Ni sawa kabisa Kyenju ila hapa nilimaanisha wale watu ambao wana a, b, c za ujenzi ila hawana muda wa kusimamia na ndo maana nikashauri uweke mtu wa karibu ili akae pale toka asubuhi then wewe muhusika unaenda jion kureview mf mimi ilitokea unarudi jion unakuta kuta au beam imepinda na ililazim baadhi ya kuta kuzivunja na tukaanza upya. Au unakuta kona haina square ila kwa ambae hana muda kabisa basi ni vizuri aweke na apate msimamizi mwenye uelewa.
Kimsing hapa changamoto ni mbili.
Kuibiwa vifaa na ubora wa ujenzi
Kweli kuelewa kazi. Hivi huoni kama mleta mada anaongelea gharama nafuu? Sasa gharama nafuu na kumkabidhi engineer wapi na wapi? Kwa maisha ya mtanzania wa kawaida hivi katika nyumba 10 ukizichagua bila bias ni ngapi utaona zilisimamiwa na mkandarasi? Hapa kinachoongelewa ni nyumba za kawaida.
Naomba ufanunuzi kuhusu hizo unazoita nyumba za kawaida.
Zinajengwaje kwa makaratasi au?
Patamu hapo Makame hebu rudia tena maana ni patamu sana hapo
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.
Si lazina awe engineer anaweza kuwa architect or Quantity Surveyor pia tena engineer awe structural engineer mana ma engineer wapo wengi hata IT na electrical wote engineer but hawana sifa za kusimamia
Ndo umeandika nini? Sisi tunazungumzia mimba wewe unatuletea vitambi.
Huu ni uchambuzi wa ujenzi wa kilocal sana,nyumba kama nyumba ujenzi wake husimamiwa na injinia mwanzo mwisho,hiyo ujenzi kusimamia mke wako labda unajenga kibanda cha mama lishe.
Hapo ndo tunapokosea watanzania,
Kwako wewe nyumba ya kawaida ni ipi?
Unapompeleka site mke wako asie na ujuzi wa chochote kuhusu ujenzi ina maana gani?
Huyo haendi kusimamia ujenzi bali anaenda kumlinda fundi asiibe matirial yako ya kubangaiza.
Heading na maelezo vinakinzana. Sijaona wazo lolote jipya uliloleta la kupunguza gharama za ujenzi. Unless kama ni fundi na unatafuta kazi!
Safi sana Nyamgluu hii ndo maana na lengo la kuanzisha huu uzi ili tupeane ideas,
Nakubariana na swala la corridor na paa ila sujaelewa hapo kwenye madirisha kuwa kati, pls fafanua.
Mimi jikon kwangu hakutunzwi chochote mf masufuria, chumvi, etc kila kitu kinakaa stoo ambayo iko jiran na jiko na jikon panabaki majiko tu. So vitu vinatolewa stoo wakat vinahitajika na kurudishwa stoo vinapokuwa havitumiki, that means jiko muda wote halina chombo na ni safi
Pia nimeweka balcon mbele ya nyumba ambayo inatosha ku accomodate sub sitting na sub dinning ndogo maana sitaki kila mgeni aingie main sebure au dining kuu. So pale mbele pana set za viti na meza kama ilivyo sutting na dining. Kwa hiyo kuna sitting rooms mbili na dinning rooms mbili.
Pia nikaweka milango ya kutoka njee iko minne.
1.Mmoja uko jikon
2.Mwingine unakutoa nje upande wa kushoto
3.Watatu unakutoa nje upande wa nyuma mkabara na main door
4.Plus main door
Halafu sikuweka mbwembe lakin almost zaidi ya nusu ya ukuta wa dinning ni grili tu ili kupata mwanga na hewa, kesho ntaweka picha.
Pia sitaki kwangu itumike extensions za umeme, so nimeweka sockets za kutosha kwa maana kwamba kila kitu kichomekwe ukutani na zaidi nimeweka system mbili tofaut za umeme kwa kila kitu...taa na sockets yaan zipo zenye umeme wa solar na zipo za tanesco