Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Ukiipata hiyo dawa niambie na mimi pa kuipata maana, maana ulevi wangu umekuwa kero kwa jamii nzima na aibu kwangu.
Nikilewa mtaa mzima hawalali, natukana, napiga kelele, mlingoti nausimaisha kisha natembea uchi mchana kweupeeeee
 
Njia rahisi ya kuacha pombe ni kujitenga na marafiki walevi pili kama una familia jiweke karibu nayo kuliko mwanzoni mweleze mkeo nataka kuacha pombe atakupa ushirikiano wa kutosha kwani huwa wanakereka sana tunavyorudi usiku wa manane.Ila kubali kukashfiwa na marafiki kuwa mke kakutawala utakapojitenga nao(kama upo pembezoni ya mji anzisha ufugaji hata wa kuku mifugo itakuweka busy mda wa jioni na hutapata mda wa kupanda kwenye stuli ndefu.

Mi nalanduka peke yangu wala sihitaji ushawishi wa washkaji.
Tangu jana niko hapa Kona Baa Shekilango road, nimelewa hadi sasa pombe zinajiondoa zenyewe kichwani
 
wana jf mnisaidie kwa hili kwa anayefahamu dawa ya kuacha kunywa pombe aina yoyote,nimeanza kunywa pombe tangu nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi mwaka 1996 mpaka sasa,nimejaribu sana kuacha lakini imeshindikana,je kuna dawa maalumu?
ukifika baa usininunue, hiyo ndiyo dawa pekee.
 
Ukiipata hiyo dawa niambie na mimi pa kuipata maana, maana ulevi wangu umekuwa kero kwa jamii nzima na aibu kwangu.
Nikilewa mtaa mzima hawalali, natukana, napiga kelele, mlingoti nausimaisha kisha natembea uchi mchana kweupeeeee
hamia mtaani ninaoishi mimi uone kama hatutalala kwa sababu ya mapombe yako!
 
dawa ya UKWELI ya kuacha kunywa pombe ni kuacha kunywa pombe. Dawa hii inafanya kazi INSTANTLY na haina side effects.
Maana yake ni kwamba inabidi uamue toka ndani ya ubongo wako.
 
kwawewe inaonekana kifo ndo kinaweza kukutenganisha na unywaji wako...silivyo uahamie IRAN
 
Mbona simpo jamani!

Tafuteni fedha ya kutosha kiasi mnywe mpaka muwe chakali hamjitambui. Mtapoamka mkakuta mmevunjiwa yai uani, wallah nawaambia hamtakunywa pombe tena maishani mwenu
 
Dah! Pagumu hapo ila the only thing that can work ni self determination, that's all.
 
Daah,sasa bia zimepanda bei watu mnaamua kuacha pombe!ongeza bidii kipato kiongezeke jombaaa.Ukiacha pombe ni hasara kwa taifa na hatutoruhusu hili,kama vipi njoo hapa double view hotel tuliongelee swala lako la kuacha pombe huku tukilamba za mwisho mwisho!
 
mzazi wangu alikua mlevi hadi basi (Aibu) lakini kaacha . wanadamu wanafiki wakaanza kumpa ofa lakini aliacha kabisa akafikia kiwango cha kusikia harufu tu ni kutapika ndo wakaamini. jitoe muhanga. pia kuwa karibu na mtu wa kukumonitor
 
mwendee Yesu maana yeye anasema njoni k wangu nyote mlio lemewa na mi zigo nami ntawapumzisha
 
Hapo patata mkuu,Jiulize kwanza kwa nn unataka kuacha?Kipato or Inakuendesha?Uki incontrol pombe utajiona umeacha.Bt kama ni kipato bado hata ukiwa na mia mbili utataka unywe ka konyag.Cha msing amua kwa nn unataka uache?
 
Kuacha pombe hakuna dawa bali uimara wa nafsi yako. Hakuna awezaye kukusaidi kuacha kunywa pombe isipokuwa wewe mwenyewe.
 
Kuacha ni wewe kuamua,mi ramadhani yote huwa sigusi na inawezekana so ukiamua utaweza.
 
wana jf mnisaidie kwa hili kwa anayefahamu dawa ya kuacha kunywa pombe aina yoyote,nimeanza kunywa pombe tangu nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi mwaka 1996 mpaka sasa,nimejaribu sana kuacha lakini imeshindikana,je kuna dawa maalumu?
joel amani Dawa yaKucha kunywa Pombe siku ukiwa umelewa kama yupo Mama yoyote yule anaye nyonyesha mwambie akutilie Maziwa yake kidogo kwenye Pombe yako ukinywa ntu ndio itakuwa wewe ni mwanzo na mwisho wa kunywa hiyo Pombe.

Ukiipata hiyo dawa niambie na mimi pa kuipata maana, maana ulevi wangu umekuwa kero kwa jamii nzima na aibu kwangu.
Nikilewa mtaa mzima hawalali, natukana, napiga kelele, mlingoti nausimaisha kisha natembea uchi mchana kweupeeeee
Bujibuji Dawa ingine ya kuacha kunywa Pombe mtafute Muislam yoyote yule aliyekwenda Maka kuhiji anayo maji ya Zamzam ayasomee dua kisha akupe unywe hutakunywa tena wewe hiyo pombe.
 
Last edited by a moderator:
No cheap medicine, it is just your utmost will to stop!
 
Ukiipata hiyo dawa niambie na mimi pa kuipata maana, maana ulevi wangu umekuwa kero kwa jamii nzima na aibu kwangu.
Nikilewa mtaa mzima hawalali, natukana, napiga kelele, mlingoti nausimaisha kisha natembea uchi mchana kweupeeeee

Daah! watu wengine kweli mnazifaidi pombe,yaani ukinywa unakuwa FILII namna hiyo,mi mwenzenu ,sijui nina tatizo gani!? hata ninywe vp nabaki na akili zangu,sijawahi hata kutukana kwa kipindi chote takribani miaka 16 ,sasa
 
Back
Top Bottom