Wakuu!
Naomba mnisaidie jinsi ya kuacha kunywa pombe, yani nakunywa sana bia.. Nataka kuacha ila nashindwa.
Cha ajabu nikinywa bia, huwa nasikia sana raha, kama nilikuwa na stress zinapotea [emoji16]
Msaada wenu, naomba.
Kuacha pombe kunafanana sana na kumuacha 'couple' ama mpenzi wako huku ukingali unampenda, hakuna mchezo hapo huwa mpaka uilazimishe dhamira ndiyo ushinde, vinginevyo utashitukia 'unarudiana'!
Jambo hilo unapotaka kulifanya lazima uandae mazingira ya utekelezaji wa dhamira yako hiyo.
Usishawishiwe na mtu, dhamira hiyo iwe ni thabiti, itoke katikati ya moyo wako hapo utaweza na utashinda.
Nimesema uandae mazingira maana yake ule muda huru uliokuwa unautumia kwenda kwenye ma bar uutafutie kazi zenye tija za kufanya, ili muda huo uwe ndani ya ratiba ya kazi hizo, pia piga vita vikao na marafiki zako wanywaji ama kujipitisha maeneo shawishi.
Kule kusema unapokunywa unajisikia raha sana ndiyo 'uteja' wenyewe huo na ndiyo kiini cha mjadala huu.
Na raha hizo ni illusions tu za ubongo ambazo unatakiwa kuzipiga vita ili uzoee kuishi bila hiyo 'raha' ya bandia.
Kisha usijidanganye kubadili aina ya pombe, kwa mfano, uache bia uhamie kwenye wine ama mbege, hapo utakuwa unaruka mkojo unakanyaga desh desh!
Pia usijifariji kwa 'kuacha kidogo kidogo'!
Kuacha kidogo kidogo maana yake haujadhamiria kuacha bali umepunguza tu.
Na utakapoanza 'program' ya kuacha, usije thubutu kuonja pombe nyingine yoyote ile kwa kisingizio chochote ili kuulinda muda uliotumia kuacha, vinginevyo utakuwa unacheza mchezo wa merry go round wa kuzunguka na kurudi pale pa mwanzo kuanza upya!
Sasa utakuwa unaacha na kuanza upya hadi lini?
Nimekupa mbinu niliyoitumia mimi kuacha kabisa kutumia pombe (niliitwa mlevi) miaka 30 iliyopita sasa na nishazoea na kusahau.
Zile ndoto za kuota ninakunywa ama nimelewa ziliisha niisha kichwani na sifikirii kutia pombe kinywani mwangu tena maisha.