Njombe: RC Mataka: sitaki kusikia mtu ameambiwa gloves hazipo kwa mama mjamzito kwa kuwa huduma ya mama na mtoto ni bure

Kama sera na muongozo wa wizara ya Afya unasema huduma za mama mjamzito kujifungua ni bure, sasa mjamzito anapodaiwa kulipa pesa ya kujifungua wakati huduma hizo ni bure hiyo pesa inakwenda kwa nani?
Yaaa ni Bure lakini uende na vifaa vyako
 
Huyu jamaa sio kiongozi mzuri maana kasifiwa mbio kapiliza nyumbani?

Naamini Bora mropokaji anayesema ukweli kuliko anayejifanya anabusara muongo.

Maana mkweli anafanya tujue Kuna tatizo tutalijadiri ila mwongo anayejifanya anabusara anafanya propaganda ionekane tatizo hakuna wakati lipo.
Sera ya afya ya taifa yote ni moja DSM na Njombe Sasa huyo mwongo atueleze hiyo budget wameitoa wapi ili tujue DSM wamefeli wapi
Mkuu huyu ndio mkweli. Kwasababu Sera inasema akina mama wajifungue bure. Kama hakuna dawa na vifaa tiba ndio serikali iwajibike kwa kuweka Sera wasioweza kutimiza. Ila hao wahudumu wanatakiwa hivyo vitu watoe bure visipokuwepo hakuna wa kuwalaumu. Sasa sio yule mropokaji anaelazimisha kana kwamba ndio Sera waliyoweka.
 
Kulea mimba ni gharama kuliko hizo gloves, tunachangia kwa kuwa ni wajibu wa maandalizi yenyewe ya kumpokea mtoto.
Labda ikiwa kuna mtu amepungukiwa ahudumiwe, ila ikiwekwa kuwa ni bure migogoro na wananchi inaongezeka
 
Sasa huyo jamaa atatengeneza bomu maana wanaume watagoma kutoa pesa za vifaa wakihisi wanapigwa na wake zao na kuwasababishia ugumu wa kazi wakunga
Labda imeanza sasa io bure ngoja tuone.
 
Mkuu huyu ndio mkweli. Kwasababu Sera inasema akina mama wajifungue bure. Kama hakuna dawa na vifaa tiba ndio serikali iwajibike kwa kuweka Sera wasioweza kutimiza. Ila hao wahudumu wanatakiwa hivyo vitu watoe bure visipokuwepo hakuna wa kuwalaumu. Sasa sio yule mropokaji anaelazimisha kana kwamba ndio Sera waliyoweka.
Ni ukweli je ndio serikali inachofanya maana atasabisha watumishi wa chini kabisa ambao wanamishara duni waonekane wanauza vifaa.

Inabidi iangaliwe kama wizara ya afya inapeleka badget na vifaa Kwa wakati maana analaumiwa mtumishi wa mwisho asiyejua chochote
 
Kama sera na muongozo wa wizara ya Afya unasema huduma za mama mjamzito kujifungua ni bure, sasa mjamzito anapodaiwa kulipa pesa ya kujifungua wakati huduma hizo ni bure hiyo pesa inakwenda kwa nani?
Wizara ya afya inatunga sera na miongozo lakini watekelezaji ni wengine. Wanasiasa wanachokosea ni kuwaambia wananchi huduma za uzazi na watoto chini ya miaka mitano ni bure halafu haipeleki fedha kulingana na gharama na mwisho wa siku vituo vinapoona vitacollapse vinawalipisha
 
RC wa Njombe na wa Dar ni wa nchi mbili tofauti!?
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amepiga marufuku wataalamu wa afya mkoani humo kutoza fedha wala vifaa tiba kwa mama mjamzito kwa kuwa huduma ya mama na mtoto ni bure, na kuwataka kufuata muongozo wa Sera ya Afya kwa usahihi.

RC Mtaka ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) ambapo amesema wanawake wajawazito hawatozwi gharama za kujifungua hivyo wataamu wa afya wanapaswa kutekeleza agizo hilo.

"Wanawake wajawazito hawatozwi gharama za kujifungua, sitakubali kusikiliza kwamba mtu ameenda hospitali ameambiwa ‘gloves’ haipo, nyuzi ya kushona haipo, sijui pamba haipo tusiruhusu hilo jambo", amesema RC Mtaka

Pia soma: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani.

View attachment 3225153
Ni kweli Huduma ni Bure au ni siasa tuu za kusagiana kunguni?
 
Utafikir nchi mbili tofauti
 
Back
Top Bottom