Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Hiyo ni michezo ya SGT's na WO's wasiotaka kuhamishwa au wenye masrahi na hizo KJ's. We angalia utakuta mtu ana miaka kibao bila uhamisho mpaka anakaribia kustaafu.
Kuna SGT mmoja alitemeshwa mwenge nikiwa pale ndio mgeni. Huyu mtata akikuwa anageuka fisi na kusomba mifugo ya wenzake, kuku, bata, mbuzi, kondoo abapita nao. Ila huyu alitemeshwa mwenge ingawa ni kwa ishu nyingine ya kipuuzi sana.

Kuna mwengine naye ni SGT huyu alikuwa anawaingili watu kimiujuza na wengine mpaka kuwa na uwehu hususani waliokinzana naye saba. Huyu ni noma ila naye ameshavua buti mwaka juzi hapo kwa taarifa niliyopewa. Hii hali nimepata kusimuliwa na kuikuta camp mbili tofauti.

WO's wengi niliokutana nao walikuwa na vimbwanga ila vya kawaida, wengi kwa ajili ya ulinzi wao. Ila hawa ma SGT's acha kabisa.
 
Niliwai kuishi wilaya ya bahi Dodoma...kuna siku moja Niko nje ya nyumba majira ya mchana wa saa 7 hivi,alitokea mtu gafla akaniomba nimletee maji ya kunywa ,nilipoingia ndani nakutoka nikakuta yupo kifua wazi wakati alikuwa kavaa shati....na Hana chochote alichobeba.....nikampatia maji akanywa kisha akaniambia kuwa anaenda safari ya mbali na katokea Dodoma mjini kwa mguu....kisha akaondoa ....alipiga hatua Kama 4 baada ya hapo sikuona mtu upande wowote ule ........2005 ilikuwa .....
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]aisee uliogopa mkuu?
 
hili tukio sijui niite ndoto au uhalisia.
nikiwa na miaka 14 mikoani mbeya wilaya ya kyela, kuna siku nimelala usiku nikaota nipo sehemu na mtoto wa jirani yangu na baba yake ambao wanakijiji walikuwa wanawatuhumu kwamba ni wachawi, sina uhakika kuhusu hilo.
basi huko tulipokuwa tulikuwa tunafanya mambo mengi ni kama sherehe hivi, baadae baba wa yule kijana akasema mda umeisha inatubidi turudi nyumbani. Tukaanza kupaa wakati tunakaribia kufika nyumbani ghafla nikawa kama nimeshtuka kutoka usingizini kabla sijaingia ndani, lakini chakushangaza nikiwa bado sijielewi vizuri nikaona ukuta unafunguka na nikaingia kwa kasi ya kama spidi 500 mpaka kitandani. Nilivyofika kitandani akili ndio ikaa sawa, sasa nikawa najiuliza hii ni ndoto au uhalisia sijawahi pata jibu mpaka leo.
Ndoto hiyo.
 
Binafsi sikuwahi kushuhudia mambo ya kutisha,hata Kama yalikuwepo madogomadogo yalikuwa ya kawaida tu..Ila baada ya kuoa na kubarikiwa na mwanangu wa kiume mambo yalianza kubadilika.

Ni hivi,

Mwanangu wakati akiwa na miaka Kama mitano hivi alianza kuongea kuhusu mambo yaliyotushangaza sana mimi na mke wangu..kuna wakati mmoja kulinyesha mvua ya rasharasha tu tukawa tunarudi home kutoka madukani naye..kawaida Kuna Ile harufu ya mchanga baada ya mvua ya aina hii kunyesha baada ya muda mrefu..sasa kilichonishangaza ni kuwa mwanangu alianza kusema kwamba anahisi harufu ya mungu..nikamwambia ni harufu ya mchanga tu Ila akawa mkali kidogo kwamba nakataa kukubaliana naye kuwa mungu hunukia hivo..tulipofika home lile Jambo likanifikilisha sana nikasema japo huenda ni upuuzi tu wa kitoto wacha nimwambie mke wangu..ndipo naye akaniambia kwamba kuna wakati kijana wetu alikuwa akimtayarisha kuenda shuleni kisha mtoto akamwambia kwamba anampenda sana na sio Kama mamake yule mwingine wa "nyumba iliozeeka"alisema kwamba yule mamake mwingine ni mkali na wakati mwingine hampi hata chakula kizuri..hili Jambo lilitushtua Sana na siku moja nikamwambia mwanangu anipeleke "nyumbani kwao huko kulikozeeka"

Yani nilishtuka mwanangu aliponiongoza hadi tunafika sehemu flani kuna jumba kubwa na ambalo kwa muonekano ni Kama lilijengwa miaka ya zamani na ambalo hamna anayeishi humo..japo hatukuingia nilishtuka sana.

Ilipita siku nyingi mwanetu akitupa shuhuda za mambo ya ajabu ajabu nasi tukawa tunaomba Mungu sana amuepushe na mambo ya kivile..Ila yaliendelea tu..

Siku moja nakumbuka ilikuwa jumapili fulani naelekea home mida ya saa tatu hivi usiku..nikawa nimepitia kwenye njia flani ambacho kipo katikati ya shamba kubwa na wakati ule limepandwa mhindi..niseme tu nilikuwa nimetoka kujipumzisha kidogo na marafiki kwa hiyo nilikuwa nimenyonya Guiness mbili hivi..ila nilipoinua macho kuangalia mbele nilishtuka kuna mwanamke mbele yangu na manukato yake nayahisi kabisa..alikuwa mrefu kidogo ana mwili wa kawaida tu nikimaanisha kimaumbile..alionekana kutembea Kama mtu aliyechoka sana kwa hiyo hakuwa anaharakisha..kilichonishangaza ni kwamba nilijitahidi sana kuharakisha nimkaribie yule mwanamke Ila ilishindikana..nikawa ni Kama vile nimesimama kabisa naye akawa bado anatembea..

Ni mambo mengi tu ila kwa sasa ni muda sana sijasikia mambo Kama hayo tena na namshukuru mungu sana..tukio la mwisho lilitokea 2004

Dah pole sana. Ila nakupongeza kwa ulezi mzuri wa kutopuuzia maneno aliokwambia mwanao na kumconvince akupeleke hio nyumba yake nyingine iliozeeka. Dah.
 
Isije ikawa mtoto alivotoa siri ndo wakaamua kumdhuru, I hope alikufa kwa mipango ya Mungu na sio kwajil ya Binadam waovu 🙁 nimeogopa mpk nimewasha tochi hapa kitandani sitoizima [emoji22]
sitoizima[emoji23][emoji23][emoji23] daah kumbe waoga tupo wengi. Mimi siwezi kulala giza totoro aisee tangu niko mdogo naogopa giza kama ukoma
Lazima ndani kwangu kuwe na chanzo cha mwanga.

lakini kuna siku huwa nasense tu kuwa leo siko okay nakua na woga tu yani saa ingine hata room zamani nilikua silali natoka naenda kulala sebleni kama niko room ntalala na taa sikuhio ntaangalia movie usiku kucha, na nikipitiwa usingizi ntakabwa mpaka nijute.Nikikasirika nikasononeka vitu vyangu vinavunjika au nadhurika mwenyewe
 
Ilikuwa mwaka 2009,Kuna siku nimelala nikawa naota kuwa nimepanda daladala kituo cha mwenge naelekea posta basi nikawa nimekaa siti ya nyuma ya Costa. Basi kufika kituo cha Victoria akapanda mdada mmoja akaja kukaaa karibu yangu siti ya nyuma,tukaendelea na Safari kufika kituo cha mbuyuni yule dada wa ndotoni akaniachia kikaratasi kina namba za simu akashukia kituo cha mbuyuni,baada ya mda nikastuka kutoka ndotoni kucheki saa ya simu mda huo ni saa tisa za usiku. Basi nimestuka kila kitu kwenye ndoto nilikuwa nakumbuka mpka namba za siku,kesho yake nawahadithia ndugu zangu nilichoota ndotoni na mpka namba za siku zilizokuwa kwenye karatasi nazikumbuka,wakaniambia tujaribu kuzipiga. Baada ya kupiga anapokea msichana ana lafudhi ya kiarabu anaitwa Nasrat na anaishi sinza,nilichofanya ni kuvunja laini na kutafuta line nyingine mpka leo sielew ile ndoto na coincidence zake
Alivyopokea alikufahamu? Au alikukumbuka?
 
sitoizima[emoji23][emoji23][emoji23] daah kumbe waoga tupo wengi. Mimi siwezi kulala giza totoro aisee tangu niko mdogo naogopa giza kama ukoma
Lazima ndani kwangu kuwe na chanzo cha mwanga.
lakini kuna siku huwa nasense tu kuwa leo siko okay nakua na woga tu yani saa ingine hata room zamani nilikua silali natoka naenda kulala sebleni kama niko room ntalala na taa sikuhio ntaangalia movie usiku kucha, na nikipitiwa usingizi ntakabwa mpaka nijute.Nikikasirika nikasononeka vitu vyangu vinavunjika au nadhurika mwenyewe

Dah pole sana.. Mimi siogopi giza na siwez kulala na Taa napenda iwe giza totoro, ila mara mojamoja nikipata mshtuko au uwoga wa gafla km jana ndo nawasha Tochi au Taa😂😂😂 Nilishtuka sana kusoma kwamba yule mtoto alifariki Dah imenifanya nifikirie kwamba mambo yalikua mazito sana,

Kwahio na ww ukipata hisia mbaya ukikasirika vitu vyako vinavunjika bila sababu?? Dah sijui kwanini haya mauzauza ya kichawi yapo Africa
 
yes nikikasirika vitu vinavunjika au naanguka naumia
Dah pole sana.. Mimi siogopi giza na siwez kulala na Taa napenda iwe giza totoro, ila mara mojamoja nikipata mshtuko au uwoga wa gafla km jana ndo nawasha Tochi au Taa[emoji23][emoji23][emoji23] Nilishtuka sana kusoma kwamba yule mtoto alifariki Dah imenifanya nifikirie kwamba mambo yalikua mazito sana,

Kwahio na ww ukipata hisia mbaya ukikasirika vitu vyako vinavunjika bila sababu?? Dah sijui kwanini haya mauzauza ya kichawi yapo Africa
 
Back
Top Bottom