Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Kwa sasa bado mkuu mambo yangu hayajanikalia sawa kwa ajili ya kwenda huko nina mishe nyingine mpaka niziweke sawa ndio nitaanza kwenda huko.

Tafuta sehemu nyingine yakwenda kufanya biashara lakini sio Burundi .....Mimi nipo Kigoma na Burundi tunaenda mara kwa mara lakini sio sehemu salama kabisa na warundi Wana maisha magumu sana asikwambie mtu
Asee mi naamini kuna fursa kwenye hizi nchi zenye uchumi wa chini na watu wanazidharau. Mi Burundi ntaenda tu liwalo na liwe. Napenda kupata mwongozo kwa waliowagi kwenda huko kuhusu utaribu wa kuingiza vyakula na ushuru wa mazao upoje.
 
Kama unaona haja ya kwenda Burundi njoo tuungane. Tuwe wabongo wawili watatau tunaenda pamoja kusoma gape. Kuna washkaji zangu Warundi wapo Bujumbura na wapo tayari kutupokea na kufanya biashara na sisi. Nimefuatilia usafiri ni kuanzia 80,000 mpaka 100,000 kutoka Dar - Bujumbura. Kama una passport inagongwa bure unaingia. Ila kama huna utalipa mpakani Tsh 40,000. Mpaka sasa tupo watanzania 3 tulio tayari kwenda. Ukipenda jiunge nasi. Nipigie 0756981717.
 
Tanzania ilivyo kubwa na fursa kibao ya nini kwenda burundi kufanya umachinga.kama unaenda Burundi fine ila uende kama muwekezaji na mtajii wa maana sio chinga,k wanza usalama mdogo na ni masikini kuliko sisi,
Hata sisi ni masikini bado wanakuja watu kutoka mbali huko wanafanya biashara kwetu
 
Tanzania ilivyo kubwa na fursa kibao ya nini kwenda burundi kufanya umachinga.kama unaenda Burundi fine ila uende kama muwekezaji na mtajii wa maana sio chinga,k wanza usalama mdogo na ni masikini kuliko sisi,
Ingekuwa bora sana kama ungetupa walau fursa 3 ulizoziona wewe hapa nyumbani mkuu.
 
Sisi sii masikini trust me hii nchi inautajiri mwingi sema tu wananchi wamesinzia
Mkuu ipo hivi ukiwa na mtaji wa Tsh 2,000,000/- kwa hapa kwetu ni mtaji wa kawaida sana, lkn hiyo hiyo pesa ukiwa Burundi unafanya biashara kubwa na inaonekana

Mimi nimefika Burundi mara kibao na mwaka huuhuuu january nilikuwepo kule napajua vzr, ni sehemu nzuri sana ya kuwekeza hasa kwenye mavazi, chakula na vipodozi (japo hapa kwenye vipodozi warundi sio watu wa manukato sana nazungumzia pafyumu sana sana ni losheni

Narudia tena biashara ipo, nenda ukaone pia usalama upo wa kutosha nenda
 
Asante mkuu ntafanya hivyo
 
Wanadhulum sijapata kuona! Mlipane mkono kwa mkono. Jamaa alinidhulum mzigo wa sangara parefu na akataka kuniua hotel. Ukiwa burund huo umaskin wa kutisha sikuona maisha ni kama bongo tu. Changamoto ni zile zile. Sema vijana wa kule tatzo la ajira ni kubwa mno na wana wepes wa kutumia nguvu kupata na uasi.
 
Mnipitie mpakani huku Mnanila center twezetu Burundi, ila kitu kimoja ambacho huwa kinawavunja watu moyo ni uvamizi wa mara kwa mara njiani, yaani warundi hawanaga mchezo tunaishi nao tunawafahamu,
 
๐๐š๐จ๐ฆ๐›๐š ๐ง๐ข๐œ๐ก๐š๐ง๐ ๐ข๐ž ๐ฆ๐š๐๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ค๐š๐ฌ๐ข ๐ค๐ข๐๐จ๐ ๐จ, ๐›๐ฎ๐ซ๐ฎ๐ง๐๐ข ๐ง๐ข๐ค๐ฐ๐ž๐ฅ๐ข ๐ค๐ฎ๐ง๐š ๐ฎ๐ฆ๐š๐ฌ๐ข๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ค๐ฎ๐ญ๐จ๐ค๐š๐ง๐š ๐ง๐š ๐ง๐š๐ฆ๐ง๐š ๐ฌ๐ข๐ฌ๐ข ๐“๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š ๐ญ๐ฎ๐ง๐š๐ฐ๐š๐ณ๐ข๐๐ข ๐ญ๐ก๐š๐ฆ๐š๐ง๐ข ๐ฉ๐ž๐ฌ๐š ๐ฒ๐š๐จ( ๐Ÿ๐š๐ซ๐š๐ง๐ ๐š) ๐ฒ๐š๐š๐ง๐ข ๐ฎ๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ง๐š ๐“๐ฌ๐ก,1000/= ๐ฎ๐ค๐ข๐ž๐ฑ๐œ๐ก๐š๐ง๐ ๐ž ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐๐š ๐Ÿ๐š๐ซ๐š๐ง๐ ๐š ๐ฎ๐ง๐š๐ฉ๐š๐ญ๐š 1200/=, ๐ง๐š ๐ค๐ฎ๐ง๐š ๐ญ๐ข๐ฆ๐ž ๐ก๐ฎ๐ฐ๐š ๐ข๐ง๐š๐ฉ๐š๐ง๐๐š ๐ณ๐š๐ข๐๐ข.
๐•๐ข๐ญ๐ฎ ๐ฏ๐ข๐ง๐š๐ฏ๐ฒ๐จ ๐ฎ๐ณ๐ข๐ค๐š ๐ค๐ฎ๐ฅ๐ž ๐ค๐ฐ๐š ๐ฎ๐ก๐š๐ซ๐š๐ค๐š ๐ฌ๐š๐ง๐š ๐ค๐ฎ๐ฅ๐ž ๐ง๐š ๐ฎ๐ค๐š๐ญ๐ž๐ง๐ ๐ž๐ง๐ž๐ณ๐š ๐ฎ๐ญ๐š๐ฃ๐ข๐ซ๐ข ๐ง๐ข,
1.๐ค๐š๐ซ๐š๐ง๐ ๐š
2.๐ฆ๐œ๐ก๐ž๐ฅ๐ž
3.๐Œ๐š๐ก๐ข๐ง๐๐ข.
4.๐Œ๐ข๐ก๐จ๐ ๐จ ๐ข๐ฅ๐ข๐ฒ๐จ ๐ค๐š๐ฎ๐ค๐š( ๐ค๐š๐ฆ๐›๐š๐ซ๐š๐ง๐ ๐š).
5 ๐Œ๐š๐ ๐จ๐๐จ๐ซ๐จ
6.๐’๐ข๐ฆ๐ฎ
๐‡๐ข๐ฏ๐ฒ๐จ ๐ง๐ข ๐›๐š๐š๐๐ก๐ข ๐ฒ๐š ๐›๐ข๐๐ก๐š๐š ๐ฎ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐ฉ๐ข๐ ๐š ๐ฉ๐ž๐ฌ๐š ๐ฆ๐ฉ๐š๐ค๐š ๐ฎ๐ค๐š๐ค๐ข๐ฆ๐›๐ข๐š

๐•๐ข๐ญ๐ฎ ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐จ ๐ฎ๐ง๐š๐ฐ๐ž๐ณ๐š ๐ค๐ฎ๐œ๐ก๐ฎ๐ค๐ฎ๐š ๐ค๐ฎ๐ฅ๐ž ๐ง๐š ๐ฎ๐ค๐š๐ฅ๐ž๐ญ๐š ๐“๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š ๐ฎ๐ค๐š๐ฉ๐ข๐ ๐š ๐Ÿ๐š๐ข๐๐š ๐ณ๐š๐ข๐๐ข ๐ค๐š๐ฆ๐š ๐ฎ๐ญ๐š๐ฉ๐š๐ญ๐š ๐ฌ๐จ๐ค๐จ ๐ฅ๐š๐ค๐ž .
1. ๐•๐ข๐ญ๐ž๐ง๐ ๐ž ๐ง๐š ๐ค๐ก๐š๐ง๐ ๐š
2. ๐’๐š๐›๐ฎ๐ง๐ข ๐ณ๐š ๐›๐ฎ๐ซ๐ฎ๐ง๐๐ข.
3. ๐ฏ๐ข๐Ÿ๐š๐š ๐ฏ๐ฒ๐š ๐ฎ๐ฆ๐ž๐ฆ๐ž.
๐ก๐ข๐ฏ๐ข ๐ง๐ข ๐›๐š๐š๐๐ก๐ข ๐ค๐ฎ๐ญ๐จ๐ค๐š๐ง๐š ๐ง๐š ๐ ๐ก๐š๐ซ๐š๐ฆ๐š ๐ฒ๐š ๐ค๐ฎ๐ฅ๐ž ๐ฏ๐ข๐ฉ๐จ ๐›๐ž๐ข ๐ฒ๐š ๐œ๐ก๐ข๐ง๐ข ๐ณ๐š๐ข๐๐ข ๐ง๐š ๐ฎ๐ค๐ข๐Ÿ๐š๐ง๐ข๐ค๐ข๐ฐ๐š ๐ค๐ฎ๐Ÿ๐ข๐ค๐ข๐ฌ๐ก๐š ๐“๐ณ ๐ฎ๐ง๐š๐ฉ๐ข๐ ๐š ๐Ÿ๐š๐ข๐๐š ๐ฆ๐š๐ซ๐š ๐ฆ๐›๐ข๐ฅ๐ข.
๐๐š๐จ๐ฆ๐›๐š ๐ค๐ฎ๐ฐ๐š๐ฌ๐ข๐ซ๐ข๐ฌ๐ก๐š
 
Kuna sehemu nakuelewa ila kubali tu burundi ni masikini east africa nzima
Kwani wewe unaenda Burundi kufuata umaskini wao ama kufuata fursa za biashara. Nadhani lengo lako kwenda Burundi likifikiwa unaweza kufanya maamuzi sahihi ya kwenda ama hapana. Vinginevyo Dangote angeenda kuwekeza kiwanda cha Saruji Washington DC USA na sio Mtwara kuchere.

Cc. Ngosha Mashine
 
Gharama za kupitisha mpakani
 
Mnipitie mpakani huku Mnanila center twezetu Burundi, ila kitu kimoja ambacho huwa kinawavunja watu moyo ni uvamizi wa mara kwa mara njiani, yaani warundi hawanaga mchezo tunaishi nao tunawafahamu,
Acha kutisha watu wewe jamaa. Uvamizi uvamizi, kwani wao wanaishije na huo uvamizi. Acha watu waende kujionea na wakienda usidhani watakuzibia fursa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ