....... nianze kunywa bia na siku kama sina hela nakunywa makonyagi na nikiianza tu kunywa basi tarudi home saa sita na nikiwahi sana basi ni saa nne,yani kwa siku nakunywa bia zaidi ya 13 na sigara 40
Naombeni kama kuna mtu anajuwa dawa yoyote ila aniambie Tashukuru sana endapo tapata tiba
Ninakunywa ila nimepunguza sana na ninaelekea kuacha kama wewe unavyodhamiria. Cha msingi ni wewe mwenyewe kuendelea na dhamira yako na kama umeoa mke wako ni muhimu sana kwani ana nafasi ya kukusaidia. Mimi nilikuwa nakunywa kuanzia asubuhi, na wakati mwingine nilikuwa naenda kazini nishapiga Bavaria 8.6 kama tatu hivi, na jioni usiseme....akina Black label na wenzake chupa ilikuwa inaisha...ila baada ya kuamua kutaka kuacha nilipewa technique na wataalam ambazo nyingine naona wadau wameshazisema. Naomba nikupe experience yangu!
1. Acha kabisa kunywa Whysky na Konyagi...endelea na bia tu
2. Anza kupunguza idadi ya bia unazokunywa kwa siku...
3. Anza kuruka siku moja moja bila kunywa bia, siku ambazo hunywi kunywa maji mengi sana....endelea hivyo mpaka ifike mara moja kwa wiki n.k
4.Ukishindwa na hata ukujikuta umeanza huo mpango halafu hapo katikati ukauvuriga kwa kutwanga creti nzima uzife moyo, uanze tena huo mpango, Usiondoke kweye DHAMIRA YAKO YA KUACH...
5. Niliamua kumpa mke wangu ashie pesa zangu ili kufanikisha hayo, na kwa kweli mke wangu alinisaidia kwani mshahara ukiingia au nikipata posho yoyote ya safari ndio shida ilikuwepo hapo, niliamua kuwa mkweli na kubaki na pesa za mambo ya kawaida tu na zikiisha basi, mambo yote ya pesa ni mke wangu tu alikuwa anayafanya na kunijulisha...hili niliamua mwenyewe baada ya kuona nimekuwa mlevi wa kupindukia.....
6. Nilmuomba sana Mungu anisaidie kuniondolea ile hamu ya pombe, kweli huwa siendi sana kanisani ila ninasali mwenyewe hasa usiku, imenisaidia sana na kunijenga...
7. Sasa ni kama mwaka umepita baada ya kuanza mpango huo wa hiyari na kwa kweli nimepunguza sana na kwa mwezi ninaweza kunywa bia si zaidi ya sita tu, na nikizikosa hainisumbui kabisa.....na sasa naweza kuwa na pesa na wala nisinunue bia kabisa....Namshukuru Mungu sana na mke wangu.