu huko kwenye pombe ndio ulipatia cheo kazini.Wewe ukiwa nao waambie uko kwenye dozi ya muda mrefu.Usitangaze umeacha pombe watatumia mbinu kukurudisha kundini.
3.Ukitoka nyumbani usitoke na hela nyingi.
4.Ukiona ngumu agiza bia mbili nywea nyumbani
5.Wakati mwingine wake zetu ni chanzo cha sisi kutoka kuna wake vimeo sana gubu haliishi.Muda ukiona hali hiyo nenda nyumba za ibada au fanya zoezi la kukutoa jasho au lima bustani au shamba.
6.Hamu ya pombe ikikushika chemsha maji lita 1.5 kunywa yakiwa vuguvugu utalala usingizi wa pono.Usidanganyike utakuwa unakunywa soda nyingi ukiacha pombe soda zina madhara kuliko pombe
ANGALIZO
Sio kila mnywa pombe hana maendeleo na sio kila asiyekunywa ana maendeleo.Kwa utafiti wangu wasiokunywa wengine ni wazinzi mno ana nyumba ndogo aheri anayekunywa
Mimi nimejaribu nimeweza mwaka umeisha sasa ila sijaacha ninasemaga nimepumzika