Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Mimi binafsi nakumbu miaka ya nyuma sana katika kijiji chetu walikuja waganga ambao wanaitwa lambalamba bs bwana hao kz yao kutoa uchawi kwa kila nyumba na kila mtaa sasa nilichokishuudia kwa macho yangu, palikuwa na kijana akawa anawazalau wale waganga Ebwana wakamgeuza mwanamke palepale,sasa ikawa mshikemshike kumpepua ndugu wakja yomi pale wanawaomba wamueke sawa waganga wakawa wanataka 300000 taslim ndugu awana wao wana 200000,Ndio kuwasaidia.

Jamani uchawi upo,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh kama The Conjuring mzee hawa wachawi hawafai kabisa.
 
Nilikua nipo kwenye mood ya kumasturbate yaani nilikua natafuta uzi wa mwisho kabla sijaingia xvideos sasa nimefika hapa na xvideos siendi leteni visa niburudike.
😂😂😂😂Manina
 
Nabii Eliya na mwanafunzi wake Elisha
 
Tatizo huwa walioshuhudia hawatoi background,warumi atleast anaeleza yeye alikuwa anafanya ushirikina...
Kingine hawajaribu kuhusianisha mantiki kama alikuwa katika hali gani kiafya, au shughuli za kawaida alizofanya siku hiyo...
Ni ngumu kujua bayana lakini atleast unatafuta majibu kisayansi...
Sikumbuki mwaka ila ilikuwa Arusha nikaenda guest baada ya safari ya masaa kama 10, nikalala nikajiskia kama nakabwa, mimi sio mtu wa dini ila katika fujo za life niliwahi kuokoka nikiwa kijana mdogo wa miaka kumi na kitu later nika quit.Hivyo nikawa nakeme kwa jina la Yesu...
Baada ya muda nikarudi tena Arusha, nikawaza guest cheap zimejaa ngoja niende pale pale😂,hamad!!nikapewa chumba changu kile kile na ninakumbuka kisanga kile nikalala,hali ikajirudia ya kukabwa😆,this time sikumbuka Yesu nikawa nakomaa huku najaribu kuchapa ngumi...nikaamka.

Natoka nje naskia wahudumu wanamalizia stori "...wengine wanakuwa na waganga wao..." sikutilia maanani.Conclusion yangu ikawa nilichoka sana na safari,hakukuwa na oxygen ya kutosha, na kwa mara pili nilichoka na safari+hofu ya ile mara ya kwanza na oxygen haikutosha.

****Mara: nyumba ina ng'ombe mmoja wa kisasa lakini saa saba usiku nikaskia vishindo mithili ya farasi wanakimbia nje ya chumba namuuliza dogo umeskia,kasema ndio nikatoka nje hakuna kitu...hii nimebaki puzzled.
Dodoma:Najiona nashindwa kupumua tena hata mchana lakini nakuwa kama nimefungua macho na naona somehow clear wanachofanya wenzangu labda wanatumia simu,wanachat n.k lakini nikiamka na kuwauliza wanasema nilikuwa nimelala.Hapa nilikuwa na stress sana time hizo.

conclusion yangu
Dar es Salaam: Hapa kidogo nishakuwa mdadisi kidogo nagonga meditation kwa kujifunza funza bado najifunza sometimes nakwama hasa kuwa vegetarian.Ikaja kitu kama naskia nakabwa mara kabla sijafikiwa nikatamka "mantra" moja ya ki meditation pale pale ikapotea😃.
So Falsafa yangu ni kuwa ukijenga hofu na ku pay attention huo ulimwengu unakukaribisha.TUSIOGOPE, likitoke jini sijui mchawi SIMAMA na jipe courage...cuz hofu haipukiki,lakini kujipa ujasiri kunaweza kukuvusha
 
Nakumbuka Miaka ya tisini mwishoni mkoani Dodoma, kuna kituko kiliwahi tokea na mimi nilikua shuhuda kulikua na mzee mmoja alimuacha mkewe akaamua kuishi na mke mwingine, yule mke aliyechwa hakufurahi ile hali akaamua kwenda kwa sangoma aisee!

Ile nyumba ilikua haikaliki maana mmewe na huyo mke mpya kila siku walikua wanachezea viboko, pia mawe yalikua yanarushwa juu ya bati mfululizio na hayakujulikana yanatoka wapi, ila yakidondoka chini yanageuka kuwa kinyesi cha binadamu, vyombo kabatini vilikua vinatikisika mwanzo mwisho na aliyekua akivitingisha hajulikani.

Baada ya mauzauza kuwa mengi waliita mashekhe wapige duwa ila wapi haikusaidia, ikabidi waikimbie ile nyumba, ile nyumba ilikaa kama miaka zaidi ya 12 bila mtu kuishi, hadi yule mzee mwenye nyumba alipofariki mwaka 2014 ikabidi watoto wake waiuze, mtu aliyeinunua aliibomoa yote (kwavile ilikua imechakaa) akajenga nyumba mpya, kuna nduguyng yeye bado yupo Dom aliniambia tangu imeuzwa hakuna mauzauza yaliyotoke.
 
Wachawi waliniiba wakanitoa chumbani wanipeleka kunilaza chini ya mtungi..kwenye kona la nyumba. Walinipata asubuhi nikiwa nimesinzia nimefunikwa ushungi kama mtoto mchanga.
Hakuna kitu hapo.
Ushamuona mtu ana amka na kutembea nje kisha anarudi na kulala lakini kesho akiambiwa alichofanya anakataa katakata?
Kuna mtu tulikuwa nae boarding school cell mate kwenye bweni alikuwa ana amka anafanya vitu kesho analalamika wenzie katika cell hiyo wamemtendea hivyo. Yeye hata akilala mapema saa 1 usiku ikifika saa nne usiku anaweza kuanza hiyo shida yake.

Tunaita sleep walking, unaweza kwenda kulima usiku ukiamka asubuhi una majeraha ya kujiumiza unasema wachawi, au unaenda kulala chini ya mtungi ukiamka ukajikuta hapo unasema ulipelekwa na mtu (wachawi/jini).
 
Mkuu mwli ulipataje nguvu za kukimbia hvo
 
Ilikuwa mwaka 2004 Mzee wetu alihamishiwa kikazi mkoa fulani kanda ya ziwa, ikabidi familia yote tuhamie huko..
Kutokana na uchache wa nyumba za serikali akapangisha nyumba mtaani.

Mzee akapata safari ya kikazi kwa muda, Maza nae akawa chuo mkoa mwingine.. Nikabakia mimi na brother.
Mambo yakaanza, siku ya kwanza tukasikia madirisha ya nyumba yanafunguliwa na upepo mkali unaingia ndani ilikuwa saa nne usiku, tukatoka na mapanga kutafuta mwizi hakuonekana.

Siku ya pili mlango ukafunguliwa na kiumbe kilichoingia kikawa kinafanya shughuli zote tunazofanya mchana mf. Kuwasha radio na kubadili station, kufagia, kufungua fridge nk.

Tulihangaika ikawa kila siku mziki unanza saa mbili usiku, tukawa hatulali.. Akaja mshikaji wake broo akamwambia tukae nje usiku kwenye pembe ya nyumba tutawaona wanaotusumbua.

Tukajipanga tukaenda kukaa, baada kama ya dakika arobani alipita mtu wa kwanza anakimbia kinyume nyume mwendo wake sijapata kuona, baada ya muda akarudi akiwa na mwenzake wakiwa na mwendo wa kawaida tukawatambua kumbe ni baba mwenye nyumba na jirani yetu.

Jambo la kutisha waliamua kutuadhibu baada ya kutugundua tumewaona.. Hivyo tulipigwa ganzi karibia masaa matatu hamna kusogea wala kuongea hata kujikuna. Wao wakaendelea na mambo yao.
 
Nilikua ninamika 5 kipindi hiko..
Na unachosema nakifahamu. Haikua hicho
 
Nilikua ninamika 5 kipindi hiko..
Na unachosema nakifahamu. Haikua hicho
Sleep walking haijalishi umri wa mtu.
Huko Marekani kuna mtu aliuwa mkewe wakati anaota usingizini kavamiwa, jamaa alishinda kesi ya mauwaji sababu ya tatizo lake la kudumu la sleep walking.
Jamaa alikuwa mara nyingi anaamka na kwenda kuzunguka mtaani anarudi ndani anapika breakfast anarudi kulala na asubuhi hakumbuki.

Amewahi kuumia mara nyingi wakati anatembea bila viatu huku akiwa amelala, muda wote huo anaota.

Huyo room mate tukiwa shule ya sekondari alikuwa na umri zaidi ya miaka 14.
Anaruka kitandani na kupiga kelele au kutoka nje anatembea na kurudi kula, usipomstua kesho anakataa kabisa.
Jamaa waliokuwa madarasa ya juu yake mle chumbani kwetu walikuwa wanampiga makofi tunamcheka, yeye analalamika wameenda kumtoa kitandani na kumpigia pembeni ya kitanda kumbe kaamka mwenyewe huku tunamuona, maana wakati mwingine ni mapema saa 4 au saa 5 usiku wengine bado tunapiga soga (stori).
 
Sawa kiongozi
 
Sawa kiongozi
Najua umekubali kuepusha ubishi lakini rohoni bado una amini ilikuwa nguvu za giza au mazingara ya kichawi au majini.

Siyo lazima niwe sahihi nadharia yangu, lakini nilikuwa najaribu kuelezea uwezekano wa hilo kutokea kisayansi ya baiolojia, maana sleep walking ni tatizo la kibaiolojia kwamba kuna sehemu ya ubongo wako iliyotakiwa kulala/kupumzika ilikuwa bado inaendelea kufanya kazi.
Ilitakiwa sehemu ya ubongo inayo husika kuwezesha viungo vyako kama limbs zisifanye kazi nayo ilale kama sehemu zingine za ubongo, ibakie sehemu ya ubongo ile ya kufanya kazi za msingi za upumuaji na kusukuma damu.

CC: Carleen njoo unikosoe baiolojia huku, mimi sikusoma kabisa Biology elimu ya upili au kokote zaidi ya shule ya msingi St. Kayumba.
 
Kwel hamkutumia dawa hata tone ili kuwaona??

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Kwel hamkutumia dawa hata tone ili kuwaona??

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
Hapana na wewe ukipata muda wa kuchezea kama sisi jaribu tu, utashangaa sana ya dunia. Ila uwe na moyo kwasababu haujui wataamua kukuadhibu vipi wakigundua umewaona
 
Hapana na wewe ukipata muda wa kuchezea kama sisi jaribu tu, utashangaa sana ya dunia. Ila uwe na moyo kwasababu haujui wataamua kukuadhibu vipi wakigundua umewaona
Unakaa kwenye kona kwa nje au kwa ndani, na nikiwaona halafu nikasepa inakuwaje kabla hawajarudi?
 
Nabii Elisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…