Kwa wale wenye ardhi ya kichanga basi mchanga utakao tolewa shimoni ndo utaanza nao kwenye ujenzi na wengine unakuta anapata bahati ya maji pia so unauwa ndege wawili kwa jiwe moja
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.
Musidharau udongo au mawe au mchanga unaotoka kwenye mashimo ya choo maana wengi wetu tunakosea sana hapo.
Utakuta mtu kesha maliza ujenzi wa jengo ndo anachimba kisima sasa inamlazim atafute lory kusomba kifusi wakati kama angeanza na shimo basi kile kifusi kingetumika kujaza ndani ya msingi. Mf mimi toka nianze ujenzi sikuwahi kusomba kifusi maana shimo la choo lenye upana 12m na urefu wa 15m liliweza kujaza msingi na uzuri ardhi ya hapa kwangu ni mawe tupu so sikupata taabu kununua mawe wala kifusi.
shimo la 12m x 15m? kwa wengine hiki kiwanja cha kutosha ujenzi wa bungalow
Safi sana Nyamgluu hii ndo maana na lengo la kuanzisha huu uzi ili tupeane ideas,
Nakubariana na swala la corridor na paa ila sujaelewa hapo kwenye madirisha kuwa kati, pls fafanua.
Mimi jikon kwangu hakutunzwi chochote mf masufuria, chumvi, etc kila kitu kinakaa stoo ambayo iko jiran na jiko na jikon panabaki majiko tu. So vitu vinatolewa stoo wakat vinahitajika na kurudishwa stoo vinapokuwa havitumiki, that means jiko muda wote halina chombo na ni safi
Pia nimeweka balcon mbele ya nyumba ambayo inatosha ku accomodate sub sitting na sub dinning ndogo maana sitaki kila mgeni aingie main sebure au dining kuu. So pale mbele pana set za viti na meza kama ilivyo sutting na dining. Kwa hiyo kuna sitting rooms mbili na dinning rooms mbili.
Pia nikaweka milango ya kutoka njee iko minne.
1.Mmoja uko jikon
2.Mwingine unakutoa nje upande wa kushoto
3.Watatu unakutoa nje upande wa nyuma mkabara na main door
4.Plus main door
Halafu sikuweka mbwembe lakin almost zaidi ya nusu ya ukuta wa dinning ni grili tu ili kupata mwanga na hewa, kesho ntaweka picha.
Pia sitaki kwangu itumike extensions za umeme, so nimeweka sockets za kutosha kwa maana kwamba kila kitu kichomekwe ukutani na zaidi nimeweka system mbili tofaut za umeme kwa kila kitu...taa na sockets yaan zipo zenye umeme wa solar na zipo za tanesco
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.
Ndo maana kuna vyuo vya kufundisha mainjinia kwa akili yako wale wakafanye kazi wapi? Wewe unasimamia fundi wakati hujui ufundi ina maana gani?
Hata huyo mleta mada unaemsapoti anasema chimba shimo upate mchanga wa kujengea,hivi kweli hapo kuna ujenzi wa nyumba kweli? Ktk ujenzi kila kitu lazima kiende na vipimo
1.aina ya udongo ktk site
2.msingi ueje kulingana na aina ya udongo
3.mchana uwe namba ngapi
4.kokoto ziwe namba ngapi
5.maji yawe na madini gani
6.n.k nakadhalika
Huyo anataka nyumba ya gharama kubwa, eti engr ???
Usisahau kuvuta maji kwanza usinunue maji ni gharama ya ziada!!!
Moja, hivi wood flooring na tiles za mchina ni ipi bora na rahisi? pili, kuna umuhimu/faida gani ya kutumia gypsum plaster badala ya ile plaster ya chokaa na cement?
Hizi zote ni nadharia tu......uhalisia unabaki palepale kuwa nyumba nyingi watu wanazoishi wamejenga bila usimamizi wa injinia na nyumba ni bora nyingine zimeshakaa 40 years bila hata crack!Ndo maana kuna vyuo vya kufundisha mainjinia kwa akili yako wale wakafanye kazi wapi? Wewe unasimamia fundi wakati hujui ufundi ina maana gani?
Hata huyo mleta mada unaemsapoti anasema chimba shimo upate mchanga wa kujengea,hivi kweli hapo kuna ujenzi wa nyumba kweli? Ktk ujenzi kila kitu lazima kiende na vipimo
1.aina ya udongo ktk site
2.msingi ueje kulingana na aina ya udongo
3.mchana uwe namba ngapi
4.kokoto ziwe namba ngapi
5.maji yawe na madini gani
6.n.k nakadhalika
Itakua ni shimo la swimming pool,kama ni choo basi ni choo cha kata.
Naunga hoja mkono nimejifunza mawili matatu. Hasa pale unaposema uanze na mashimo ya choo. Ni kweli shimo udogo kwa maeneo ambayo maji mi tatizo unaweza pia ikatumika kuhifadhia maji kwa ajili ya ujenzi.