Pay respect to your warriors.
Mnakosa kazi za kufanya kuja kudanganyana habari msizozijua kuhusu komandoo na ukomandoo wenyewe!
Najua wengi mnabeza sana jeshi la nchi yenu linaloundwa na ndugu zenu ( watanzania) na kuhusudu majeshi ya mataifa mengine msiyo hata na uelewa nayo.
Ndugu Wanajamiiforums, komaando/komandoo ni askari wa jeshi la nchi ( nchi yoyote Ile) aliyepewa mafunzo maalumu ya kufanya operation za kijeshi kwenye mazingira magumu, kupambana na ugaidi, kuhujumu ngome na vikosi vya adui pamoja na kuvisaidia vikosi vya jeshi.
Kama ilivyo nchi nyingi duniani, jeshi la Tanzania Lina vitengo maalumu vya ukomandoo katika kamandi muhimu tatu;
Yaani 1. Nchi kavu
2. Anga
3. Wanamaji
Wanajitoa katika Hali ngumu ambazo raia wa kawaida ( civilians) hawawezi kufahamu.
Wakati tukinywa bia, shisha na mademu night club, Kuna wenzetu wako makini na mipaka ya taifa hili.
Niwaambie tu, mmewazoea sana hao makomandoo na kufikia hatua ya kuwakejeli mtakavyo labda ni kwa sababu Huwa wanafanya maonesho mepesi ya kimedani kwenye sikukuu za kitaifa.
Hayo ni madogo sana kati ya mengi wayafanyayo. Kuwaheshimu na kuwaombea ni Vema zaidi kuliko kuwadharau na kuwajadili katika namna isiyofaa.
Kufuzu ukomandoo ni kazi ngumu sana ambayo si kila mwanajeshi anaweza kufikia. Ni wiki+ miezi+ na miaka hutumika kumuandaa komandoo.
Wanajeshi wasio makomandoo wanawaheshimu sana makomandoo lakini raia wa kawaida wa jamiiforums anajua kupima hadhi ya ukomandoo kwa mizani yake.
Ni ngumu sana kuwasihi watu wakaachana na mambo wasiyoyajua, hii ni kwa sababu wanataka kujifurahisha na kukejeli watakavyo.