Asante mkuu
Allency ila ingekua vizuri ungenambia ww ulifanyeke Ku recover
Binafsi nilikua adicted,kiasi kwamba nikishika kikombe cha maji mikono inatetemeka,nilikua nikiishiwa pesa nauza vitu vyangu vizur,nilikua sikai na cm,uaminifu kwenye familia ulipotea kwangu,watu walikua hata kunituma kitu nikanunue waliogppa,kifupi hadi familia ilinichukia sababu ya pombe,na nimekunywa pombe zote unazozijua wewe za kizungu na kienyeji,hadi shule nilikataa wakati huo.hapo ni kifupi tu nikikusimulia fully story unaweza andika kitabu,hii ni hadithi ya miaka 6 iliyopita nimeacha pombe 2010 december
Sasa hivi ukiniona maisha yangu huwez amin,na baadhi ya watu mtaani hawaamini,Sababu ndani ya miaka hii 6,nikaweza soma kozi fupifupi za taaluma nimeajiriwa,nimejenga nyumba kubwa ya vyumba7 nimepangisha5 na 2 nakaa mwenywe,nina kigar changu cha kunipeleka job nimenunua shamba kama heka40 moro.Umri wangu ni miaka 32 tu.
Mabadiliko haya yote ni baada ya kuacha pombe na vijana wengi mtaan wanabadilika kupitia mm Sababu nilikua naitwa chapombe wakati huo.
Kiukweli huwa natamani nialikwe kwenye makongamano ya vijana niwape mfano hai kupitia mimi.
Lakini katika haya yote kwangu kuna Baraka za Mungu zilipita kwangu maana kwa akili zangu haikuwa kaz rahis.
Tokea kipindi hicho ckuwah itamani pombe wala kugusa kinywa changu.
Nikutie nguvu endelea kuamini unacho amin,mwanzon watakukatisha tamaa lakini simama