Njombe: Ajinyonga hadi kufa kwa kunyimwa unyumba na mkewe ambaye alidai mume hajaokoka

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Damas Mgaya (38), mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake kwa kutumia kamba ya kiatu, kufuatia madai ya mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa jana, Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi, akieleza kuwa marehemu alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha.

Kwa mujibu wa Kamanda Banga, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na kutokuelewana kati ya marehemu na mkewe kuhusu masuala ya ndoa na tendo la ndoa.

Inadaiwa kuwa mke wa marehemu alikataa kushiriki tendo la ndoa akieleza kuwa mumewe hajaokoka, hali ambayo inadaiwa kuchangia mgogoro huo wa kifamilia na kumsababishia marehemu msongo wa mawazo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Banga ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhimiza mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano katika familia na jamii, huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua kwa vitendo vinavyokiuka sheria.
 
SI angenyonga kichwa cha chini kwa mafuta au sabun badala ya kichwa cha juu
Omba YASIKUKUTE

Jamaa katuangusha sanaa wanawake ni wengi sana

Mimi hata nikimpenda mtu nafanya moyo wangu unakua complicated ku hill unatafuta Mwanamke mwingine soon moyo unapoa na unaanza kumuona wa KAWAIDA

Hakubabaishi tenaa
 
Damas Mgaya (38), mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake kwa kutumia kamba ya kiatu, kufuatia madai ya mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa jana, Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi, akieleza kuwa marehemu alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha.

Kwa mujibu wa Kamanda Banga, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na kutokuelewana kati ya marehemu na mkewe kuhusu masuala ya ndoa na tendo la ndoa.

Inadaiwa kuwa mke wa marehemu alikataa kushiriki tendo la ndoa akieleza kuwa mumewe hajaokoka, hali ambayo inadaiwa kuchangia mgogoro huo wa kifamilia na kumsababishia marehemu msongo wa mawazo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Banga ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhimiza mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano katika familia na jamii, huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua kwa vitendo vinavyokiuka sheria.
Hapo kuna Tatzo lingine sio papuch 2.
 
Back
Top Bottom