Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona hata yeye katoa Angalizo
Ungeweka picha ya hizo nyumba ulizojenga kwa Bei hiyo
Okay nitakuwa pia nawapa ushauri kamanda wangu maana nina uzoefu wa materials nzuri na za kawaidaNimekuelewa mkuu. Lakini pia kumbuka unawasaidia lushauri wanaotaka kujenga.
Kuna watu hata hiyo tofauti ya 28 na 30 haijui.
Hii inaweza kuwa fursa nzuri ukiweza kuwaelekeza watu namna ya kupata vitu vizuri kwa gharama nafuu. Kwenye ujenzi wanaojenga wanalalamika sana kupigwa na mafundi.
sawa DianaWeka picha ya kazi yako
kwa kuangalia kwa macho tu ni vigumu kutoa makisio haipungui 50million ukijumuisha na eneo la kiwanja.View attachment 1505039
Kama haka kanagharimu ngapi.?
He is smart ! Ameainisha yote hayo , !Hapo msingi hadi lenta kwa 4.9 M paangaliwe vizuri. Kuna vigezo vingi sana inabidi vitazamwe mfano aina ya udongo unapojenga, kiwanja hakina mwinuko upande mmoja au hakipo bondeni? Misingi ya maeneo tofauti itatofautiana kukidhi hivyo vigezo. Bei haiwezi kufanana.
Kuna Uzi humu mtu anataka kujenga chumba kimoja ana bajeti ya 6milions , nadhani ungemsaidia mawazo hayandiyo mkuu ni pamoja na tofali.
Ok nilikoseaana bajeti ya 3millions not 6millions kama sikosei na amepata fundi tayari.
Wakuu mko salama!
Ninaweza kukujengea nyumba kama utanipa ramani au nitakupa mimi ramani pamoja na kukuandalia bajeti kwa kila hatua. kuanzia msingi mpaka finishing.
Nikisema flat nina maana ya kujenga nyumba ambayo siyo ghorofa bali ni single roofing, isiyo na many floor.
Mfano nina design na kujenga nyumba za bei nafuu kabisa.
mfano nyumba ya kulala ya futi 10 kwa 10 ( chumba kimoja ) vikiwa vitatu, kimoja master, sebule jiko, dinning ,public toilet kwa kuanzia msingi mpaka lenta ni shilingi milioni 4,900,000 TZ tu.
NOTE: hii bajeti ni kwa eneo lenye mwinuko tambarare na udongo usio mkorofi kama udongo wa kichanga, pia kwa tofali za kuchoma au za block ambazo sio zile za inch 6 ikiwa ni tofauti na hapo bajeti itapanda kutoka 4.9 .
Na kama nyumba ikipauliwa na kumaliziwa madirisha yenye aluminium na milango ni shilingi milioni 17,900,000 TZ jumla kuu.
Gharama nyingine hazihusiki kwenye bajeti tajwa hapo juu, kama
kupiga gypsum powder,
gypsum body,
skimming, grouting,
tiles building,
sewage system za maji safi na taka pamoja na choo,
electrical suppliances & wiring,
kuframe wallpapers,
Kufunga rain gutters,
makabati ya jikoni na mables plus decorations nyingine hazihusishwi na bajeti ya juu.
Nicheki PM tufanye kazi na nikupatie msaada mzuri juu ya ujenzi wa nyumba yako nipo kwa ajili ya kukusaidia ndugu yangu pale unapoumiza kichwa utaweza vipi kujenga nyumba.
Au nipigie kwa nambari +255 678 502 276
Pia natoa ushauri juu ya ujenzi, usisite kunitafuta pale unapohitaji ushauri.
Ahsanteni wadau wenzangu.
shukurani mkuu Vladimir LeninUzi mzuri huu
kila la kheri ndugu, karibu na naamini utafanikisha.Mkuu Mr increase number yako nimeichukua nina kakiwanja kangu 30×25 nina mpango wa kujenga nyumba za kupangisha set 4 zenye sitting room,room mbili za kulala,choo na jiko dogo nataka nipabane patoshe naona wewe utanifaa.
Fundi ninaye wewe nitaweza kukulipa kwa ushauri tu hii ni project ni ya mwakani ngoja nipambane kujikusanya kwanza.
Sent using Jamii Forums mobile app