Njia za kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba

Njia za kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba

akohi

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Posts
787
Reaction score
526
Kwanza kabisa anza na kuchimba na kujengea mashimo ya choo. Hii itasaidia ule udongo au mawe uyajaze ndani ya msingi wa nyumba na kama ni sehemu ya mchanga basi utatumia ule mchanga kufyatulia tofari.

Huna haja ya kununua mbao ambazo ni treated maana siku hizi zinachakachuliwa na zaidi zinapakwa rangi tu wala hawazitreat unless uagize toka kiwandani direct, cha kufanya nunua mbao za kawaida then nunua mafuta ya diesel na weka vijana wape na brush wazipake mafuta, i guarantee hakuna mdudu atasogea.

Pia wakati wa kununua mbao usikubali wakupimie kwa futi zao maana nyingi zimekatwa urefu na kuungwa mf futi inaurefu wa mita ishirini basi wanakata katikati lets say toka mita nne mpaka kumi so wewe utaona mita ishirini kumbe umeuziwa mita kumi na tu. So kubali kuingia gharama ya kununua futi.

Pia sio lazima kila ujenzi uchimbe msingi mrefu la hasha maana kama eneo lako ni mawe au miamba sasa unachimba nini? Ila kama eneo lako ni tifutifu au mfinyanzi au kichanga basi shart wachimbe msingi mrefu.

Hakikisha unapoanza ujenzi uwe na mtu wako au mke au mme au ndg yako atakaye simamia other wise utalaumiana na wajenzi tu hasa kwenye materials.

Zaidi jenga mazingira ya wewe mwenyewe kwenda kununua au kulipia materials usimpe fundi hela, japo baadhi ni waaminifu.

Kubaliana na fundi kazi yote lakin mlipe kwa piece work na usikubari wewe ndo umdai...atakimbia tu.

Na mwisho tujifunze kuto copy na kupaste ramani za nyumba. Mf nyumba nyingi zina milango miwili. Why? Kwanini nikitaka kwenda nyuma nipite jikon? Kwanin kila mgen afikie sebureni moja kwa moja?

Na huwa sielewi most of houses zina ka balcon pale mbele yaana over 90% za nyumba na unakuta sitting room pia hapo hapo mbaya zaidi piga ua utakuta nyumba ina vyumba vitatu lakin viwili tu ndo vinamadirisha mawili kingine dirisha moja tu...why? Inamaana uwezo wetu wa kufikiria ndo umeishia hapo...laa hasha tatizo tulilonalo na ku copy na ku paste.

Maana utakuta nyumba nyingi hazitumii mlango wa mbele sababu ya poor deaigning na pia wakati wa jua kali wala sebureni hapatamaniki kukaa.

Pandeni miti ya kutosha majumbani kwenu.

alfred.kohi@kcd.co.tz

Wengine ongezeeni....
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Patamu hapo Makame hebu rudia tena maana ni patamu sana hapo
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Usiuite ki-local, ndio ujenzi wa most of Tanzanians. We usifikirie kila mtanzania anaishi Dar tena City Center, Mbezi, n.k. Au wanaishi Arusha, Mwanza n.k. Watanzania wengi ujenzi wao ndo huo aliochambua jamaa. Kama wewe unatumia ma-engineer basi weka uchambuzi wako watu wachangie!
Hongera mtoa post japo bado hujaitendea haki sana heading!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Tunashukuru kwa kupeana mbinu za hapa na pale ikiwemo kuokoa gharama za ziada
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Kweli kuelewa kazi. Hivi huoni kama mleta mada anaongelea gharama nafuu? Sasa gharama nafuu na kumkabidhi engineer wapi na wapi? Kwa maisha ya mtanzania wa kawaida hivi katika nyumba 10 ukizichagua bila bias ni ngapi utaona zilisimamiwa na mkandarasi? Hapa kinachoongelewa ni nyumba za kawaida.
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Hujui unachokiongea maana huu uzi umelenga kwa wenye kipato cha kawaida sio nyinyi wenyw uwezo wa Turn Key Project.
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Sio kweli bana,nyumba za kuishi hapa Africa mzima ni za kawaida ambazo unaweza jenga kwa kusimamia wewe mwenyewe au nduguyo au mkeo,swala la kuweka injinia wa ujenzi wa nyumba ya kuishi ni la watu wachache sana wenye uwezo kifedha,watu wengi town na nje ya town tunawaona pindi wanapojenga na uwezo wao,ataanzia wapi kumlipa injinia wakati malipo yake tu ni boma limenyanyuka,by the way unajua vyema japo unajaribu kujikweza
 
Hata yeye unaweza kuta hana hata mti wa mpera mjini,ni mbwembwe tu za wabongo

Sema lini unataka kuja kwangu kigamboni ili ujifunze na uone ninachokiongea
 
Back
Top Bottom