Naunga hoja mkono nimejifunza mawili matatu. Hasa pale unaposema uanze na mashimo ya choo. Ni kweli shimo udogo kwa maeneo ambayo maji mi tatizo unaweza pia ikatumika kuhifadhia maji kwa ajili ya ujenzi.
Makamee i guess some thing is not right to you upstairs.
Kama hujui sio lazima uchangie.
We ndo wale umerithi kila kitu hata bei ya kiwanja, tofari, cement hujui, na huna kitu tangible cha kujivunia kama mpambananaji.
Niliamua kuchimba shimo la choo kubwa ili kwanza niachane na karaha ya kila mwezi au miwili unaleta gari la kufyonza uchafu maana shimo limejaa, pili ili nipate mawe na kifusi cha kutosha.
Na kulijenga hilo shimo ililazim tuweke concrete beam toka chini then juu tuka suka beam zungine mbili kwa umbo la alama ya kujumilisha, mwisho ndo tukamwaga zege la kufunika eneo lote.
Unqposema choo cha kata ndo umedhirisha kwa 100% ya ku copy na ku paste vitu, mpaka leo huwa sielewi kwanini watu tuna standise ukubwa wa mashimo ya vyoo? Why? Na ndo maana kila kukicha vinajaa na inakuwa kero.
Mimi kwa ujenzi wangu mambi mengi niliamua kurekebisha makosa ya wengi.
Kwa wale wenye ardhi ya kichanga basi mchanga utakao tolewa shimoni ndo utaanza nao kwenye ujenzi na wengine unakuta anapata bahati ya maji pia so unauwa ndege wawili kwa jiwe moja
Vipimo ni futi sio mita, nimerekebisha
Kwa akili mlazo kama zako unajua jiografia ya maeneo yote unaweza kuchimba na kupata matirial ya kujengea,
Kama hujui maeneo kama Arusha udongo wake haufai kwa chochote hata uchimbe mita 200 kwenda chini,na baadhi ya maeneo inakulazimu uhamishe udongo na ulete udongo mpya ili uweze kujenga.
Makame jifunze kuwa positive na ku appreciate, unapoona mtu kakosea ni vizuri kukosoa ili mambo yaende lakin sio kejeri ambazo hazina tija
Hata kukalili ni sehemu ya kujifunza unless hutambui maana halisi ya jf.
Jiulize wewe binafsi toka umejiunga jf ume add value ipi?
Sawa King Kong ila matumizi ya maji ni endelevu si ukichimba utaendelea na kumaliza ujenzi lakin matumizi ya maji hayakomi mf kwangu mimepanda miti mingi sana kiasi watu wanapaita pale penye miti mingi hahaha na niliweza kuikuza kwasababu ya maji na hata kumwagilia kuta na zege ili ikomae inakuwa rahisi tofauti na maji ya kununua maana ijulikane kuwa cement haiitaji joto wala jua kali, inahitaji ubaridi ili ikomae na kukauka vizuri, ikipata joto inaungua na ndo maana kuta zinabanduka au kupata nyufa
Nakubaliana na mleta mada kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa maeneo mengine makubaliana na Makamee pamoja na King Kong. Suala la fundi pamoja na msimamizi ni la kuzingatiwa sana, inatakiwa wawe ni watu wenye uelewa mpana katika hii fani ya ujenzi, hasa msimamizi. Binafsi nimekwisha kumbana na mafundi wengi tena kwa kuelekezwa na mtu kwamba anaye fundi mzuri kumbe hamna kitu, ni fundi wa kupanga tofali na kupiga plaster. Mafundi wengi hawajui masuala ya "ratio" wengi hawajui vipimo vya zege, fundi anakwambia ununue nondo za 12mm kwa ajili ya kusuka colum au beam, na anatumia nondo 3 bila kuweka rings za kushikilia hizo nondo. Ushauri wangu, kama hauna uelewa na mambo ya ujenzi mtafute mtaalamu wa ujenzi akupe ushauri, siyo lazima asimamie unaweza kumtumi kukupa ushauri tu. Kumbuka unaweza kukwepa gharama lakini baada ya muda mfupi ukaingia gharama kubwa kuliko za mwanzo, kv msingi na kuta kupata nyufa au rangi ukutani kupata fangasi.
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.
We umewahi kujenga?