Mkuu
Huyo ndugu yako Kwanza mkikaa nae msiwe mnamsema na kumwambia pombe inamuharibia maisha ,inammalizia hela ,hafanyi kitu cha maana na maneno mengine ambayo yeye binafs ataona kama mnamsema vibaya hapo ndyo mtampagawisha zaid
Wakat mwingine huwezi jua Nini kinamfanya anakunywa kiasi hicho yaweza kuwa ipo sababu
Mlevi mzuri Ni yule ambaye hela anaacha nyumbani na anabeba kiasi tu kidogo kile alichokadiria kwamba nikipata chupa kadhaa ndio idadi yangu
Je unajua kwamba Kila mlevi anajua Ni chupa ngapi akifika ndio stimu znapanda na anaanza anahisi burudan?
Anzeni hapo Kwanza,utanipa feedback,usitake tu vuuuuuu! Aache pombe ningumu kama unga.
ataacha mwenyewe
Ila Kila siku mkimpigia kelele hizo kelele zenu zitafanya aongeze kreti nyingine maana ataona kama mnamsema vbaya na mnamuona hafai kwenu..
Mimi binafsi nilikuwa hivyo naweza nikaenda na 5laki nikarudi mweupee(bar Kuna ushawishi na marafk wa kujuana bar tu)
But ndugu walioamua wanikazie wakaanza kunisoma saa ngapi naenda bar(huwa Ni usiku nikitoka job) hata kama hanywi ataenda pamoja na wewe ukishalewa utaskia simu na vitu vyako nipe nikushikie umelewa sana,mdogomdogo mara kabla sijaenda anakupangia ratiba,unapinga mpaka unazoea
Hapa ninapoandika uzi huu nipo home mzinga umekufa zimebaki chupa 5 za bia ndio zinanisukumasukuma kumalizia usiku maana hata bar sitaman kukaa Tena Ni kuchukua na kutulia home na ndio najua kiasi gani nilipoteza huko nyuma(pesa zangu zinaniuma zileee)
Kumuachisha mtu pombe kibabe,maneno mabaya,kumsema ovyo Ni ngumu yatakiwa hata asipoacha apunguze na awe na ratiba maalum mwishoni mwenyewe ataona Nini afanye au vipi apange kuhusu pombe
Ni kama wewe mtu akuambie usitumie simu yako sababu inakumalizia sana bando na unakuwa busy sana kuchat utamuelewa wkt umeshazoea?
Mazoea mabaya
Nendeni nae taratibu,mwisho wale waliokuwa bar wanakula hela zake utawaskia ''siku izi huonekani bro unachukua na kusepa."
Lakini haya mawazo yangu tu!.
Sent using
Jamii Forums mobile app