Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Kila siku nilikuwa nakunywa bia sita na zaidi IPA Dogfish 90 (9% Alcohol) mpaka nikaanza kupata issues ndogo ndogo za kiafya. April mwaka huu rafiki yangu mmoja akanikokota kwenda kwenye retreat ya kilokole porini kwa siku tatu. Usiku ule wa kwanza tu mhubiri anasimama nikasikia "Wengine hapa ni walevi. Kwa jina la Yesu nakuhakikishia ukiondoka hapa hutakunywa pombe tena". Something clicked inside and I was touched. Nililia sana usiku ule in front of about 200 men. Basi nilizingirwa nikawekewa mikono nikaombewa mpaka nikawa hoi. Nilirudi home na kutupa bia zote zilizokuwa kwenye cooler. Halafu rafiki yangu mmoja akaniambia kuwa nikipata hamu ya pombe basi nile tikiti maji la baridi. Nilifanya hivyo na baada ya wiki mbili hamu yote ya pombe ikaisha na tangu mwezi wa nne 2015 sijaonja pombe tena. Gym, mboga mboga na matunda aisee nimerudi kwenye fomu balaa mpaka watu hawaamini. Huu ndo ushuhuda wangu wa kweli kuhusu kuacha pombe na sijui kama utakusaidia. Usikate tamaa na kama una nia ya kweli ya kuacha inawezekana hata kama ikibidi ni kupitia maombi na higher power. Good luck!