Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni

Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni

Pole nyingi kwa watoto na wote waliofiwa, ni huzuni kubwa tunaposikia habari hizi tunatamani isingekuwa hivyo lakini imesha kubwa na hatuwezi kufanya isiwe tena.
Tukio hili halitamfadisha kwa namna yoyote huyo mtuhumiwa hata kama yeye alikua amefanyiwa ubaya kiasi gani, iwe kwetu funzo kwamba maisha yana thamani kubwa kuliko ubaya wowote, tuanishi mara moja tu katika ardhi hii ya dunia, tuyathamini maisha kuliko hisia na maslahi yetu yote.
 
Shetani ameingilia hii taasisi ya ndoa
Shetani mnamuonea.
Mpaka inafikia hatua hii,kuna badhi ya mambo yanakuwa yameendelea kwa mda sana. Sema tu wahanga wa haya mambo,ni watoto. Hii taasisi usipokuwa mvumilivu,unaishia pabaya. Ebu,jiulize hao watoto maisha yao yatakuwaje! Hata ndugu wakiwachukua,kuwatenganisha tu,kikwazo. Na pengine si kwamba huyo mama alikuwa hayaoni,ila alikaa tu kwa ajili ya watoto wake.
Au nae mama kauli za ukauzu zilizidi jama nae uvumilivu ukamshinda.

Mbona simpo tu. Hamuelewani,tafuteni uongozi na watu wazima,mjue watoto watalelewaje. Sema tu,wakiachana,kesho wameshapata wenza tena,watoto wanaenda kuteseka.
Serikali ingekaa na kuangalia namna ya kupunguza au kukomesha huu upuuzi,maana miaka 20-30 mbeleni,ni shida. Huyu mtoto kuoa na kuolewa ni tabu tupu
 
Mkuu wa Polisi wilaya ya Makete mrakibu mwandamizi wa Polisi Assel Mwampamba amesema tukio hilo si la kawaida na kutoa ushauri kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwa na namba za jeshi la Polisi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza "Hili lingezuilika sasa ametoka na Panga mkakimbia wote na wanaume acheni uwoga yaani mtu yuko mmoja anacharanga mtu ninyi mmekimbia mngekuwa mnamrushia mawe asingeendelea kukata mtu pale"
Lakini mh afande wananchi wangemrushia mawe na kumuua huyo muuaji kabla hajatelekeza hilo tukio mngewakamata tena kwa kujichukulia sheria mkononi.
 
Kamuua vibaya sana japo hakuna kifo kizuri ila hiki hapana
Nakosa lugha nzuri ya kuandika ila tuwe wavumilivu kwenye ndoa Kuna mitihani migumu sana
 
Sasa kama ni mboga mbona haionekani?
mkuu tofautisha kati ya Njombe na makete.Makete ipo mkoa wa njombe,yawezekana umeishi njombe mjini hujaingia makete.Makete kule kwenye milima ya kulima ngano,bangi ilikuwa inaota yenyewe.Hata mking'oa huu mwaka,mwakani ipo tena.
kale ka ukanda ka kutoka pale makete mjini kwenda bulongwa,unakujua kisajanilo?then utapita masalala,uje utanziwa,uitafute ilolo,uende igalula,uende madege,uitafute ndamba then ije ikusi uione bulongwa🙂
ingawa sijarudi mitaa ile zaidi ya miaka 11 sasa,labda mambo yamebadilika
 
Back
Top Bottom