Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

duhh!! noma sana,, lile ziwa la kilozi ilikuwa lipite na ww mzebaba, pole sana, yan wachawi na wezi hawakutakiwa kbs kuwepo duniani hapa. [/QUOTE]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo shule ya msingi sio Mwenge huko Tabora
 
mimi pia sijui ni miongoni mwa hao watu ambao macho yamefungwa, sijui ndio nini mm huwaga ni mgumu sana kulala usingizi ila nikilala huwa nimelala, jambo lolote la hatari watu wengine wanaweza kulisikia mi nisisikie, kuna mwaka nikiwa young kama darasa la 5 hivi Bundi aliliaga mti ambao uko pembeni kabisa na dirisha langu sikusikia hata robo wakati huo karibu mtaa mzima wanamsikia.

haya mambo ya sijui kumwagwa mchanga juu ya bati, watu kutembea wataskia wote mimi nalala sisikii hata tone.

Labda ujanja wa ndoto, nikiota kitu au kusema (foresee) inakua hivyo hivyo imepelekea watu wangu wa karibu hawatakagi nitie neno kwenye jambo lolote wanalotaka kufanya maana neno langu haliangukii chini
 
Mimi nitasimulia kisa kimoja tu, tena cha utotoni maana kiliniogopesha sana kwa umri ule wa miaka isiyofika hata kumi. Hiki ni kisa kati ya visa vingi vya nguvu za giza nilivyovishuhudia, na ninavyoendelea kuvishuhudia mpaka kesho. Mnivumilie na mnisamehe mdogo wenu maana nitaandika kurasa ndefu.

Picha linaanza pale marehemu mama(PKA mama yangu mzazi, na Mungu akurehemu kwa rehema zake) alipoolewa na baba yangu. Kwa miaka zaidi ya mitatu, mama hakuweza kukaa na ujauzito zaidi ya miezi mitatu, na badala yake mimba ziliharibika.
Mama aliisha kwa masimango, na kuonekana sawasawa na papai linalobeba corona badala ya vitamin! (Ni mchezo uliokuwa ukichezwa na majirani zetu, wenyej wa Kigoma, na Ukweleni hapo)....Lakini mama hakuchoka kuvumilia, na kumwomba Mungu.

Hatimaye mama akashika ujauzito wangu, haukutoka tena, na nikazaliwa pale MNH, na nikaitwa jina la "dawa ya Mungu", maisha yakaendelea kijijini kwetu Boko.

Katika makuzi yangu, utotoni wazazi wangu walikumbana na matukio na changamoto nyingi za kukatisha tamaa. Kuna wakati usiku mama alimka na akakuta sipo kitandani, ananitafuta kwa mda mrefu wakiwa na mzee, hatimaye wananikuta chini ya uvungu wa kitanda nalia, au wananikuta kwenye pembe ya nyumba, mama alikuwa akilia weee, hatimaye maisha yanaendelea. Ilifika mda nikiwa na umri wa mwaka na nusu, nililishwa nyama ya kisigino ya maiti, niliumwa sana kutikana na hili chupuchupu nilambe udongo, wazazi walipambana, Mungu akasaidia, nikatoka salama.

Balaa kwa macho yangu, lilikuwa hapa sasa. Nikiwa darasa la pili, miaka hiyo ya tisini nilitokewa na tukio la kwanza, mubashara ambalo lilinitisha sana maana hapa niliona kwa macho na akili zangu. Usiku nikiwa nimelala ghafla nywele nikahisi zinasisimuka, damu inaenda mbio, na mwili unachemka....ghafla nikashtuka na kuamka paaap! Uso kwa uso na mwanaume aliyeshika kitanda changu, miguuni mwangu nywele zake zinawaka moto mkubwa ila haziteketei, macho yake yanawaka moto kama mkaa wa moto, na mikucha mirefu.

Kulia kwangu, wanawake wanne wakiwa uchi kabisa, wamebeba vyungu kichwani vinawaka moto. Kushoto kwangu wanaume watatu wapo uchi nao wamebeba vyungu, nao vinawaka moto, na mtu mmoja wa kiume(jini) mrefu akikaribia kugusa paa, mweupe kwa rangi(mwarabu) amevaa miwani mweupe, kanzu ndefu, nyeupe mpaka chini, na alikuwa na ndefu ndefu kiasi.

Tukakaziana macho sana, nikawa nawageukia wote mithili nataka niamke niwarukie ila nahisi nazuiwa, nataka kupiga kelele sauti haitoki. Baada ya dakika kama 3 au 4, nikaanza kuuona ukuta kwenye pembe ya nyumba, mubashara unafunguka na wanaanza wanawake kutoka nje kinyumenyume, wakifuata wanaume, na yule jini anakuwa wa mwisho. Hatimaye ukuta unajifunga tena baap! Na hatimaye ndo sauti inatoka mamaaaaaaa........!!!

Mama na baba wanakuja, wananikuta nalia na nimeloa jasho mwili mzima. Hatimaye nawasimulia, mama analia sana, ananikumbatia, na anamlilia Mungu, ananichukua ananipeleka chumbani kwake kwenda kulala nao chumbani kwao. Mama akaniambia watoto ni malaika, huona majini na wachawi ila ukikua hutowaona. Ila haikuwa hivyo mimi mpaka kesho hawa washenzi hawakatishi anga zangu.

Asubuhi ikafika, nikajiandaa kwenda zangu shule, na mama akaniambia kwa sasa hali ilipofikia itabidi niwe nalala na mbwa chumbani kwangu, yaani mbwa anafungwa kwenye mguu wa kitanda changu. Hii ilinisaidia ila hawa washenzi walimuua mbwa wetu(PKA Jeck) ni mbwa aliyepambana sana na hawa washenzi, ila usiku mmoja alipiga kelele kushtuka damu zinamtoka puani na mdomoni ndo ukawa mwisho wake Jeck wangu.

Hili ni tukio mojawapo kati ya matukio mengi niliyokumbana, na ninayokumbana nayo. Ila kama ukilala unaamka tu flesh bila kuona haya mavitu, muombe Mungu akujalie hivyo hivyo. Haya mavitu yanatisha sana.
Asanteni, na poleni kwa kuwachosha!

Nakumbuka siku moja usiku niko na mama jikoni(majiko ya nje) nikawa nasinzia mama akanambia niende ndani nilale ataniamsha msosi ukiiva. Kulikuwa na mvua inanyesha.
Ile nipo njiani naelekea ndani nilikutana na mwanga mkali wa kutisha ukanirusha nikaanguka chini nikawa nimezubaa sielewi nini kinaendelea ndo baadae kama sekunde kadhaa nikasikia muungurumo wa kutisha tena ndo nikagundua ni radi mama akaja kunichukuwa pale siku hiyo hata sikula na nililala kwa kuweweseka kila nikifumba macho nakiona kile kitu cha ajabu. Hakielezeki kwakweli.
Kesho yake tunaamka tukakuta mfenesi unaanza kunyauka kumbe ile radi iliupiga ule mfenesi.

Siku nyingine niko nyuma ya nyumba kwenye saa 1:30 usiku napaki gari(nilikuwa natengeneza gari za magome ya mgomba) so nilikuwa nimetengeneza kaeneo nyuma ya nyumba kakuzitunzia gari zangu nikimaliza kuzichezea
Nikiwa naendelea kuzipanga kulitokea kitu kama mshale/mkuki unamwanga kwa mbele mithili ya wekundu wa chuma kilichochemshwa kwa moto mkali. Hiki kitu kikapita juu kidogo ya nyumba kikaenda kuishilia migombani mpaka upeo wa macho ulipoishia. Cha ajabu ni kwamba kilipita karibu sana kiasi kwamba mtu ungeweza kuruka ungekikamata so haikuwa kimondo ila pia pamoja na kupita migombani ambapo hua imeota zigzag hakikugonga mgomba hadi kinaishilia

Siku nyingine tumetoka kuchunga mbuzi nafungua mlango wa nyumba ya mbuzi mwenzangu kanishikia kibatari kwa ajili ya kunimulikia wakati wa kuwafunga kwenye mambo zao zilizopigiliwa chini mule ndani mwenzangu akaona vitu viwili vinang'aa darini kwenye kona akanionyesha anauliza vilikuwa vitu gani si ndo kumulika vizuri tunakutanisha uso kwa macho na bundi mweusii. Aisee asikwambie mtu huyu ndege ana sura ya kutisha, nilijikuta mkojo unapita huku napiga kelele wakaja wakubwa wakamfukuza. Kwa kweli ile sura ilikuwa inaniijia kichwani karibu wiki nzima nikiwa sehem yenye giza
 
Mi sijawahi shuhudia mauzauza yoyote ila hadi leo nashangaa kuna siku nimeota mama flani hapa mtaani (namjua) alikuwa ananilazimisha kula nyanya,nyanya zilikuwa nyingi sana ananisokomezea mdomoni mimi nameza tu....ajabu nilipokuja kushtuka nikajikuta nimeshiba halafu tumbo limejaa kishenzi yaani
 
Shukuru Mungu kama hujawahi kutana na hayo mambo,
Mambo hayo husababishwa na Kama kuna Ndugu wana michezo hiyo, Majirani au watu wanaokuzunguka maeneo unayoishi na husababishwa na Husda,michezo,mazoea
Hayo Mambo bwana mkubwa yapo sana sana tu, kama hayajakukuta utayadharau na kupuuza, Kuna muda unakutana na majaribu mpaka unajiuliza hivi kweli mm huwa nasali, kama nasali mbona bado siko imara huyu Mungu ninae miomba ni wa wapi,mbona wengine hawakumbani na hizi zahama..

Mfn: Sumbawanga unaweza sikia vitimbi vingi sana ila wewe ukapangiwa kazi huko ukaishi vzr na ukakataa kuhama kabisa, ila mwinhine anaweza pangiwa huko mwezi mmoja tu akakutana na vitimbi vya hatari haya mambo yanaendana na Ukoo sometimes
 
Mwamba pole sana kwa uliyoyapitia. Si vibaya uka share nasi hayo unayoendelea kuyapitia hata kwa ufupi kama ulivyofupisha hichi ulichotupatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo Ishu Ilimpata Mzee wangu. Alikuta Yupo Umbali wa Kama 20KM hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…