Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

2021 wanachama wanazidi kupungua kwa kasi sana!!
Mmeona nini ambacho wengine atujakiona?
 
Tatizo lipo kwenye serengeti lite 8 hapo.
Tumia pombe KIDOGO kwa ajili ya tumbo lako, maisha bila pombe yafaa nini? mpe masikini pombe asahau shida zake, ila usisahau ole wake aamkaye asubuhi na mapema kwenda kufata mvinyo.
Kunywa pombe kidogo jioni baada ya kazi ila usiwe mlevi.
 
Kwa wewe mnywa Serengeti light ukiamua kuacha ni rahisi kuliko wale wagonga spirit.
 
Mi nafikiri ni maamuzi tu.
Mimi nilikuwa cha pombe haswa,lakini siku nilipoamua kuacha nilijisemea tu toka moyoni 'mimi pombe basi,imetosha'!.
Mwaka wa 3 huu sasa sijaigusa wala kufikiria kunywa.
Nina marafiki ambao ni wanywaji na mara nyingi tunakutana weekend sehemu za sterehe wao wanagonga vyombo,mimi nakula zangu nyama nashushia na maji mdogo mdogo.
Sikuwahi kujitenga na marafiki wanywaji na sehemu za vinywaji ndio nazopigia msosi nikiwa na mishe town.
 
Zoezi ambalo limewahi kufeli ni kujitenga na rafiki zako walevi. Siku mtakayokutana yani unakunywa za muda wote ambao ulijitenga nao.

Kama rafiki zako wote ni walevi usitafute marafiki wapya. Waambie rafiki zako lengo na nia yako ya kuacha pombe na waombe wakupe ushirikiano iwapo utakua unakutana nao ukiwa unakunywa maji wasiwe wanakulazimisha kupiga vyombo. Kama hawatakupa ushirikiano basi hamna budi kujitenga nao kwa muda na kutafuta vitu vingine vya kufanya mpaka pale utakapoweza kujicontrol kukaa nao bila kuagiza bia yani ukanywa maji au kinywaji kingine ambacho hakina kilevi bila kujisikia kutaka kunywa pombe.

Tengeneza detox water au Iced tea muda wote iwepo nyumbani kwako. Katika muda ambao unajisikia kama kunywa pombe unakunywa detox yako au Iced tea.

Kuna mtu kasema hapo kukaa na pombe ndani, kama kweli una dhamira ya dhati kaa na pombe yako pendwa ndani, jione kama utaeza kunywa au utaweza kuipotezea na kama utaweza kunywa je unaweza kunywa kwa kujizuia. Ukishaweza kuipotezea au kunywa kwa kujiuzia uko kwenye njia sahihi ya kufikia malengo ya kuacha pombe.
 
Kuacha pombe ni jambo gumu sana kama umeshafikka hatua ya umywaji wa kitabia, humwaji wa kitabia mi hatari sana kwani hupelekea kuharibu afya, kupoteza fedha nyingi, kuwa mgomvi, kufanya mambo ya hovyo na nk ukifikia hatua hii ni vema ukaanza kuchukuwa hatua.

Nenda pale Dodoma hospitali ya mirembe utapata tiba na hakika utaacha pombe, Tumepeleka ndugu zetu wawili pale mmoja ameacha kabisa pombe na mwingine amepunguza kwa zaidi ya asilia 70 afya yake imerudi na anatunza familia yake.

Ila kwa hili naona wewe si mnywaji sana sema kama umelitambua mapema ni jambo jema kwani ukiendelea zaidi hali itakuwa mbaya.

Ushauri wangu kwako jitahidi uwe unakunywa mara 2 angalau kwa wiki kwa kiasi cha fedha unachokimudu.

Jaribu kufanya mambo ya maana na kipato chako ili usiwe na hela inayokuwa float bakiza fedha itakayo kusaidia nauli na vitu vya msingi.
 
Sema toka nifanikiwe kuacha kuvuta bangi naamini hakuna kitu mtu anashindwa acha,,,ila Bia sikushauri uache
 
Tiba yako ndo yangu,ukisaidiwa hapa nami nitakuwa nimesaidika.ILA mimi toka tarehe 1/1/21 nimejiwekea mikakati ya kutokunywa kinywaji aina ya kinywaji iitwayo Konyagi na K vant kwani naona mwaka jana nilikuwa mtu wa kufa kwa kuzidisha na kuyanywa sana majitu hayo,nimeungua midomo,nahisi maini pia si salama.Namshukuru Mungu leo ni siku ya 11 bila kuonja hayo mavitu.

So nami natamani nikifanikiwa hili ndo nije hatua ya pili ya kuiacha beer.
NOTE:Hii sio kauli kwa ajili ya kujihami na karo za January bali inatoka moyoni,kwn nimeyagonga mno na kila mtu akiniona ananiambia ACHA spirits,hawa watu nawaona malaika natafakari sana juu yao kwangu,why me!!
Mi ntaachana na K Vant pale daktari bingwa atakaponihakikishia kuwa kama nikinywa leo basi kesho nitadedi...

Tena ntaupima ukweli wake kwa kunywa japo vi-tots viwili usiku ili nione nikiamka asubuhi kama ziraili atanibeep...
 
Anza kuwa unapiga value moja kwa siku alafu hii pia itakusaidia kuimarisha ndoa yako
 
Mi ntaachana na K Vant pale daktari bingwa atakaponihakikishia kuwa kama nikinywa leo basi kesho nitadedi...

Tena ntaupima ukweli wake kwa kunywa japo vi-tots viwili usiku ili nione nikiamka asubuhi kama ziraili atanibeep...
Hahhahaha wa chama mimi nimekwambia madhara machache yangu,ila hakika hii kitu nahisi naishindwa,sasa sijui na age inachangia?coz kwenye 40's kurudi nyuma nilikuwa nasema km wewe but now days nikiikunywa mambo yangu yanaenda hovyo

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Wakuu kwema?

Pombe pekee ninayokunywa huwa ni serengeti light,so imefikia point nataka niache kunywa kabisa kitu kinachoitwa pombe.kila nikijaribu kuacha nashindwa..mfano jana kizembezembe tu nimejikuta nimepiga chupa 8 za serengeti light.

Naomba mnipe mbinu za kuachana na unywaji wa pombe wakuu.
Ukishainunua na ikawa tayari imeshafunguliwa, unaacha kuibugia kwenda mdomoni, badala yake unaimwaga chini. Hapo ndiyo utakuwa umeweza kuacha kunywa bia
 
Wakuu kwema?

Pombe pekee ninayokunywa huwa ni Serengeti Lite, so imefikia point nataka niache kunywa kabisa kitu kinachoitwa pombe. Kila nikijaribu kuacha nashindwa. Mfano jana kizembezembe tu nimejikuta nimepiga chupa 8 za Serengeti Lite.

Naomba mnipe mbinu za kuachana na unywaji wa pombe wakuu.
Kwa nini unataka kuacha?
 
Back
Top Bottom