Naomba msaada kwa anaefaham dawa ya kuacha pombe
kuna jamaa alinipa hiki kitabu nimuuzie. kinaweza kukusaidia.
Kuna dawa nyingi ambazo hutumika kusaidia watu kuacha pombe. baadhi ya dawa hizo ni kama disulfiram, fluoxetine ambayo kwa kawaida ni dawa ya sonona(depression). Dawa zingine ni pamoja na ondasentron, acamprosate, setraline na topiramate. Katika dawa zote disulfiram ndio imetokea kuwa maarufu sana na ndio tutakayo izungumzia sana katika kitabu hiki.
Disulfiram ni dawa ambayo mtu akiitumia halafu akatumia pombe hupata madhara ambayo yatamfanya asitumie/asitamani pombe. ni kama vile kula yamini. Mtu anayetumia dawa hii huelezwa kwa undani madhara yatakayo mpata akitumia pombe. kwa kuogopa madhara mtu huyu hawezi kutumia pombe. toka mtu atumie dawa hii hatakiwi kutumia pombe hata kidogo ndani ya siku kumi na nne (wiki mbili) vinginevyo atapata madhara.
Pombe hata inayopatikana kwenye vipodozi vya kupaka na mouth washes (dawa za maji za kusafisha kinywa) inaweza kusababisha madhara makubwa. Uzuri ni kwamba madhara haya hayaui na huisha yenyewe japokuwa mtu anaweza hitaji uangalizi wa mtaalamu wa afya kumpunguzia madhara ayapatayo.
41
Madhara yanayoweza mpata mtu akitumia pombe na disulfiram ni kama yafuatayo. Kuvimba uso, maumivu makali ya kichwa, kupata tabu kupumua, kichefuchefu, kutapika sana, kutoka jasho kwa wingi, kiu kali, maumivu ya kifua, moyo kwenda mbio, kushindwa kuona vizuri na kuchanganyikiwa. Watu wenye magonjwa ya moyo na magonjwa ya akili hawapaswi kutumia disulfiram kwa sababu ina