sawima
JF-Expert Member
- Jul 9, 2019
- 5,496
- 8,491
Yap, coz kapatia, kila nikitaka kuchomoa nashindwa
Aisee pole sana! Vp unafanya juhudi yoyote kujichomoa huko?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yap, coz kapatia, kila nikitaka kuchomoa nashindwa
Napigana sana, hila naona nakutana na wasanii tuAisee pole sana! Vp unafanya juhudi yoyote kujichomoa huko?
Alphonce mawazo akikatwa mapanga huko Geita, mchana Mbingi zikishuhudia, kwa agizo toka kwa nanii, huku wakipongezana , hao hao wakampiga Lissu risasi, wakamvunja Mbowe mguu wakakimbilia kusemea kule kwenye kinga ya kisheria alikuwa kwa vimada wake, HAYA NDIO MAMBO YA KUTISHA TOKA NIZALIWEMungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Na kwa Bahati nzuri akaweka kizuizi kwa kupitia uwezo wake wa kiungu hili tusiweze kushuhudia viumbe hivyo ambavyo havionekani kwa macho yetu ya kibinadamu isipokua kwa utaalamu flani wa mambo ya kiroho.
Viumbe hivyo vikiwemo , Malaika, Majini , Wachawi pamoja na viumbe vingine vya kutisha sana, ikiwemo wanyama wa ajabu wenye ukubwa wenye kutetemesha na kuogofya kwa wanadamu wa kawaida.
Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”
Danieli 8:3 “Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.”
Danieli 8:5 “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”
Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”
Wengi tukisoma Habari kama hizi za kuona simba mwenye vichwa vinne na miguu kama ya binadamu, beberu mwenye pembe kumi, nyoka mwenye vichwa saba na wanyama wengine wa kutisha, tunajipa moyo na kusema hiyo ni lugha tu ya biblia/ lugha ya picha hakuna viumbe kama hivyo. Ila ukweli ni kuwa viumbe hivyo vipo na vinaishi kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huu wetu unaonekana. Na kuna binadamu wenzetu wameshashuhudia kabisa kwa macho yao.
Tuachane na hayo na turudi kwenye maada yetu ya leo . Tuzungumzie kuhusu mikasa ya kutisha ambayo tumewahi kukutana nayo kwenye ulimwengu huu ambayo kwa namna moja au nyingine vimekuacha midomo wazi na kukufanya uwe traumatized.
Ngoja nianze na mikasa / mambo ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani ambayo mpaka sasa hivi bado najiuliza kama ni viini macho au ni kweli , lakini ukweli unabaki kuwa ni kweli .
1. Jini kuchomoza baharini na kuelea hewani.
Nakumbuka ilikua ni usiku wa manane, nikiwa kwenye harakati za ushikirikina Uko sehem( sipendi kutaja jina). Nikiwa na mganga akiendelea kufanya mambo ya kishirikina baharini, Ambapo alisema anaita kiumbe( jini) hili anitimizie haja zangu . Kwa akili yangu nilijua tu ni danganya toto, hakuna lolote. Baada ya kama dakika 45 za yule mganga kufanya ushirikina wake. Ghafla akatokea mwanamke mrefu tofauti na urefu wetu wa kawaida wa binadamu alikua baharini anaelea tu, miguu haionekani kwa kweli nilikimbia, Bahati nzuri wale wasaidizi wa mganga wakanikamata kunizuia nisikimbie. Uzuri hakua anatisha wala nini, alikua tu ni mwanamke wa kawaida ingawa alikua na urefu usio na kawaida, na alikua kakasirika sana, alikua analalamika tunamuita sana tuna shida gani.....
2. Niliwahi kushuhudia kwa macho yangu , binadamu akiwa nusu mtu , nusu simba, Ana sura ya kutisha sana , mbaya mfano hakuna, ilibaki kidogo tu nizimie.
3. Binadamu mfupi kama stuli, Ana ndevu nyingi mpaka chini na alikua na mguu mmoja tu , na macho yake yanawaka moto.
4. Mzimu wa mtu maarufu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita.
Hii ndo mikasa ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani, ambayo kiukweli mpaka leo inanipa shida sana, na ilichukua miaka kadhaa mpaka kuweza kukubali hii hali mpaka kufikia kuzoea kidogo. Ila hapa duniani kuna viumbe vya ajabu mno, na kama ukitaka kuviona unaweza.
View attachment 1430585
Sent from my iPhone using JamiiForums
Unaweza kuta kuna mkulima alikuona huo muda nae akahadithia ameona jini mwanafunzi usiku wa manane.Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari,
Dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori fulani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule,
aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Napigana sana, hila naona nakutana na wasanii tu
Nakumbuka kuna mwaka tulienda kufanya sampling mkoa fulani, kutoka mjini hadi huko kiijijini ni mbali mno na barabara zenyewe ziko hovyo.
Baada ya sampling tukaanza safari ya kurudi mjini, njiani kuna mzee mmoja akatuomba lift tukamwambia mzee gari imejaa akasema sawa,
Basi baada ya kama km 2 gari likaharibika tukachokonoa chokonoa yule mzee akatukuta na akatupita, gari lika faa tuakanza safari, tukampita yule mzee tena ila baadaye likaharibika tena, yule mzee akatupita tena.
Basi mchezo ukawa ule ule mwisho tukaona itakuwa huyu mzee ndo anatuchezea, tukaona ngoja tumpe lift tu, alivyotukuta tena tunachokonoa chokoa tukamwambia mzee, subiri turekebishe tukupe lift mzee akakubari.
Gari lilivyo faa halikuhabirika tena hadi tunafika mjini.
Kuna binadamu wamepewa uwezo wa kung'amua vitu na kuna wengine katika ulimwengu wa kiroho ni vipofu wasioona kitu chochote. Macho yao yamefungwa. Sikumbuki vizuri ila katika biblia kuna mtume mmoja walizingirwa na maadui lakini hakuonesha wasi wasi wowote. msaidizi wake akamwambia sasa tunauwawa. Yeye akajibu ondoa wasiwasi tunaulinzi yule akashangaa ulinzi u wapi. Ndipo yule mtume akamfungua macho yule mtumishi akaona jeshi kubwa la malaika limewazunguka. Ndipo wasiwasi ukaondoka. wanaojua Biblia watasema ni nani. Nilitaka tu kukwambia haya mambo ni ktk roho. uwezi yaona mpaka uwe katika ulimwengu wa rohoni. Majini, Malaika uwezi waona kwa macho ya nyama. Kuna watu wanazaliwa wananguvu maalum za kiroho. Haya mambo yapo!
Du masoja wenzako haoHilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.
Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.
Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!
[emoji23][emoji23][emoji23] NachiHilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.
Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.
Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!
alikua anaumwa nini pengine yupo mzima kachukuliowa tu msukule kwa scenario ulioiandikaDogo hayupo tena duniani..ila naamini aliko saivi yupo huru kabisa..
kanuni ya kichawi haipo kwamba atakuja KUwanga 9 usiku anaweza kukuwahi saa 7 kbl ya 9 kuamka.Amka saa 9 usiku na usali/uswali kwa Imani moyoni kumuomba Mungu wako akuondolee hayo matatizo kwa Iman kubwa moyoni, fululiza Daily naimani utapata Relief.
Acheni watoto wazuri waoga waje kwangu kwa mana uwoga hawatauhisi kamwe wakiwa kwanguHuu Uzi unanitiishaa[emoji87]
kanuni ya kichawi haipo kwamba atakuja KUwanga 9 usiku anaweza kukuwahi saa 7 kbl ya 9 kuamka.
Imani yako maombi ni muda gani?Kwani nimesema aamke saa 9 kwajili ya kudeal na mchawi au aamke kwa kusali na kuomba Dua? Kila mtu na Imani yake, mie nimetoa ushauri huo coz naamini nguvu ya kuomba Dua usiku. Kwahio km ww huamini pita hivi 👉
Kuna zile bar unakuta zinajaza watu zina wahudumu warembo kweli wengine huwa ni majini hasa zile bar ambazo wamiliki wake wanamikataba ya kishetani kwa ajili ya mali
Hatari sana ile sehemu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23] Nachi
Hapana hakuna soja wafupi kiasi kile[emoji23][emoji23][emoji23]Du masoja wenzako hao
DuhNakumbuka kuna mwaka tulienda kufanya sampling mkoa fulani, kutoka mjini hadi huko kiijijini ni mbali mno na barabara zenyewe ziko hovyo.
Baada ya sampling tukaanza safari ya kurudi mjini, njiani kuna mzee mmoja akatuomba lift tukamwambia mzee gari imejaa akasema sawa,
Basi baada ya kama km 2 gari likaharibika tukachokonoa chokonoa yule mzee akatukuta na akatupita, gari lika faa tuakanza safari, tukampita yule mzee tena ila baadaye likaharibika tena, yule mzee akatupita tena.
Basi mchezo ukawa ule ule mwisho tukaona itakuwa huyu mzee ndo anatuchezea, tukaona ngoja tumpe lift tu, alivyotukuta tena tunachokonoa chokoa tukamwambia mzee, subiri turekebishe tukupe lift mzee akakubari.
Gari lilivyo faa halikuhabirika tena hadi tunafika mjini.