Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Sawa mkuu me sijakataza mtu but tahadhari ni muhim pia
Burundi kupo peace sn nimekaa huko 2017 hadi 2018 tena wakijua ww ni mtz wanapenda sn watanzania, maisha ni simple sn buja chakula Chao kikuu ni ugali hasa wa mhogo ila ni mtamu sn na mweupe kama sembe ukipata na dagaa wa ziwa nyasa wakikaangwa na vile vitunguu vyao dah noma sn ntarudi buja coz nilitengeneza connection ya watu wema huko
 
Ndugu zangu kuna biashara nataka kujaribu kufanya ya kutoa bidhaa kariakoo kupeleka Burundi ila katika pitapita, nimegundua changamoto zifuatazo.

1. Mabadiko ya dhamani ya pesa ya Burundi
2. Ugumu wa kubadilisha fedha. Yaan ukiwa na faranga ni ngumu sana kuirudisha kuwa Shilingi.
3. Suala la usalama hasa unapokuwa na cash.

Naomba msaada kwa Mrundi au Mtanzania mwenye uzoefu au uelewa kwenye hayo masuala. Napenda kujua tofauti ya thamani ya fedha zetu pia bidhaa zenye uhitaji mkubwa Burundi zinazopatikana Bongo.

Shukran sana.
Ni thamani sio dhamani
 
Burundi kupo peace sn nimekaa huko 2017 hadi 2018 tena wakijua ww ni mtz wanapenda sn watanzania, maisha ni simple sn buja chakula Chao kikuu ni ugali hasa wa mhogo ila ni mtamu sn na mweupe kama sembe ukipata na dagaa wa ziwa nyasa wakikaangwa na vile vitunguu vyao dah noma sn ntarudi buja coz nilitengeneza connection ya watu wema huko
Sio wote ni wabaya but kunavisehemu sehemu kikinuka kimenuka kweli, vip ulifanikiwa kufika mkoa unaitwa makamba, je kule kuko vip
 
Mkuu ipo hivi ukiwa na mtaji wa Tsh 2,000,000/- kwa hapa kwetu ni mtaji wa kawaida sana, lkn hiyo hiyo pesa ukiwa Burundi unafanya biashara kubwa na inaonekana

Mimi nimefika Burundi mara kibao na mwaka huuhuuu january nilikuwepo kule napajua vzr, ni sehemu nzuri sana ya kuwekeza hasa kwenye mavazi, chakula na vipodozi (japo hapa kwenye vipodozi warundi sio watu wa manukato sana nazungumzia pafyumu sana sana ni losheni

Narudia tena biashara ipo, nenda ukaone pia usalama upo wa kutosha nenda
Dig more deep pls.....! If you can
 
Nataka nijue Zaidi kuhusu hizo sabuni maarufu kama Savona zinakuwa kwenye vi box vidogo piece 24 kwa kila ka box, hivi huko zinauzwaje
 
Dig more deep pls.....! If you can
Raia wengi wanaamini sana utapeli, mm Burundi napajua vzr usalama upo biashara pia ipoooo Harmonize aliwahi kuingia mkataba na kampuni moja ya sigara "YES" inatokea Burundi

Hapa tunajaribu ku-share fursa sio kutapeli kwanza mm sio Mrundi useme labda naitetea nchi yangu hapana

Kule fursa ipo, nikipata mda nitakucha kuchimba madini ya kutosha mkuu kwa faida ya wapambanaji

Maana isije kuwa wengine wanabisha na bado wanasikilizia michongo itiki huku wakiwa wamelala
 
Kwani wewe unaenda Burundi kufuata umaskini wao ama kufuata fursa za biashara. Nadhani lengo lako kwenda Burundi likifikiwa unaweza kufanya maamuzi sahihi ya kwenda ama hapana. Vinginevyo Dangote angeenda kuwekeza kiwanda cha Saruji Washington DC USA na sio Mtwara kuchere.

Cc. Ngosha Mashine
Kabisa mkuu, mm nimeuliza kitu ukitaja nchi tano kubwa kiuchumi duniani (tajiri) China huiachi harafu unakuta wachina wanafanya umachinga Kariakoo Tz nchi ambayo kwenye 100 ya nchi tajiri haimo, sisi na Burundi tofauti ipo lkn ni kidogo sana sisi ni wa 29 kutoka mwisho kiuchumi duniani
 
Sio wote ni wabaya but kunavisehemu sehemu kikinuka kimenuka kweli, vip ulifanikiwa kufika mkoa unaitwa makamba, je kule kuko vip
Nisiwe muongo huo mji wa makamba niliupita tu kwenye gari maana mie nilivukia boda ya tz na Burundi inaitwa manyovu, so ukivuka boda makamba ni miji ya mwanzo sn kwa muonekano ni pazuri sn kumekaa kama njombe hv ila kuna milima mingi sn na hali ya ubaridi flani hv kuna fursa sn za biashara coz niliona hekaheka sn pale, boy trust me buja usalama upo wa kutosha, ukitaka kuenjoy fursa za biashara fika hadi Burundi na Congo bukavu sio mbali sn na bunjumbura huko wacongo wanapenda sn hizi simu za iPhone. Ntarudi tena Congo japo now napanga kwenda mbali zaidi ya Africa
 
Me nipo manyovo mnanila mara nyingi napereka karanga sehemu moja inaitwa kayonzi, i kweli kuna baridi maana kuanzia miezi ya 5,mpaka 8 baridi huwa kali sana kiasi cha milima kufunikwa na hali kama ya mvuke/moshi mzito, kwa wazee wa biashara za mitumba hasa koti ,sweta na jaketi miezi hiyo ndo yakupiga pesa
 
Kama unaona haja ya kwenda Burundi njoo tuungane. Tuwe wabongo wawili watatau tunaenda pamoja kusoma gape. Kuna washkaji zangu Warundi wapo Bujumbura na wapo tayari kutupokea na kufanya biashara na sisi. Nimefuatilia usafiri ni kuanzia 80,000 mpaka 100,000 kutoka Dar - Bujumbura. Kama una passport inagongwa bure unaingia. Ila kama huna utalipa mpakani Tsh 40,000. Mpaka sasa tupo watanzania 3 tulio tayari kwenda. Ukipenda jiunge nasi. Nipigie 0756981717.
Safari lini niunge tela
 
Ndugu zangu. Naomba msaada zaidi kuhusu Burundi. Nataka kwenda sasa kupeleka viatu, yebo, pochi na bidhaa kadhaa za urembo za akina dada. Kwa mujibu wa taarifa za mabadiliko ya fedha, Franc ya Bururundi ipo juu yetu X2. Na CRDB wapo Burundi. Nauliza hivi, Je nikiuza bidhaa zangu kwa Franc alafu nikaweka CRDB nikiwa kule si itadouble? Alafu nakuja kuitolea Bongo ikiwa na faida X2? Msaada please.
 
Kwa Rwanda pakoje, maana naona hio Burundi ni masikini sana,na jamaa walio ingia msituni nao sio poa hao, nadhani watakua na tabia kama waZulu,naskia Rwanda ipo juu kwa kilakitu, mtupe ABC za kwa Kageme kdg
 
Back
Top Bottom