kisugujira
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 774
- 200
Wadau/wakuu wa jamvi nisaidien katika hili nataman sana kuacha pombe lakini nashindwa nifanyaje? Na je kuna dawa maalum ya kutumia ambayo inaweza nsaidia?(mi ni nywaj wa kama bia 7 na kuendelea kwa siku wakat mwingine had nazima kabisa)
Nakupongeza kwa uamuzi wako uliouchukua wa kuomba ushauri wa kutaka kuacha kunywa POMBE! Ni watu wachache sana wanaweza kufanya kama wewe! Kwa kupitia JF unaweza ukapata members wazuri na wabaya watakaokupa ushauri wa kila aina.
Mimi binafsi nilikuwa mlevi wa kupindukia! Kila nikijaribu kuacha kunywa nilikuwa nashindwa kutokana na ushawishi wa rafiki zangu! Siku moja nikiwa naendesha gari huku nikiwa nimelewa nilipata ajari mbaya sana. Namshukuru Mungu sikufa wala kiungo cha mwili wangu kukatika. Lakini nina makovu mwilini kama kumbukumbu!
Msukumo unaoupata moyoni mwako kuwa uache pombe, hata mimi nilikuwa naupata na kupuuzia! Hebu fikiria ni pesa ngapi umepoteza kwa kunywa pombe? Ni faida gani umeipata kwa kunywa pombe? Amua mwenyewe sasa toka moyoni kuwa pombe sikutaki tena pamoja na wafuasi wako na Mungu atakusaidia. Usisubiri yakupate yaliyonipata mimi na walevi wengine.