Njombe: Katekista wa Kanisa Katoliki apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kubaka

Njombe: Katekista wa Kanisa Katoliki apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kubaka

Huu uzi unanikumbusha haya ..
 
Hili tatizo halihusiani na imani ya mtu bali linamuhusu mtu husika aliye fanya kitendo hicho,hili ni tukio baya sana haijalishi limefanywa na mtu mwenye imani ya dini ipi,hili ni jambo la kukemewa na kila Binadamu mwenye utimamu wa akili.
Kapiga kavu ,na hulka yake nasio hulka ya kanisa
 
Ila angekuwa sheikh, ungehusishwa uislam
Sana Tu mkuu, Ila kwakuwa waislamu siku zote tunaamini katika haki Kwa mujibu wa Dini yetu ndio maana tunaona sio sahihi kulaumu taasisi badala ya mtu
 
Kitanzi tu halali yake yanajaza magereza tu
 
Njombe, katekista wa kanisa katoliki apandishwa kizimbani kwa kumbaka binti wa miaka 17 nyuma ya jengo la kanisa.

=======

Simon Njavike (43) ambaye ni Katekista wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Mlangali Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya hiyo akituhumiwa kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17.

Mwendesha mashtaka Angelo Marco mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ludewa Isaac Ayengo amesema Mshtakiwa Simon Njavike ambaye ni Mwalimu wa Watoto wa kipaimara akiwemo Binti huyo amekuwa akifanya vizuri katika mafunzo yake ya Kipaimara hivyo katekista alimpa Tsh. 10,000 kama zawadi ya kufanya vizuri kwenye mafunzo hayo.

Baada ya siku kadhaa Mshtakiwa alianza kumtaka kimapenzi lakini Binti huyo alikataa ndipo akaanza kudai kurudishiwa TSh. 10,000 yake aliyokuwa amempa lakini Binti alishindwa kuirudisha kutokana na kutokuwa nayo.

Ameeleza kuwa baada ya siku kadhaa Mtuhumiwa alimuita Binti nyuma ya kanisa majira ya mchana ambako kuna msitu na binti alipofika akamkamata kwa nguvu na kuingia nae katika msitu kisha akatimiza lengo lake na kutokomea kusiko julikana.

Polisi walifanya jitihada za kumtafuta na baada ya siku kadhaa alikamatwa na kufikishwa Mahakamani ambapo amekana shitaka hilo na kupelekea kesi hiyo kuahirishwa mpaka February 09 mwaka huu.

Millard Ayo TV
hii tabia ya wahudumu wa kiimani kubaka na kunajisi kwamini inaendelea?
 
Back
Top Bottom