Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Sina hata hisa moja kumbuka ule ni mfano tu
 
Asante mkuu Allency ila ingekua vizuri ungenambia ww ulifanyeke Ku recover
Binafsi nilikua adicted,kiasi kwamba nikishika kikombe cha maji mikono inatetemeka,nilikua nikiishiwa pesa nauza vitu vyangu vizur,nilikua sikai na cm,uaminifu kwenye familia ulipotea kwangu,watu walikua hata kunituma kitu nikanunue waliogppa,kifupi hadi familia ilinichukia sababu ya pombe,na nimekunywa pombe zote unazozijua wewe za kizungu na kienyeji,hadi shule nilikataa wakati huo.hapo ni kifupi tu nikikusimulia fully story unaweza andika kitabu,hii ni hadithi ya miaka 6 iliyopita nimeacha pombe 2010 december
Sasa hivi ukiniona maisha yangu huwez amin,na baadhi ya watu mtaani hawaamini,Sababu ndani ya miaka hii 6,nikaweza soma kozi fupifupi za taaluma nimeajiriwa,nimejenga nyumba kubwa ya vyumba7 nimepangisha5 na 2 nakaa mwenywe,nina kigar changu cha kunipeleka job nimenunua shamba kama heka40 moro.Umri wangu ni miaka 32 tu.
Mabadiliko haya yote ni baada ya kuacha pombe na vijana wengi mtaan wanabadilika kupitia mm Sababu nilikua naitwa chapombe wakati huo.
Kiukweli huwa natamani nialikwe kwenye makongamano ya vijana niwape mfano hai kupitia mimi.
Lakini katika haya yote kwangu kuna Baraka za Mungu zilipita kwangu maana kwa akili zangu haikuwa kaz rahis.
Tokea kipindi hicho ckuwah itamani pombe wala kugusa kinywa changu.
Nikutie nguvu endelea kuamini unacho amin,mwanzon watakukatisha tamaa lakini simama
 
Habari wakuu..
nimefanikiwa kuacha pombe hapa karibuni lakini nimekua na tatizo la kutopata usingizi toka nilipoacha naombeni msaada nifanye nini kuondokana na hali hii
Mimi imekuwa tofauti. Nilivyokuwa nakunywa nilikuwa sipati usingizi hata mida ya wanga, sasa nimeacha nalala vizuri sana tena mapema.

Jitahidi kufanya mazoezi uchoke, utalala tu.
 
Kuacha pombe si jambo rahisi kama mtu anavyoweza kufikiria, wakati mwingine kama si wote unahitaji msaada wa Mungu katika kumkabili ibirisi huyo pamoja na jitihada binafsi.
Cha msingi fanya sana mazoezi + badili mfumo wa maisha yako na marafiki ili usije rudi tena huko. Mwisho tafuta kitu kingine cha faraja kama kusoma magazeti, movies, kishiriki seminar mbalimbali na kujitolea kwa jamii kama kutoa elimu ya mazingira na vitu kama hivyo. Hii itakufanya kuwa busy na kutopata mda wa kuwaza gambe
 
Hujaacha pombe ila sema umepumzsha mwili...kuacha pombe ni mpak ufikishe miez. 6 bila kuonja kabsa,nje ya apo umepumzka kwa mda..beer zina kiu yake mkuu ambayo kuiacha mkuu ufanye kazi,mi sikushaur uache 7bu utaingia kweny vi2 vya kijinga saan ila jitahid saan uicontrol tu
 
tunaenda bar kujiburudisha baada ya shughul za mchana.
kazi na dawa.unatafuta hela ili utumie.

Nakubaliana na wewe kabisa Jombaa, Tatizo linakuja pale burudani inapopitiliza. Naingelea alcoholisim, Wengi wetu ni alcoholics lakini hatujijui, Ukiona unashindwa kulala bila kustua moja jua tayari kuna Tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…