Nakubaliana na mleta mada kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa maeneo mengine makubaliana na
Makamee pamoja na King Kong. Suala la fundi pamoja na msimamizi ni la kuzingatiwa sana, inatakiwa wawe ni watu wenye uelewa mpana katika hii fani ya ujenzi, hasa msimamizi. Binafsi nimekwisha kumbana na mafundi wengi tena kwa kuelekezwa na mtu kwamba anaye fundi mzuri kumbe hamna kitu, ni fundi wa kupanga tofali na kupiga plaster. Mafundi wengi hawajui masuala ya "ratio" wengi hawajui vipimo vya zege, fundi anakwambia ununue nondo za 12mm kwa ajili ya kusuka colum au beam, na anatumia nondo 3 bila kuweka rings za kushikilia hizo nondo. Ushauri wangu, kama hauna uelewa na mambo ya ujenzi mtafute mtaalamu wa ujenzi akupe ushauri, siyo lazima asimamie unaweza kumtumi kukupa ushauri tu. Kumbuka unaweza kukwepa gharama lakini baada ya muda mfupi ukaingia gharama kubwa kuliko za mwanzo, kv msingi na kuta kupata nyufa au rangi ukutani kupata fangasi.