Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Kunywa pombe usiambiwe na mtu acha pombe ukaacha, bado utarudia, kunywa hadi we mwenyewe uache.

Sent using Jamii Forums mobile app
Njia nyingine ya kuacha ni kuwa na patner mke/mme ambaye hatumii kabisa. Mimi huwa natumia ila wife hatumii,na hatuishi pamoja kutokana na kazi,sasa nimegundua nikiwa peke yangu nakunywa muda mwingi. Wife hapendi harufu kabisa sasa nakuwaga najicontrol sana tukiwa wote,mpaka kuna wakati nakuwa kama nimeacha ila nikirudi kazini naanza tena
 
[QUOTE="Makanyagio,
Weka wazi mkuu, pombe inaporudisha maendeleo yake nyuma we inakuathiri vipi? je ni mtu unaemtegemea kimaisha? Kama hapana mi najua Pombe ni starehe na mara nyingi mtu anatakiwa anywe pesa ya ziada. Anyway, niliwahi sikia huko kanda ya ziwa wana dawa flani huwekwa katika pombe mtu akinywa hiyo pombe basi atachukia pombe maisha yake yote yaliyobaki.

Kingine ni mtu mwenyewe tu, huenda kuna mambo yanamsibu jaribu kwanza kuchunguza kama yapo uanze kutatua hayo, watu wengine ni wasiri sana anapokuwa na matatizo hasemi wala hatafuti ushauri, hii hupelekea kufanya mambo ambayo hugeuka ulaibu. Binafsi niliwahi pitia hali ya ulevi chanzo kilikuwa broken heart( i met my first love at 26 years), niliamini she is the only one but nikaja realize alikuwa mchumba wa mtu na alikuwa anajitahidi sana kunificha.

Nilipoamua kuachana nae sikupenda lakini ilikuwa ni bora kuliko kushare, imagine unajua anatoka na mtu mwingine halafu mda unapokuwa nae anakwambia anaweka simu silent and then next time unampigia unakuta hapokei badae anakwambia simu niliweka silent, she is telling you alikuwa anasokotwa, ha ha haaa.


Niliona aibu kuwaambia washkaji kwa hofu watanicheka na kila mawazo yalipozidi nikaishia kuwa mlevi, jamaa mmoja akakutana na yule dada ndo kumuita shemeji bidada akaeleza mkasa mzima, jamaa waliniweka kikao wakanishauri and believe me tangu siku hiyo niliacha ulevi. Now i drink occasionally na huwa sinywi zaidi ya bia 2. I only go out 2 weekends in a month, the rest i dedicate to work and that really has changed my llife. YOUR WOMAN AND ONE TRUE LOVER IS ONLY YOUR MAMA.
 
Kisayansi pombe iko kwenye kundi moja na madawa ya kulevya. Ukishazoea kunywa pombe kupita kiasi unakuwa na addiction ya pombe. Ukiacha kunywa pombe utajisikia kama mgonjwa na unakuwa huwezi kula vizuri na kulala usingizi.
Hali hii imewafanya walevi kuona kama wamefungwa na kwa hiyo akinywa pombe anakuwa amefunguliwa.

Wao wanasema "kutoa Lock"

Njia za kufuata kuacha ulevi ni zile zile zinazofuatwa na mla unga. Lakini mtu anaweza kuacha pombe kwa kumfanya awe busy muda mwingi na kumchosha kimwili (physically) na kiakili(mentally). Mtu aliyechoka mara nyingi anakuwa na usingizi mwingi kitu ambacho mlevi anakikosa asipokunywa.

Wanafalsafa husema " Idle labor is the factory of devil). Kwa watu wengi wasio na shughuli nyingi za kufanya kwa muda mrefu huishia kufanya mambo ya starehe kama kunywa pombe, kutumia madawa ya kulevya, kufanya umalaya, kubuni mbinu za kuiba n.k.

Vitu kama Kusali mara kwa mara pia humwezesha mtu kujiepusha na pombe kwa sababu nyumba za ibada hawaruhusiwi watu waliolewa kuingia ndani.
 
Njia moja ya kuwezesha kujikwamua kwenye ulevi, ni kuacha kunywa pombe. Who knew? Yaani ile chupa ya kwanza tu asinywe kinywaji kilichomo. Utaona mara moja anaacha kuwa mlevi.
 
Niko napambana kuacha siku ya 51 Leo naona kama kuna mafanikio. mimi niliamua tu kuichukia Pombe. imenipotezea mengi mno kama sio pombe hata leo singekua nina type hapa
 
Kwa mfano "Pombe,sigara na Soda ni mojawapo ya vitu vinavyolitafuna Taifa pole pole,ingawa wengi wetu tutumiapo tunadhani ni sehemu ya maisha,ufahari na mazoea"
Tunywe maziwa,tufanye mazoezi na kupumzisha miili yetu.
EMT,
 
Back
Top Bottom