Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Sawa mkuu me sijakataza mtu but tahadhari ni muhim pia
Burundi kupo peace sn nimekaa huko 2017 hadi 2018 tena wakijua ww ni mtz wanapenda sn watanzania, maisha ni simple sn buja chakula Chao kikuu ni ugali hasa wa mhogo ila ni mtamu sn na mweupe kama sembe ukipata na dagaa wa ziwa nyasa wakikaangwa na vile vitunguu vyao dah noma sn ntarudi buja coz nilitengeneza connection ya watu wema huko
 
Ni thamani sio dhamani
 
Sio wote ni wabaya but kunavisehemu sehemu kikinuka kimenuka kweli, vip ulifanikiwa kufika mkoa unaitwa makamba, je kule kuko vip
 
Dig more deep pls.....! If you can
 
Nataka nijue Zaidi kuhusu hizo sabuni maarufu kama Savona zinakuwa kwenye vi box vidogo piece 24 kwa kila ka box, hivi huko zinauzwaje
 
Dig more deep pls.....! If you can
Raia wengi wanaamini sana utapeli, mm Burundi napajua vzr usalama upo biashara pia ipoooo Harmonize aliwahi kuingia mkataba na kampuni moja ya sigara "YES" inatokea Burundi

Hapa tunajaribu ku-share fursa sio kutapeli kwanza mm sio Mrundi useme labda naitetea nchi yangu hapana

Kule fursa ipo, nikipata mda nitakucha kuchimba madini ya kutosha mkuu kwa faida ya wapambanaji


Maana isije kuwa wengine wanabisha na bado wanasikilizia michongo itiki huku wakiwa wamelala
 
Kabisa mkuu, mm nimeuliza kitu ukitaja nchi tano kubwa kiuchumi duniani (tajiri) China huiachi harafu unakuta wachina wanafanya umachinga Kariakoo Tz nchi ambayo kwenye 100 ya nchi tajiri haimo, sisi na Burundi tofauti ipo lkn ni kidogo sana sisi ni wa 29 kutoka mwisho kiuchumi duniani
 
Sio wote ni wabaya but kunavisehemu sehemu kikinuka kimenuka kweli, vip ulifanikiwa kufika mkoa unaitwa makamba, je kule kuko vip
Nisiwe muongo huo mji wa makamba niliupita tu kwenye gari maana mie nilivukia boda ya tz na Burundi inaitwa manyovu, so ukivuka boda makamba ni miji ya mwanzo sn kwa muonekano ni pazuri sn kumekaa kama njombe hv ila kuna milima mingi sn na hali ya ubaridi flani hv kuna fursa sn za biashara coz niliona hekaheka sn pale, boy trust me buja usalama upo wa kutosha, ukitaka kuenjoy fursa za biashara fika hadi Burundi na Congo bukavu sio mbali sn na bunjumbura huko wacongo wanapenda sn hizi simu za iPhone. Ntarudi tena Congo japo now napanga kwenda mbali zaidi ya Africa
 
Me nipo manyovo mnanila mara nyingi napereka karanga sehemu moja inaitwa kayonzi, i kweli kuna baridi maana kuanzia miezi ya 5,mpaka 8 baridi huwa kali sana kiasi cha milima kufunikwa na hali kama ya mvuke/moshi mzito, kwa wazee wa biashara za mitumba hasa koti ,sweta na jaketi miezi hiyo ndo yakupiga pesa
 
Safari lini niunge tela
 
Ndugu zangu. Naomba msaada zaidi kuhusu Burundi. Nataka kwenda sasa kupeleka viatu, yebo, pochi na bidhaa kadhaa za urembo za akina dada. Kwa mujibu wa taarifa za mabadiliko ya fedha, Franc ya Bururundi ipo juu yetu X2. Na CRDB wapo Burundi. Nauliza hivi, Je nikiuza bidhaa zangu kwa Franc alafu nikaweka CRDB nikiwa kule si itadouble? Alafu nakuja kuitolea Bongo ikiwa na faida X2? Msaada please.
 
Kwa Rwanda pakoje, maana naona hio Burundi ni masikini sana,na jamaa walio ingia msituni nao sio poa hao, nadhani watakua na tabia kama waZulu,naskia Rwanda ipo juu kwa kilakitu, mtupe ABC za kwa Kageme kdg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…