Yoshua Bin Sira: 31:25-31, 40:2025) Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa kileo (pombe), yaani mvinyo,Imewaangamiza wengi.26) Tanuru hujaribu kazi ya mhunzi, na mvinyo mioyo ya watu, katika ugomvi wa wenye kiburi.27) Kwa wanadamu mvinyo ni kama maji ya uzima, ukinywa kwa kiasi. Je, anao uzima gani mtu asiye na mvinyo? Nayo imeumbwa ili kuwafurahisha wanadamu.28) Mvinyo ni furaha ya moyo na changamko ya roho, ikinywewa kwa wakati wake na ya kutosha.29) Lakini kunywa mno ni uchungu wa roho, na fedheha, na ugomvi.30) Kileo humzidishia mpumbavu mitego ya kumletea hasara; hupunguza nguvu, na zaidi huleta jeraha.31) Usimkaripie jirani yako kwenye karamu ya mvinyo, wala usimdhihaki anapocheka, wala usimwambie neno la shutumu, wala usimnyenye kwa kutaka alipe deni.40:20 - Kunywa mvinyo na kuimba kunachangamsha moyo, na upendano wa rafiki hupita yote.Zaburi 104:15Na divai imfurahishe mtu moyo wake; aungaze uso wake kwa mafuta, na mkate umburudishe mtu roho yake.Mhuburi 10:19Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, na divai huyafurahisha maisha, na fedha huleta jawabu la mambo yote.1timotheo 5:23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.