Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

I.Huyo mwinjilisti alikushika mkono ndio mkakizunguka kiumbe? Mlikizungukaje kwa kushikana kama ni kirefu

Au alikushika usikimbie akakuachia mkakizunguka? Na hukukimbia tena? Sio rahisi

II. Hao wazee uliowaona bwenini ndio mwendelezo wa ulichokiona darasani?
Hapana darasani nilikuta kiumbe aina ya fisi maana mm nimeishi serengeti najua hao wanyama hutumika sana kwa nia ovu
 
Tulivyokiona alinishika mkono kwa maana nasiweweseke na kukimbia kutokana na mshtuko na kunipa ishara tukakizunguka kile kiumbe

Hicho kiumbe huwezi kukielezea hata kidogo wajumbe tupate haya picha flani kwenye mawazo yetu
 
mbn hujasema hicho kitu ulichokiona darasani? na kwann umwache ima aende wkt umeona kitu kisicho cha kawaida

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kiuhalisia nilitakiwa nimweleze ila nilihisi naweza kuwa nifikra au usingiz ila mwili ulisisimka nikaona ngoja nirud bwenini nisali kwanza ila baada ya yeye kuanguka nikajua haikuwa kuna shida kweli
 
Hicho kiumbe huwezi kukielezea hata kidogo wajumbe tupate haya picha flani kwenye mawazo yetu
Ni kiumbe aina ya binadamu ila ni mrefu asie na mwisho eneo hilo kuna miti aina ya girivelia na huyo kiumbe alionekana kupita kimo cha miti hiyo ila wenyeji baada ya kueleza wao wanaita kabhebba very dangerous kama utakutana nacho na ukaamua kukimbia wanasema lazma kikudhuru
 
Hapo sawa Maelezo yamekamilika ila yameleta swali jingine, kwamba hicho kiumbe ukikutana nacho unachotakiwa ni kukausha kama hujaliona na kuendelea na mambo yako?
 
Hapo sawa Maelezo yamekamilika ila yameleta swali jingine, kwamba hicho kiumbe ukikutana nacho unachotakiwa ni kukausha kama hujaliona na kuendelea na mambo yako?
Kulingana na uzoefu wa wenyeji
Ila nikiwa shuhuda huko huko tulizika watu wawili vifo vya kutatanisha nikiwa msibani taarifa zieleza watu hao walikutana na hicho kiumbe na wakakimbia maana wote nilioshuhudia vifo vyao walikutwa hawajajeruhiwa ila walifia mlangoni
 
Hili nimethibitisha. Wach nitakuja andika hapa niliyoshuhudia wilayani Musoma kipindi nakaa nyarigamba
1-Kuhusu Mbwa:
Miaka ya 1998 tukiwa tunaishi nyarigamba wilayani Musoma, brother angu alikua mtu wa club na mashangwe sana.

Siku moja akiwa anarudi home akaokota kitoto cha mbwa wa kizungu (enzi hizo hatujui breed , sisi tunajua tu mbwa wa kizungu) . Akampa jina la BEACH/BITCH kwa kuwa alimuokota akiwa anatoka nadhani ni Palm Beach.

Yule mbwa alikua mdogo ila mtata balaa. Mbwa wa size ya paka ila anakukitia na harudi nyuma. Basi kipindi hicho wanga walikua wanatupa daily visits za kutosha. Basi kale kadogi kakawa kama kikwazo.wajuba wakitimba kinauwasha balaa tunaamka.

Siku moja kakapotea kiajabu, tukakatafuta for two days, chenga. Siku moja kwa wanokajua wakasema wamekaona kwenye pagala karibu na zahanati ya makoko, daah tukaenda tukakuta jamaa wamekapaka mavi ya binadamu mwili mzima. Alafu wamekatoa meno yote mdomoni.

Tulijitahidi kuhudumia ila kalikufa kwa kushindwa kula.

2-Miti kuungua moto.

Usiku tulikua tukienda kukojoa choo cha nje (mana nyumba haikua self) ilikuwa ni kawaida kukuta miti mikubwa ya jirani na home inawaka moto mkubwa kabisaa. Ila cha ajabu asubuhi mti upo green vilevile.

3-sasa kali siku niliyovutwa kutoka kitandani mpaka chini.

Tulikua tunalala mimi na brother angu Niliyemfuatia (Mungu Amrehemu na amuweke pema) sasa kwa uwoga timing ikawa ni kuwahi kulala upande wa ukutani wa kitanda.

Siku hiyo bhana akaniwahi yeye, mimi nikawa ndio upande wa mlangoni.

Movie linaanza kama saa 7 hivi nikasikia Dirisha la Stoo linafunguliwa (tulikua tunakaa nyumba ya mwalimu shule ya nyarigamba)

Kisha mtu akaanza kutembea juu ya mabati na makorokoro yaliyopo stoo. Akaendelea kusogea mpaka akafika coridor ya sebuleni nasikia hatua zake zikiongezeka kuja chumbani. Cha ajabu hapo hata nguvu ya kuita au kupiga kelele sina hapo nimejikunja ndani ya shuka kama korosho

Akaendelea kutembea mpaka anafungua mlango wetu , akaanza kunivuta. Kila nikijitahidi sauti haitoki. Nikapambanaa mpaka bahati sauti ikatoka kupiga yowe akaniachia akakimbikia njia ile ile ya stoo.

Ndugu kuja wakaniuliza vipi nikawasimulia, wakaniambi walisikia zile hali za mabati kugusana gusana stoo ila hawakupata hilo wazo.

Nitarudi tena
 
1-Kuhusu Mbwa:
Miaka ya 1998 tukiwa tunaishi nyarigamba brother angu alikua mtu wa club na mashangwe sana.

Wachawi wapumbavu sana.
 
Wachawi wapumbavu sana.
Ni wajinga balaa.

Sasa kuna mmoja kwenye ukoo wetu, alikua anapeperuka balaa.

Mara paaap, siku ya kufa nyani. Buanaaa weee akaingia kwenye Anga la utawala wa NATO akagusa nyumba nzito.

Akapigwa kubwa kuliko aisee. Nyakati zake mwisho aliishi kwa mateso. Ikafika kipindi akaanza kutaja wenzake. (Mmojawapo nin uhusiano nae wa damu kabisa)

Walivyooona ivo wakamzima akawa haongei ghafla mpaka akavuta.
 
Nilipogundua waganga na wachawi ni wana tu.

Baada ya kupata kibarua cha kwanza na mshahara kuwa mdogo sana nilikuja kukaa dar kwa ndugu yangu .

Basi majombii yalikua yanamchezesha balaa. Mara kunyolewa, mara kupigwa chale yan ili mradi vurugu tu.

Akasema kuna mganga anafahamiana nae hivyo hana hata malipo ikabid twende akatupige kijikinga. Sikua na namna kwa kuwa naishi hapo tukaenenda mitaa ya vingunguti huko.

Phase1; Kufika bhana mida ya saa moja jioni, tukapewa madawa yamewekwa kwa maji kila mtu akaenda kuoga tukaambiwe tukalale , tutaanza kuroga mida ambayp wachawi wanatoka.

Phase; mida ya saa 7 usiku nikaamshwa. Nikawekwa kwenye kistuli, nakuta mganga kapandisha majini anafoka foka tu. Daaah.
Nikaambiwa nigeukie Kibla (nanukuu , hili lisihusishwe na dini tafadhali) nikawa sielwi elewi nikaelekezwa chap.

Gongwa chale kadha wa kadha na midawa inawashaaa. Fala yule sijui alitupaka pilipili.

Zoezi likafanyika kwa wote.

Phase3 : kuingia ndani kwenda malizia tulale sasa, ukaanza upepo mmoja sio wa kawaida unaingia ndan ya nyumba. Ikawa juu ya bati kama kuna disco wat wanacheza. Varangat mtindo mmoja.

Yule mganga akatoka na madawa na vifaa vyake nje, piga ndumba sana mpaka hali ile ikapotea.

Akarudi akatuambia ni hao washua wanaotupatiaga kichapo ndio wamekuja kumuomba kuwa wanegotiate atupe kidawa uchwara alafu baada ya muda waendele kutupa mbata kama kawa na wamemuahidi pesa. Ila akadai kawagomea.

Tukamaliza, kesho yake tukarudi home. Hali ikatulia ila baada ya muda wale wachawi sijui walireceive Major updates sijui walitumia VPN gani moto ukawa pale pale.
 
Najua umekubali kuepusha ubishi lakini rohoni bado una amini ilikuwa nguvu za giza au mazingara ya kichawi au majini.

Siyo lazima niwe sahihi nadharia yangu, lakini nilikuwa najaribu kuelezea uwezekano wa hilo kutokea kisayansi ya baiolojia, maana sleep walking ni tatizo la kibaiolojia kwamba kuna sehemu ya ubongo wako iliyotakiwa kulala/kupumzika ilikuwa bado inaendelea kufanya kazi.
Ilitakiwa sehemu ya ubongo inayo husika kuwezesha viungo vyako kama limbs zisifanye kazi nayo ilale kama sehemu zingine za ubongo, ibakie sehemu ya ubongo ile ya kufanya kazi za msingi za upumuaji na kusukuma damu.

CC: Carleen njoo unikosoe baiolojia huku, mimi sikusoma kabisa Biology elimu ya upili au kokote zaidi ya shule ya msingi St. Kayumba.
Inataka kufanana na sleeping paralysis. Aisee hiyo kitu ni noma...
 
Back
Top Bottom