Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Wakuu!

Naomba mnisaidie jinsi ya kuacha kunywa pombe, yani nakunywa sana bia.. Nataka kuacha ila nashindwa.

Cha ajabu nikinywa bia, huwa nasikia sana raha, kama nilikuwa na stress zinapotea [emoji16]

Msaada wenu, naomba.
Bora wewe ,Mimi nagonga Sana K vant na konyagi
 
Wakuu!

Naomba mnisaidie jinsi ya kuacha kunywa pombe, yani nakunywa sana bia.. Nataka kuacha ila nashindwa.

Cha ajabu nikinywa bia, huwa nasikia sana raha, kama nilikuwa na stress zinapotea [emoji16]

Msaada wenu, naomba.
Kuacha pombe kunafanana sana na kumuacha 'couple' ama mpenzi wako huku ukingali unampenda, hakuna mchezo hapo huwa mpaka uilazimishe dhamira ndiyo ushinde, vinginevyo utashitukia 'unarudiana'!

Jambo hilo unapotaka kulifanya lazima uandae mazingira ya utekelezaji wa dhamira yako hiyo.

Usishawishiwe na mtu, dhamira hiyo iwe ni thabiti, itoke katikati ya moyo wako hapo utaweza na utashinda.

Nimesema uandae mazingira maana yake ule muda huru uliokuwa unautumia kwenda kwenye ma bar uutafutie kazi zenye tija za kufanya, ili muda huo uwe ndani ya ratiba ya kazi hizo, pia piga vita vikao na marafiki zako wanywaji ama kujipitisha maeneo shawishi.

Kule kusema unapokunywa unajisikia raha sana ndiyo 'uteja' wenyewe huo na ndiyo kiini cha mjadala huu.

Na raha hizo ni illusions tu za ubongo ambazo unatakiwa kuzipiga vita ili uzoee kuishi bila hiyo 'raha' ya bandia.

Kisha usijidanganye kubadili aina ya pombe, kwa mfano, uache bia uhamie kwenye wine ama mbege, hapo utakuwa unaruka mkojo unakanyaga desh desh!

Pia usijifariji kwa 'kuacha kidogo kidogo'!

Kuacha kidogo kidogo maana yake haujadhamiria kuacha bali umepunguza tu.

Na utakapoanza 'program' ya kuacha, usije thubutu kuonja pombe nyingine yoyote ile kwa kisingizio chochote ili kuulinda muda uliotumia kuacha, vinginevyo utakuwa unacheza mchezo wa merry go round wa kuzunguka na kurudi pale pa mwanzo kuanza upya!

Sasa utakuwa unaacha na kuanza upya hadi lini?

Nimekupa mbinu niliyoitumia mimi kuacha kabisa kutumia pombe (niliitwa mlevi) miaka 30 iliyopita sasa na nishazoea na kusahau.

Zile ndoto za kuota ninakunywa ama nimelewa ziliisha niisha kichwani na sifikirii kutia pombe kinywani mwangu tena maisha.
 
Ila chupa!!!kuna hii Kilimanjaro kirikuu sijui wameiwekea sukari ya wapi?Tamu hiyoooo!
 
Angalia ni muda gani unakunywa bia
Tafuta shuguri itakayokukeep busy
Anza kupunguza kiwango cha kunywa kama ulikuwa unakunywa kumi na tano nenda na 12 ukipunguza taratibu
 
Wakuu!

Naomba mnisaidie jinsi ya kuacha kunywa pombe, yani nakunywa sana bia.. Nataka kuacha ila nashindwa.

Cha ajabu nikinywa bia, huwa nasikia sana raha, kama nilikuwa na stress zinapotea [emoji16]

Msaada wenu, naomba.
Kama uko Mwanza Jiji, ebu tukutane Villa pale Kirumba mida ya jioni tushauriane.
 
255653429097_status_0f792709959645ff98577c2494a0c40c.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda wa kunywa utumie kwa kuchukuwa mazoezi ya kukimbia anza kwa kukimbia 3km kesho 5km kesho kutwa yake 7km adi ufike 30km
 
Wakuu!

Naomba mnisaidie jinsi ya kuacha kunywa pombe, yani nakunywa sana bia.. Nataka kuacha ila nashindwa.

Cha ajabu nikinywa bia, huwa nasikia sana raha, kama nilikuwa na stress zinapotea [emoji16]

Msaada wenu, naomba.
Dondoka mfrejini mitaa ya wajuba.
 
Wakuu!

Naomba mnisaidie jinsi ya kuacha kunywa pombe, yani nakunywa sana bia.. Nataka kuacha ila nashindwa.

Cha ajabu nikinywa bia, huwa nasikia sana raha, kama nilikuwa na stress zinapotea [emoji16]

Msaada wenu, naomba.
Ipo dawa kama una nia ya dhati nione nikupe namba za wanaouza mi metumia saivi taha nikae bar sigusi
 
Habari zenu wadau

Jamani nipeni mbinu za kuweza kuepuka na kujitoa kwenye hiki kifungo cha ulevi maana inanipa hasara pamoja na kudhalilika mno mbele ya jamii ikiwa bado nikijana mdogo na mwenye nguvu

Nipeni msaada wa mbinu za KUACHA kwa mliofanikiwa kuacha kabisa, Ahsante
 
Back
Top Bottom