Njiapanda: Mtoto wa mke wangu niliyemlea tangu ana miaka 2 ameenda kutoa mahari bila kunishirikisha

Hongera saana bro umepambana sana hapa ulipofika
 
Ila duniani watu wana jeuri yaani Baba kamlea kwa taabu kweli na kumsaidia kusoma hadi kupata kazi leo anaanza dharau. Daah inauma sana
 
Huyu jamaa msaniii ,usicheze na tekinilojia
 
Ni vizuri uchukue likizo kwanza ukakae home na watoto wako.

Pia kuwa makini pia je hao watoto wote 6 ni wa kwako? Hawa wanawake ni wajanja sana
 
Ingewezekana ukamharibia dogo ajira yake itakuwa poa sana japo najua ni ngumu, ila ukitumia umafia inawezekana, mpandikizie nadawa ya kulevya au silaha nyumbani kwake, kwa kutumia mafia afukuzwe kazi akili zitawakaa sawa.
🤣🤣🤣🤣daah
 
Piga talaka huyo mkeo na huyo mtoto uliyemlea achana nae,wewe ulisha fanya wema kwao na Mungu atakulipa tu,

Weka akili yako kwenye malezi ya watoto wako,jaribu kua nao karibu.
Mbona unarahisisha sana talaka jamaa ndio kwanza amegudundua tatizo kwanini wasiongee
 
Huyu jamaa msaniii ,usicheze na tekinilojia
Sidhani kama ni msanii. Humu stori zinazokuja huws hazimhusu mwandishi moja kwa moja zingine ni za jamaa zetu na majirani na ndigu. Huwa tunavaa uhusika ili kuvuta attention na mawazo chanya ili tujua cha kuwashauri wenzetu wanaopitia mitihani.
 
Ila duniani watu wana jeuri yaani Baba kamlea kwa taabu kweli na kumsaidia kusoma hadi kupata kazi leo anaanza dharau. Daah inauma sana
Zitakuwa ni akili za mama ake hizi.... Naamini dogo hana kinyongo na mzee kabisa sema anashauriwa vibaya na mama ake..
 
Muda umekwenda sana imagine jama kaoa ana miaka 20 plus miaka 19ya dogo maana yake yuko na 30+.

Usipokuwa makini na maswala ya mwenza unajikuta muda wa uhai wako woote wewe umesindikiza wengine duniani.
Aminii mkuu...!! Wapo watu wamefanikiwa lakini hawaenjoy kabisa mafanikio yaoo... sababu ya ndoa zao kuwa za motooo
 
Shituka wewe…….. Mkeo itakuwa karudiana na mzazi mwenzie kapime DNA hao watoto 6.
 
Mkuu huyo wife wako anafanya juu chini ili hata ukistaafu usije ukagusa hela za huyo mtoto wake, anataka ahudumiwe pekeake,
au laa tayari mtoto ameshamjua baba yake na wanawasiliana
Jibu hili hapa kwa hio chief emu jiongeze tu hapo ulikua unailea Mali (asset) ya mtu mwingine, akili aliyoitumia huyo mkeo anaijua mwenyewe ila ukweli upo wazi kwamba mkeo itakua kaongea na mtoto wake na kumtengenezea mazingira ya kujiweka kando na wewe ila yote kwa yote usisahau maana halisi ya mwanaume hivyo ni vitu vidogo tu kijana wako wa kufikia kutokua na mawasiliano mazuri na wewe isikupe shida una asset 5 ziimarishe sasa zifike kwenye level zaidi ya hiyo moja ambayo sio yako (huyo mtoto sio wa wako) asikuumize kichwa na isikuumize kichwa pia hata hao watoto 5 unaowasema umezaa na huyo mkeo yanaweza ikawa asset zako hapo ni 2 tu ila 3 zote mama kauza mechi kwa Siri yaan wana baba zao ambao wewe hauwajui maana wewe pia umedodosa kwamba ulikua una katabia ka kuchepuka mara mbili tatu hivi unategemea yeye hajawahi kuuza mechi (kuchepuka) kwa Siri bila wewe kujua Kisha unakuja kushtuka kashika tumbo ana mimba, hivyo basi jikaze mwanaume 39 yrs ni parefu sio wa kulialia mapenzi hakika pia kumbuka ndoa ni akili kwa hio inabidi uitumie akili yako vizuri unapokua kwenye ndoa ili usije ukafanya maamuzi ya ajabu yatakayo ishangaza dunia, tuliza moyo kisha tumia akili yako vizuri usikurupuke kufanya maamuzi ya ajabu
 
Tafuta muda uongee nao wote kwa kina kama hawatabadilika waache waendelee na mambo yao ipo siku watakutafuta yatakapowakuta ya kuwakuta.
 
Tuliza moyo mkuu hiyo ndo kawaida ya stepsons wengi, ingekua ni wakike basi uyo mtoto angekupenda sana

Nimesoma Mbande nikakumbuka site yangu huko ngoja niende nikaicheki.
 
ulioa ukiwa na umri wa miaka 17? Ulianza mahusiano na mkeo ukiwa na umri wa miaka 15? Maelezo yako yanaonesha ulizaliwa mwaka 1985.
 
I think kuna kitu nyuma ya pazia sizani kama mtoto na mama ake ni mashetani kiasi hicho waanze tu kuku ignore, i wish tupate stori ya upande wa pili
 
Nani kasema mwanajeshi mbn unakurupuka hivyo mkuu nimesema wapi mimi no mwanajeshi???
We sajini acha ushamba mwenyewe niliposoma tu kisa chako nikajua we mjeda sasa unaficha nini? na huyo mwanao int ya 39 wala asikusumbue kichwa we hujui askari mpya alivyo na tambo na kuona askari woote aliowakuta hawana akili yeye ndo ana akili, basi tulia tuliiii atarudi tu na michozi mixer makamasi mpe muda huyo na kuhusu mkeo sikufichi wakiamua ubaya wameamua hao usikute wakikaa na mwanae wanakusema ulikuwa unawatesa 😂😂😂 we kula maongezeko yako bwana poti sugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…