Njoo tukumbushane visa na matukio kutoka kwa viranja ,mamonitor wa secondary na primary:

Njoo tukumbushane visa na matukio kutoka kwa viranja ,mamonitor wa secondary na primary:

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
4,824
Reaction score
5,587
Mi nakumbuka primary kuna kiranja alikuwaga ananionea sana kisa usmart wangu afu pia nilikuwa na materials na vifaaa vingi vya kuchezea maana mama yangu alikuwa anafanya kazi shirika moja la kugawa misaada kwa watoto kuna siku nilimwita sehemu nilimpiga mawe nilipoondoka shuleni sikurudi tena mama alinihamisha sijui nini kilijiri.

Secondary nakumbuka monitress alikuwa na tabia ya kuniandika kwa wapiga kelele bila sababu ila mwisho wa siku alikuja kunambia alitokea kunichukia sababu alinipenda sana sema Mimi sikuonesha nia tulifall in love kitu kilichonipelekea u gomvi mkubwa na aliyekuwa kiranja wa nidham nikawa mtu wa kusingiziwa na kuundiwa mazengwe kisa mtoto mzuri B.
 
Kuna headboy wetu primary alikua akiitwa mwakasasa jamaa alikua mkubwa na mtemi kinoma, cku moja kama saa sita hivi nikamfuata huku nimebadilisha majira kwenye saa yangu nikamwambia muda wa kutoka tayari, jamaa nae akakurupuka akaenda kugonga kengere ya kutoka watoto wote wakatawanyika, mwalimu kuja mbio aone aliyegonga kengere akamkuta mwakasasa jamaa alichezea fimbo ile mbaya, tokea cku hiyo jamaa akanijengea bifu!
 
Niliwahi kuwa Monitor Primary, nilikuwa naonewa sana kwa wababe likifika suala la kuandika majina ya wapiga kelele
Yaani usinikumbishe, halafu mie nikafika sec kibarua kikaanza upya... Nilikuwa nalia kila leo nikiwa primary!!!! Halafu yule mwalimu sitomsahau toka darasa la nne mpaka la saba ni mie tuu na adhabu ya viboko juu kisa nilichaguliwa nikalia!!!! Aki P..., Mungu anakuona ila Nshakusamehe!!!!!
 
Ha ha ha ha kama nakuona vile unavyonung'unika.

Pole sana Sakayo, yaani taabu ya kuwa Monitor haijawahi kumuacha Mtu salama.

Back
Top Bottom