Hili nimethibitisha. Wach nitakuja andika hapa niliyoshuhudia wilayani Musoma kipindi nakaa nyarigamba
1-Kuhusu Mbwa:
Miaka ya 1998 tukiwa tunaishi nyarigamba wilayani Musoma, brother angu alikua mtu wa club na mashangwe sana.
Siku moja akiwa anarudi home akaokota kitoto cha mbwa wa kizungu (enzi hizo hatujui breed , sisi tunajua tu mbwa wa kizungu) . Akampa jina la BEACH/BITCH kwa kuwa alimuokota akiwa anatoka nadhani ni Palm Beach.
Yule mbwa alikua mdogo ila mtata balaa. Mbwa wa size ya paka ila anakukitia na harudi nyuma. Basi kipindi hicho wanga walikua wanatupa daily visits za kutosha. Basi kale kadogi kakawa kama kikwazo.wajuba wakitimba kinauwasha balaa tunaamka.
Siku moja kakapotea kiajabu, tukakatafuta for two days, chenga. Siku moja kwa wanokajua wakasema wamekaona kwenye pagala karibu na zahanati ya makoko, daah tukaenda tukakuta jamaa wamekapaka mavi ya binadamu mwili mzima. Alafu wamekatoa meno yote mdomoni.
Tulijitahidi kuhudumia ila kalikufa kwa kushindwa kula.
2-Miti kuungua moto.
Usiku tulikua tukienda kukojoa choo cha nje (mana nyumba haikua self) ilikuwa ni kawaida kukuta miti mikubwa ya jirani na home inawaka moto mkubwa kabisaa. Ila cha ajabu asubuhi mti upo green vilevile.
3-sasa kali siku niliyovutwa kutoka kitandani mpaka chini.
Tulikua tunalala mimi na brother angu Niliyemfuatia (Mungu Amrehemu na amuweke pema) sasa kwa uwoga timing ikawa ni kuwahi kulala upande wa ukutani wa kitanda.
Siku hiyo bhana akaniwahi yeye, mimi nikawa ndio upande wa mlangoni.
Movie linaanza kama saa 7 hivi nikasikia Dirisha la Stoo linafunguliwa (tulikua tunakaa nyumba ya mwalimu shule ya nyarigamba)
Kisha mtu akaanza kutembea juu ya mabati na makorokoro yaliyopo stoo. Akaendelea kusogea mpaka akafika coridor ya sebuleni nasikia hatua zake zikiongezeka kuja chumbani. Cha ajabu hapo hata nguvu ya kuita au kupiga kelele sina hapo nimejikunja ndani ya shuka kama korosho
Akaendelea kutembea mpaka anafungua mlango wetu , akaanza kunivuta. Kila nikijitahidi sauti haitoki. Nikapambanaa mpaka bahati sauti ikatoka kupiga yowe akaniachia akakimbikia njia ile ile ya stoo.
Ndugu kuja wakaniuliza vipi nikawasimulia, wakaniambi walisikia zile hali za mabati kugusana gusana stoo ila hawakupata hilo wazo.
Nitarudi tena