husika na mada tajwa hapo juu
leo nimemshuhudia mtu kanywa vikonyogani vidogo vitatu ndogo yake ya yule jamaa anatunisha misuli kwenye chupa(wanaviita vischana sijui) ndo mara ya kwanza halafu kwa sababu katapeliwa
jamaaa ameteseka sanaa alikua analia tu na hakua amekula kitu tangu asubuhi anatia huruma sana kila mda anasema anakufa ila tumemsaidia yupo vizuri sasa hivi nlikua namuelewa sana tu anavyojiskia
huyu jamaa amenikumbusha na mm kwa mara ya kwanza nilivyokunywa pombe,ilikua wine kipindi nipo boarding school siwezi sahau niliona kama deka inapaa nilitapika sanaa chumba kizima kilikua kinanuka pombe kwa kweli nilijuta na nikajiapiza sitokunywa tena,hangover yake ilinikaa kama siku mbili hivi mdomo nlikua nahisi kama una nuka wine mda wote hata nipige mswaki vipi,nikawa najihisi nanuka pombe masaa 24 nlijiskia vibaya sana nikajiapiza sitokaa ninywe pombe tena..tangu siku hiyo nikisikia harufu ya wine natamani kutapika..sikukoma
mara ya pili nilikunywa kilimanjaro nikatapika sana,nikajua haya mambo sio yangu niaachana nayo mpaka leo sijui hata bei ya bia..nashukuru mungu mwili wangu una react vibaya kwa pombe
najua kuna watu wanataka watoke huko na wengine wanataka waende ..tuanze na hawa waliotoka,kisa gani mlikutana nacho mpaka mkaacha,njia gani mlitumia kuacha