Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Tatizo la bia kila unapokunywa ndio inazidi kuwa tamu hivyo suala la kupunguza kwa kweli linakuwa gumu na ni ngumu sana kupata kupunguza kunywa bia,nimeoa nha shem wako anakunywa ila si sana tatu zinamtosha.

Nyalotsi hongera kwa kuweza kuacha na naomba ututupie faida za kuacha pombe nadhani itatusaidia sana sisi ambao bado tupo upande huu wa wanywaji wa vilevi.
 


Hahaha pole kwa kukujibu kwa ukali mdogo wangu MKATA KIU ila kumbuka pesa unayotumia kunywa hizo pombe inawezafika kipindi huipati tena kihivyo halafu hapo ndo majukumu yamekabaa - UTAJUTA!!
Pesa unayoinywa sasa unaweza kuifanyia mambo fulani (ukitaka ushauri zaidi ni-inbox) ambayo baadae utafurahia mwenyewe
SIO KILA SIKU JUMAPILI MDOGO WANGU
 
Ni PM nitakuelekeza mahari tulikochukua dawa ya kuacha pombe na bangi ya mdogo wetu maana yeye alikuwa amekubuhu na tulitumia kila aina ya dawa ilishindikana lakini kwa dawa ya huyo mzee hata umwekee bia namna gana hataki hata kusikia harufu yake

Ile dawa unamwekea mtu aliyekubuhu kama unavosema.
Ambaye anashindwa kabisa kuacha pombe.
Huyu mdau yeye hajgfika huko.
Huyu hajaamua tu kuacha mwenyewe.
Siku akiamua ATAACHA TU.
 
inakuwaje uache bia?unataka viwanda vifungwe watu wakose ajira?mimi nikiacha bia kwetu nitawekewa vikao ili nirudi kundini.
kunywa kuna siku utapewa tuzo ya mnywaji bora.
 
ukisikia hamu ya bia kunywa MALTA,at the end of the day utajikuta ni mnywaji mzuri wa MALTA instead of alcohol
 
Kuacha bia ngumu jamani.................ila wewe unakunywa nyumbani kipi kinakushinda kuacha.....................

Mie mdingi akinywa nyumbani hamalizi bia mbili lakini akiwa bar hata 10 zinafika...........................

Hujaamua tu kuacha wewe
 

Oyo. . .wa mzumbe. . .anza therapy ya chai, it helps a lot.. .mi mshua alipunguza bierre kwa therapy za chai daily, unanunua majani yako ya ukweli kama vile earl grey or vannila, thermos yako hakikisha ina maji moto daily. . .ukitoka kazini tu unapata vikombe vyako viwili, mwezi tu unasahau bia.
 
Pole MKATA KIU !!
Mi kwa ushauri wangu ujaribu kupunguza idadi ya hizo bia. Unajua kuna kunywa bia na kugida bia !!
Cha kufanya kuwa na msimamo kwamba kwa siku nakunywa kama ni tatu basi iwe ni tatu hiyo haiwezi kuathiri kipato chako,usije ukaacha bia ukahamia kwenye ngono manake wanywa sprite nao si haba.
Mwisho kabisa usijaribu kunywa mchana pombe inanywewa baada ya kazi yani jioni, pia ni mwiko kupunguza hang over kwa kuzimulia bia nyakati za asubuhi!!
Source" BABU YANGU !
 
Mkuu uza hiyo friji na usinunue tena pombe, ichukulie kama sumu kwa maendeleo yako
 
Ukiendelea kutumia ID hiyo sahau kuacha kunywa
 

Mimi niweza kuacha bia na nikawa nakunywa wine na spirits na hapo budget ili triple.

Halafu baadaye niliacha kunywa pombe kabisa, lakini ilikuwa kwa maombi ya bila kutegemea. This is what happened.
I was praying along with T.B Joshua thru Emmanuel TV (nilikuwa na kawaida ya kuangalia Emmanuel TV kila jioni huku nikisip my white wine), so that day nilizama kiibada baada ya kuweka glass yangu pembeni; nilitapika saana wakati ibada inaendelea.

Then next day, nimetoka kazini nimechoka; nikajimiminia wine yangu again huku napata neno, after one sip sikurudia tena (that crisp and sweet taste was gone) nikaimwaga kwenye sink. Sijagusa tena pombe aina yoyote, hamu haipo tena.

N.B
Wakati naomba, kuacha pombe haikuwa kwenye maombi yangu kabisaaaaaa wala hata kuifikiria. So kwa vile wewe una nia, nina imani utafaulu.
 


Suluhisho la ukweli na la kudumu ni kuokoka. Kumkaribisha YESU moyoni mwako, awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukiamini , yeye pekee ndiye mwenye mamlaka ya kukupa uwezo wa kushinda ushawaishi wa kufanya kile kisichompendeza Mungu. Mungu akusaidie unapochukua uamuzi wa busara. Mimi nilishachukua uamuzi huo na sasa nafurahia maisha mapya ndani ya Yesu.
 
Reactions: ram

Tumia gongo mkuu make ina bei nafuu na chenji unabakisha kwa ajili ya matumizi ya familia yako!

Nimekushauri hivi kwa sababu wewe unaomba msaada wa mawazo ili kuacha kunywa bia na SI KUACHA KUNYWA POMBE/VILEVI!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Yaaani nimeshindwa kumalizia kusoma.... nilipofika kwene Kesto mate yakaanza kunitoka, macho hayaoni na koo limekauka ghafla ebu ngoja kwanza nikapige mbili hapo chini fasta nikirudi ntamalizia...
 
Wewe kiboko, nilijua tu ndo utakuwa ushauri wako, sijui F80 na yeye yuko wapi

 
Ile dawa unamwekea mtu aliyekubuhu kama unavosema.
Ambaye anashindwa kabisa kuacha pombe.
Huyu mdau yeye hajgfika huko.
Huyu hajaamua tu kuacha mwenyewe.
Siku akiamua ATAACHA TU.

amesha kuambia kuwa anashindwa kuacha ndo maana anaomba msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…