Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.
Namsema huyo jamaa anaetaka injinia unaweza kuta hana hata kiwanja wala mti wa mpera town
Namsema huyo jamaa anaetaka injinia unaweza kuta hana hata kiwanja wala mti wa mpera town
Ooh sawa kabisa na gari anapark ccm, au ndo wale watoto wamama maana mtu mzima tena muhangaikaji hawezi kukejeri namna yoyote ile ya kupunguza au ku save matumizi hasa ktk ujenzi
Sema lini unataka kuja kwangu kigamboni ili ujifunze na uone ninachokiongea
Sio kweli bana,nyumba za kuishi hapa Africa mzima ni za kawaida ambazo unaweza jenga kwa kusimamia wewe mwenyewe au nduguyo au mkeo,swala la kuweka injinia wa ujenzi wa nyumba ya kuishi ni la watu wachache sana wenye uwezo kifedha,watu wengi town na nje ya town tunawaona pindi wanapojenga na uwezo wao,ataanzia wapi kumlipa injinia wakati malipo yake tu ni boma limenyanyuka,by the way unajua vyema japo unajaribu kujikweza
Hapo ndo tunapokosea watanzania,
Kwako wewe nyumba ya kawaida ni ipi?
Unapompeleka site mke wako asie na ujuzi wa chochote kuhusu ujenzi ina maana gani?
Huyo haendi kusimamia ujenzi bali anaenda kumlinda fundi asiibe matirial yako ya kubangaiza.
Hata unapoishi unaweza kua umepanga wewe na nyumba imejengwa kwa kumtegemea fundi akisimamiwa na mwenye nyumba mwenyewe,msijifanye hamuijui Tanzania na Africa nzima juu ya hilo,kujikweza kwa nn?!
Ndo maana kuna vyuo vya kufundisha mainjinia kwa akili yako wale wakafanye kazi wapi? Wewe unasimamia fundi wakati hujui ufundi ina maana gani?
Hata huyo mleta mada unaemsapoti anasema chimba shimo upate mchanga wa kujengea,hivi kweli hapo kuna ujenzi wa nyumba kweli? Ktk ujenzi kila kitu lazima kiende na vipimo
1.aina ya udongo ktk site
2.msingi ueje kulingana na aina ya udongo
3.mchana uwe namba ngapi
4.kokoto ziwe namba ngapi
5.maji yawe na madini gani
6.n.k nakadhalika
Sio kweli bana,nyumba za kuishi hapa Africa mzima ni za kawaida ambazo unaweza jenga kwa kusimamia wewe mwenyewe au nduguyo au mkeo,swala la kuweka injinia wa ujenzi wa nyumba ya kuishi ni la watu wachache sana wenye uwezo kifedha,watu wengi town na nje ya town tunawaona pindi wanapojenga na uwezo wao,ataanzia wapi kumlipa injinia wakati malipo yake tu ni boma limenyanyuka,by the way unajua vyema japo unajaribu kujikweza
Sema lini unataka kuja kwangu kigamboni ili ujifunze na uone ninachokiongea
Mimi nina ugomvi na corridor! sipendi corridor kabisa!! Unajengeje nyumba ya kukaa wewe unaweka corridor kama gesti? Nina nyumba 2 zote hakuna corridor.
Ila kuna design moja nataka nijenge nikiwa na pesa itakua nzuri maana sijui kwanini nyumba ziwa na madirisha kati, paa la triangle na kadhalika. Nataka kama yai hivi linalokua linatoka kwa kuku! Anyways wengi hawataelewa.
Hela zangu, kiwanja changu, bado nimuige mwingine?
Niliipenda sana heading lakini kumbe iko tofauti na inavosomeka, nilitegemea nitapata mbinu mbadala za kukwepa gharama za ujenzi, kumbe ni maelekezo jinsi ya kujenga!
Hiyo ndo idea ya huu uzi,
mimi nimeweka zangu kulingana na uzoefu na nyie muongeze zenu namna ya kusave cost.
hili la namna ya kudesign limeingia by the way tu