Njia za kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba

Njia za kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba

Ni sawa kabisa Kyenju ila hapa nilimaanisha wale watu ambao wana a, b, c za ujenzi ila hawana muda wa kusimamia na ndo maana nikashauri uweke mtu wa karibu ili akae pale toka asubuhi then wewe muhusika unaenda jion kureview mf mimi ilitokea unarudi jion unakuta kuta au beam imepinda na ililazim baadhi ya kuta kuzivunja na tukaanza upya. Au unakuta kona haina square ila kwa ambae hana muda kabisa basi ni vizuri aweke na apate msimamizi mwenye uelewa.
Kimsing hapa changamoto ni mbili.

Kuibiwa vifaa na ubora wa ujenzi

Tuko pamoja mkuu, ule uzi wa solar siku hizi sioni update.
 
Kweli kuelewa kazi. Hivi huoni kama mleta mada anaongelea gharama nafuu? Sasa gharama nafuu na kumkabidhi engineer wapi na wapi? Kwa maisha ya mtanzania wa kawaida hivi katika nyumba 10 ukizichagua bila bias ni ngapi utaona zilisimamiwa na mkandarasi? Hapa kinachoongelewa ni nyumba za kawaida.

Naomba ufanunuzi kuhusu hizo unazoita nyumba za kawaida.
Zinajengwaje kwa makaratasi au?
 
Naomba ufanunuzi kuhusu hizo unazoita nyumba za kawaida.
Zinajengwaje kwa makaratasi au?

Nyumba za kawaida ni zile,
1.pesa ya ujenzi umekopa milion 7 taasisi za fedha unajenga nyumba inaisha unahamia na chenji ya kununulia bodaboda inabakia.
2.ujenzi hauangalii quality muhimu fundi kanjanja aifikishe nyumba palipokusudiwa maana mkopo ukiisha hakuna ujenzi tena.
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Si lazina awe engineer anaweza kuwa architect or Quantity Surveyor pia tena engineer awe structural engineer mana ma engineer wapo wengi hata IT na electrical wote engineer but hawana sifa za kusimamia
 
Si lazina awe engineer anaweza kuwa architect or Quantity Surveyor pia tena engineer awe structural engineer mana ma engineer wapo wengi hata IT na electrical wote engineer but hawana sifa za kusimamia

Ndo umeandika nini? Sisi tunazungumzia mimba wewe unatuletea vitambi.
 
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.

Hata kama unaye injinia kwa uzoefu wangu inabidi na wewe mwenyewe uwe makini. Nimeshajenga sana na nimeliwa pesa sana mpaka nilipoamua kuwa na ufuatiliaji wa karibu sana nikagundua mchezo mchafu unaofanywa na injinia na fundi. Fundi na injinia wanakupa bei ya cement, nondo, mbao, kokoto, mchanga n.k, ukizunguka mwenyewe unagundua ya kuwa kila mahali kuna 10%. Mwezi uliopita tu nilipewa mahesabu ya kokoto na fundi kwa kushirikiana na injinia, nikawaambia nitakuwepo mwenyewe kokoto ziitakaposhushwa. Nikagundua ya kuwa kokoto nilizolipia hazikuwa zilizoletwa, na pili nilipewa hesabu ya lori moja zaidi... Uzuri nilikuwa sijawapa pesa yao, na nikasimamia kuletewa kokoto sahihi na nikahesabu malori yaliyoshushwa. Sina haja ya kuwaeleza ukweli ulioniuma sana na niliokoa pesa sana. Nchi yetu ya 10% imani imekwisha!
 
Hapo ndo tunapokosea watanzania,
Kwako wewe nyumba ya kawaida ni ipi?
Unapompeleka site mke wako asie na ujuzi wa chochote kuhusu ujenzi ina maana gani?
Huyo haendi kusimamia ujenzi bali anaenda kumlinda fundi asiibe matirial yako ya kubangaiza.

----- mboyoyo
 
This is not not for everyone!
 
Umejieleza vizuri Na mi nakuongezea sample hizi ili uwe fundi ujenzi mwenye vielelezo Vya nyumba ulizotaja
 

Attachments

  • 1410756741017.jpg
    1410756741017.jpg
    110.5 KB · Views: 467
Hongera sana Akohi kwa kutupa tips za kupunguza gharama za ujenzi...
 
Safi sana Nyamgluu hii ndo maana na lengo la kuanzisha huu uzi ili tupeane ideas,
Nakubariana na swala la corridor na paa ila sujaelewa hapo kwenye madirisha kuwa kati, pls fafanua.

Mimi jikon kwangu hakutunzwi chochote mf masufuria, chumvi, etc kila kitu kinakaa stoo ambayo iko jiran na jiko na jikon panabaki majiko tu. So vitu vinatolewa stoo wakat vinahitajika na kurudishwa stoo vinapokuwa havitumiki, that means jiko muda wote halina chombo na ni safi

Pia nimeweka balcon mbele ya nyumba ambayo inatosha ku accomodate sub sitting na sub dinning ndogo maana sitaki kila mgeni aingie main sebure au dining kuu. So pale mbele pana set za viti na meza kama ilivyo sutting na dining. Kwa hiyo kuna sitting rooms mbili na dinning rooms mbili.

Pia nikaweka milango ya kutoka njee iko minne.
1.Mmoja uko jikon
2.Mwingine unakutoa nje upande wa kushoto
3.Watatu unakutoa nje upande wa nyuma mkabara na main door
4.Plus main door

Halafu sikuweka mbwembe lakin almost zaidi ya nusu ya ukuta wa dinning ni grili tu ili kupata mwanga na hewa, kesho ntaweka picha.

Pia sitaki kwangu itumike extensions za umeme, so nimeweka sockets za kutosha kwa maana kwamba kila kitu kichomekwe ukutani na zaidi nimeweka system mbili tofaut za umeme kwa kila kitu...taa na sockets yaan zipo zenye umeme wa solar na zipo za tanesco

Mwe! we si mtanzania wa kawaida niliyefikiri mnamuongelea hapa. Milango minne ya kwendea tu nje? hata mi napenda nyumba nzuri na unique lakini uwezo duni. Milango minne ni kati ya 1,600,000 - 2,000,000 kwa mbao nzuri standard hapa dar. Kwa hiyo nikiweka milango miwili nasevu nusu ya hiyo hela nafanyia kitu kingine. Kuwa na stoo jikoni pia kunamaanisha eneo kubwa zaidi na mlango tena na kadirisha. Mi sina hela na kiwanja changu kidogo. Hizo sockets nyingi tena nyingine za solar zingine za taanesko nazo hata mie ningependa sana kuwa nazo lakini hela sasa! Au nyie mnapata wapi hela? Mie mwalimu chaki haziuziki, natamani nifuge kuku lakini mwenye nyumba kakataa......basi nadunduliza na kukopa sakos. Hii nyumba itaisha leo kweli?
 
Back
Top Bottom