Ebhana eeh!! Haya mambo nayasikiaga tu kwa watu.Kwamba wamekutana na hili jambo.Nasikilizaga stori zao then nasikitika nao kidogo kisha najikataa(nasepa).
Kuna hizi stori za mtu kuwa unaongea na mwingine(hasa wa jinsia tofauti) halafu kuja kushtuka kapotea.Au wengine wanasema unashangaa kabadilika kawa wa jinsia yako(Haijanitokea hii).Kwangu siku zote ilikuwa ni theoretical, Sasa Leo nimekutana na practical.
Nilikuwa njiani bhana barabara fulani hivi nzur kalikali.Si nikakutana na mdada ninayemjua.Ninaposema namjua ni namjua kweli.Nilisoma nae,tuko mtaa mmoja.Nikitoka nje ya huu mkoa na kurudi,mara nyingi baada ya kuonana na familia na ndugu basi ninayefuata kumuona ni yeye.So ninamjua sana tu.
Basi stori zikaanza,kama dakika moja hivi.Sasa kwa kuwa mimi ninatembea chap kuliko yeye na yeye pia alidai amechoka,nikajikuta namtangulia kidogo mbele kihatua.Tukaendelea kuongea huku simuoni(alikuwa nyuma yangu).Sasa cha ajabu nageuka sioni mtu.Sikuamini bhana na wala sikutaka presha inipande sababu wengine humu walisema walitoka spidi.Nikatulia nikaangaza,sioni mtu.Baadaye nikawaona masela fulani hivi wanatokea.Hadi wale jamaa wananifikia bado sikuona mtu.
Sasa kinachonishangaza zaidi ni hiki:
1.Barabara ni ndefu haina kona kali kiasi kwamba waweza muona mtu toka mbali.
2.Barabara haina chocho zinazoikatiza kiasi kwamba mtu hawezi deviate akapita njia nyingine sababu njia ni hiyo moja tu.
3.Time interval; Nilivyoacha kuongea naye haikupita muda nikageuka.Time interval kati ya kuacha kuongea naye na kugeuka kuangalia uwepo wake ni approximate dakika 10.Huwezi nitoroka huo muda nisikuone na urefu wa barabara ile labda;
1.Uwe Super Hero
2.Uwe na Super natural powers.
Nilivyofika home nikaamua kwenda kicenter fulani hivi maybe ningekutana naye,holaa.Na ni nadra sana kumkosa maeneo hayo mida ya jioni.Kesho namfungia kazi.