nebuchadnezzer
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 246
- 343
Pole sana, ni heri umeandika hapa ili ufahamu ukweli, hao watu ni matapeli tu, wanaotumia kivuli cha Mungu ili wawaangamize wengine..Jambo kama lako lilishanitokea na mimi zamani kidogo, lakini kabla ya hapo nilishawahi kuwasikia kwenye radio, lakini sikutilia maanani mpaka nilipokutana nao..wakuu mie binafsi sijawahi kukutana na kisa kikubwa chakutisha kivile sema kunakimoja ambacho kilitokea ambacho kinanipa maswali mpaka iitwayo leo
ilikuwa ni kipindi flani wazee wangu wanapata huduma ya kiroho ka waumini wengine katika kanisa flani basi wakawa wanapata shuhuda mbalimbali toka kwa wenzao basi nao wakataka nao wapate baraka hizo za Mungu maana hakuna asiyezitaka ukizingatia nao walikuwa na shida zao. Basi wakaendelea kufanya taratibu zao ka kawaida ili wawezepata kibali chao cha kumshuhudia Mungu wao namie nikiwa ka mtu wa kando ka hayo mambo hayaniusu. Wakaendelea kupata maombi na kuhudhuria ibada basi siku moja kiongozi wao wa kiroho akawaahidi kufika nyumbani kwaajili ya kufanya maombi na kuombea nyumba na familia kwa ujumla
Day one alifika mida ya usiku ka mida ya saa mbili, ikiwa mama ndo alikuwepo akanialika namie kuweza kupata baraka na mengine ya kiroho, mchungaji akafanya maombo kiasi pamoja na wasaidizi wake baada ya muda akasema nitakuja sikunyingine kwaajili ya maombi tena. basi akaondoka. na mzazi akaondoka siku iliyofuatia mie ndo nikaachwa kwaajili ya kumpokea kiongozi huyo wa kiroho siku atakayokuja.
Siku iliyofuatia baada ya siku kadhaa ilikuwa ngumu kumpata kiongozi huyo wa kirohoo maana alikuwa anahudumia watu wengi na alikuwa busy na majukumu mengine ya Kanisa, nikafanya jitihada za kuwasiliana nae mara kwa mara basi akaniahidi one day atafika.
Hiyosiku aloyofika akafika salama maana alikuwa anatokea mbali kiasi na alifika mida ya usiku maana alitoka kutoa huduma sehemu nyingine basi akafanya maombi nikiwa nae na baadhi ya watu wengine baada ya hapo akaanza kumwaga maji ya baraka nyumba nzima na vyote vilivyokuwepo nyumbani hasa magari na nyumba zote na vyumba vyote, baada ya hapo akarudi tena akafanya maombi kiasi then akaniambia twende nje.
Tukazunguka kwenye eneo la nje akaanza kutafuta tafuta akaniambia ka naona kitu, nikamjibu sioni akatafuta tena na tena kwakutumia mwanga wa simu basi akaanza kusema 'lilikuwa linataka kukimbia tena na leo' basi akakiona kumbe ilikuwa kibuyu na kichupa vimefungwa pamoja na vinashanga na kitu ka irizi nyeusi na nyekundu, nilistaajabu sana. akanijuza kuwa ilikuwa inataka kukimbia na ndo maana siku ya kwanza alishindwa kuikamata. na hizo zana za kishirikina zilikuwepo sehemu nyeupe ambayo ni rahisi kuviona ila akaniambia vilikuwa ndani ya banda lililokuwepo karibu ila kwakuwa alimwaga maji yaliyobarikiwa kikashindwa kukimbia kikaishia hapo nje na akanijuza kwa macho ya kawaida huwezi ona
Mpaka leo najiuliza sana hivi ule ushirikina ulitoka wapi na uliwekwa pale nyumbani toka lini na unawezaje kukimbia pindi nguvu ya Mungu ijitokezapoooo? Mpaka leo lile tukio huwa nalikumbuka sana na vile kibuyu kilivyousisimua moyo wangu.
Mazingira yao ni hayo hayo, watakuja day one, wataondoka, kisha watarudi, mara ya pili au hata ya tatu, lakini safari hii wakiwa na vihirizi vyao walivyojiundia wenyewe, na ni lazima waje usiku..sasa wanachofanya ni kuvirusha, aidha nje,au ndani wakati wanapoingia au wanapojifanya wanafanya maombi wakati wewe umefumba macho, lakini kwa siri..Wakishamaliza, wanajifanya wameingia katika rohoni, kisha baadaye wanakwambia nimeona kitu, wanakuambia tuondoke twende..wanaelekea maeneo yale yale yaliyotupa hizo takataka zao, kisha wanajifanya wanatafuta tafuta..
Baadaye wanaona, ndio hapo wanakwambia walikuwa wanataka kukimbia wakaacha hirizi zao..sasa kama wewe ni yule wa kuombewa ombewa tu, bila kujitathimini Imani yako na Mungu wako ipo wapi, watakuzomba na maji haraka sana...
Mimi nilikuwa na watu wengine nao walikuwa wameshaogopa, kumbuka saa hiyo ni usiku wa saa 4 au 5 hivi..Lakini nilivyoona vile nikamweka chini siku subiri muda, nikamuhubiria, nikamwambia hapa umekutana na nuru, na ukijaribu kupambana na Nuru utakuwa kipofu..akaogopa, nikataka kumfukuza, watu wakasema tumwache tu asubiri asubuhi aondoke, ilipofika asubuhi aliondoka kwa aibu ya ajabu, mpaka leo hii sijui yule mtu alipotelea wapi, sijamwona tena..
Hivyo kwa ufupi jua hakuna uchawi wowote hapo,..Usiogope, ila na wewe pia, au mwingine yeyote anayesoma uzi huu, simama katika Imani yako. Mwamini Mungu. Soma Neno..Kwasababu hizi ni nyakati za mwisho. Manabii wengi wa uongo wapo duniani, na watawadanganya wengi..