Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Burundi kupo peace sn nimekaa huko 2017 hadi 2018 tena wakijua ww ni mtz wanapenda sn watanzania, maisha ni simple sn buja chakula Chao kikuu ni ugali hasa wa mhogo ila ni mtamu sn na mweupe kama sembe ukipata na dagaa wa ziwa nyasa wakikaangwa na vile vitunguu vyao dah noma sn ntarudi buja coz nilitengeneza connection ya watu wema huko
Vipi mademu wa kirundi?
 
Nina sabuni na mafuta ya nywele nilitamani kuyapeleka huko Ila Sina connection, any help wadau
 
Burundi kwa sasa matumizi ya dola sio kama zamani, kwa sasa hadi uagizaji wa mafuta umekuwa wa kusua sua mimi nina jamaa zangu wengi tuu wanahusika na malori na mara kwa mara wananipa update ya huko ikoje kwa sasa,

jana tuu nilikuwa naongea na dereva mmoja ambaye nlitaka aniletee sabuni za nyota nne nikamuuliza kama hali ya kukosekana kwa mafuta bado kupo na akanieleza bado yanasumbua,

na sababu kubwa ni waagizaji wa mafuta hawaruhusiwi kuuza kwa dola wanatakiwa watumie faranga kitu ambacho wao kwenye soko la dunia kuniwapa wakati mgumu kwenye manunuzi.

Na kuhusu benki CRDB najua bado ipo nakumbuka panaitwa buyenzi ndio tawi lipo hapo na usalama upo si kama baadhi ya watu wanavyosema hapa maana ingekuwa si hivyo madereva wetu wangesema tuu hali ikoje.

Mkuu fanya kutembelea eneo husika usiogope sana kujifunza mimi mwenyewe natarajia kwenda huko ndani ya miezi mitatu ijayo nataka nifanye biashara ya mazao na hizo sabuni.

Ila pamoja na umasikini wa Burundi bado mafuta kwao ni bei rahisi kuliko kwetu na mafuta yao kwa asilimia kubwa yanapitia kwetu.

Miji iliyochangamka ni Gitega,Ngozi, Muyinga na Bujumbura yenyewe na kwa hakika ukifnikiwa kupata bidhaa zako zikaenda sawa sawa mafanikio utayaona tuu.

Japo na watu wa kule wengi ni wabishi na majasiri sababu ya vita vita na baadhi walishaingia msituni lakini si kitu cha kukutisha sana cha msingi ishi na watu vizuri upate kufanya biashara zako kwa amani kabisa...

twende zetu buja mkuu tuache uoga watanzania.
Feedback mkuu
 
Burundi nmekaa sana Muyinga kata Buthinda kata ya Kamara magambo. Kwa wachimba Dhahabu/Gold. Pamoja na Bujumbura City Cente( Buyenzi mtaa 8 nyumba na 23), Kinama ( Nyumban kwa Msanii Kidumu), Bwiza, Kirundo, Chibitoke( Kwa wachimba Dhahabu), Ngozi mji wenye chuo kikuu kikubwa, Ruyigi, Chanikuzo,Makamba, Gitega etc
Hakuna Ujambazi ambao watu wanasema.
Bidhaa za kupeleka ni Vyakula kama Mchele mzur, Maharage ya Njano pamoja na Tambi za St Lucia. Pia kama unaweza kupeleka Dagaa wa Kigoma wanasoko sana.
Kuhusu Pesa mara ya Mwisho rate ilikua 1Tsh kwa 1.6 Faranga. Us dollar haitumik sana. Pia ukiwa boader ya Kabanga sehem za kuchange pesa zpo nyingi sana.
Biashara za Electonic zinalipa sana mikoa ya Muyinga, Ngozi, Gitega. Laptop kwao bado zinauzwa Bei kubwa bado.
 
Umetoka lini huko mkuu?

Back
Top Bottom