Njoo tuambizane ni nani ungependa kukutana naye

Njoo tuambizane ni nani ungependa kukutana naye

Life starts at 45

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2015
Posts
998
Reaction score
987
Wakuu unajua kuna muda unasema ningekutana na mtu huyu basi ningependa kujua moja mbili tatu, basi hapa ni mahala pako pengine ukapata nafasi hiyo.

Mimi binafsi ningependa kukutana na wafuatao


1. John Pombe Magufuli (Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
[emoji117] Huyu swali langu kubwa ningependa kujua ni vipi aliweza kupambana na Corona au ni kitu gani aligundua kipo nyuma ya pazia maana haiwezekani mpaka leo bado jirani zetu wanapambana nayo.

2. Pastor David Mmbaga
[emoji117] Huyu ningemuuliza ameweza vipi kuwa na imani aliyonayo maana mimi bado naferi kila nikijaribu angalau kuifikia nusu ya iman yake, japo nina imani ipo siku nitaifikia.

Vipi wewe mdau ungependa kuonanna na nani na ni vitu vipi ungependa kufaham kutoka kwake?
 
Ningependa kuonana na alietoa wazo la kusajili kwa alama za viDoLe!

Ningependa kuonana na alietengeneza ulimwengu Kuna maswali kuntu ningependa nimuhoji!
 
Ningependa kukutana na founder wa IPhone nimuulize kinagaubaga kwanini aliamua kung’ata lile apple nyuma ya iPhone?ndo hivyo tena haiwezekani 🥺
😂😂😂😂😂😂😂
 
Yale ya kitaalam ....alafu jina jina mbona unanitakiaa kesi za kujib chief[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nitende kosa mimi halafu kesi ujibu wewe?[emoji1782]
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom