Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Wadau/wakuu wa jamvi nisaidien katika hili nataman sana kuacha pombe lakini nashindwa nifanyaje? Na je kuna dawa maalum ya kutumia ambayo inaweza nsaidia?(mi ni nywaj wa kama bia 7 na kuendelea kwa siku wakat mwingine had nazima kabisa)

Nakupongeza kwa uamuzi wako uliouchukua wa kuomba ushauri wa kutaka kuacha kunywa POMBE! Ni watu wachache sana wanaweza kufanya kama wewe! Kwa kupitia JF unaweza ukapata members wazuri na wabaya watakaokupa ushauri wa kila aina.

Mimi binafsi nilikuwa mlevi wa kupindukia! Kila nikijaribu kuacha kunywa nilikuwa nashindwa kutokana na ushawishi wa rafiki zangu! Siku moja nikiwa naendesha gari huku nikiwa nimelewa nilipata ajari mbaya sana. Namshukuru Mungu sikufa wala kiungo cha mwili wangu kukatika. Lakini nina makovu mwilini kama kumbukumbu!

Msukumo unaoupata moyoni mwako kuwa uache pombe, hata mimi nilikuwa naupata na kupuuzia! Hebu fikiria ni pesa ngapi umepoteza kwa kunywa pombe? Ni faida gani umeipata kwa kunywa pombe? Amua mwenyewe sasa toka moyoni kuwa pombe sikutaki tena pamoja na wafuasi wako na Mungu atakusaidia. Usisubiri yakupate yaliyonipata mimi na walevi wengine.
 
kaka pambana kama nami ninavyopambana,mi pia niko mapambanoni wiki ya pili hii sijaonja hii ni mara baada ya my wife wangu kuniambia nichague mke au pombe! manaake mi huwaga nazioga sio kunywa coz nikiingia bar hazipungui bia 10 nakuendelea!
 
Wadau/wakuu wa jamvi nisaidien katika hili nataman sana kuacha pombe lakini nashindwa nifanyaje? Na je kuna dawa maalum ya kutumia ambayo inaweza nsaidia?(mi ni nywaj wa kama bia 7 na kuendelea kwa siku wakat mwingine had nazima kabisa)
Jambo la kwanza ni kuacha kunywa pombe jaribu kuchunguza chanzo kilichokufanya uanze kunywa pombe?Tafuta suluhisho kama kuna sababu zilosababisha uwe mlevi.
Dawa zipo mojawapo ni NALTREXON au ACAMPROSATE hizi dawa zinakupunguzia hitaji na abstinence symptoms za alcohol.
DISULFIRAM ni chaguo jingine.
 
Wadau/wakuu wa jamvi nisaidien katika hili nataman sana kuacha pombe lakini nashindwa nifanyaje? Na je kuna dawa maalum ya kutumia ambayo inaweza nsaidia?(mi ni nywaj wa kama bia 7 na kuendelea kwa siku wakat mwingine had nazima kabisa)
wanasema ukiamka mkojo wa kwanza ukiamka asubuhi ndio dawa hasa wa wamama wajawazito....
 
nasikia kinyesi cha mtoto mchanga ni dawa,ulambe na chengine upake kidogo kwnye paji la uso kwa muda wa wiki moja,unaacha kabisa
 
Uache pombe ili iweje? Au unataka serikali ikose mapato yatokanayo na biere zako za kila siku? Ujue kuacha kwako kuta waathiri watanzania wengi sana we endelea tu mpwa na ukishindwa kabisa mtafute aliyekufundisha kunywa kisha akuelekeze namna ya kuacha
 
really?
 
Acha ushamba mkiri na kumkubali yesu kuwa bwana na mwokozi wako, yeye atatenda!
 
Tatizo walevi wakiambiwa kwenda kwa wataalamu wa akili wanaona wanadhalilishwa.

Lakini ukweli upo hapo, nenda kwa wataalam wa ushauri wa kuancha pombe.
Hata kama ukipewa dawa ya kuacha leo, bila kufuata ushauri waweza pata repalse baadae.

Unajishushia heshima yako kwa kutoa ushauri laini namna hii.

Siu akivunjiwa yai uwani mbona hatahitaji msaada wa mawazo wala dawa.
 
Sina ushauri rasmi nnaoweza kukupa ila nna uhakika kitendo cha kutambua kua unatakiwa kuacha ni hatua moja itakayokufikisha kuacha kabisa. Walevi wengi hawawezi kuacha pombe simply bcoz hawataki kukubali kama ulevi ni tatizo.
 
kaka pambana kama nami
ninavyopambana,mi pia niko mapambanoni wiki ya pili hii sijaonja hii ni
mara baada ya my wife wangu kuniambia nichague mke au pombe! manaake mi
huwaga nazioga sio kunywa coz nikiingia bar hazipungui bia 10
nakuendelea!

ha ha ha haaa,sana tu mkuu,mi mwenyewe nipo kwenye mapambano makali ya kuacha viserengeti vyangu,ila kagemu ni kagumuu,hapa 2pu nishamoka 2 na nimepata free serengeti 1,kuna kuacha hapo kaka,tatizo hii kampuni wana kagemu kao kananipatiaga elf 10,40 za bila kutegemea,ila hiki kigemu kikifinito,naacha pombe,nani kamwaga pombe yangu,nauliza,ngwea anajibu,siyo mimi,marehemu bwanaa
 
Mtukane bosi wako akikutimua kazi utakosa mshahara na ukikosa mshahara utakosa hela ya kununua pombe na itapelekea moja kwa moja wewe kuacha pombe
 
Nakupongeza kwa uamuzi wako uliouchukua wa kuomba ushauri wa kutaka kuacha kunywa POMBE! Ni watu wachache sana wanaweza kufanya kama wewe! Kwa kupitia JF unaweza ukapata members wazuri na wabaya watakaokupa ushauri wa kila aina.

Mimi binafsi nilikuwa mlevi wa kupindukia! Kila nikijaribu kuacha kunywa nilikuwa nashindwa kutokana na ushawishi wa rafiki zangu! Siku moja nikiwa naendesha gari huku nikiwa nimelewa nilipata ajari mbaya sana. Namshukuru Mungu sikufa wala kiungo cha mwili wangu kukatika. Lakini nina makovu mwilini kama kumbukumbu!

Msukumo unaoupata moyoni mwako kuwa uache pombe, hata mimi nilikuwa naupata na kupuuzia! Hebu fikiria ni pesa ngapi umepoteza kwa kunywa pombe? Ni faida gani umeipata kwa kunywa pombe? Amua mwenyewe sasa toka moyoni kuwa pombe sikutaki tena pamoja na wafuasi wako na Mungu atakusaidia. Usisubiri yakupate yaliyonipata mimi na walevi wengine.

kaka very simple"! just weka nia mungu atakuongoza na epuka makundi ya vishawishi vya pombe
 
Mtukane bosi wako akikutimua kazi utakosa mshahara na ukikosa mshahara utakosa hela ya kununua pombe na itapelekea moja kwa moja wewe kuacha pombe

kila siku namlaumu sana Mrema kwa kuharamisha bange.
 
Back
Top Bottom